1. Habari2. Taifa

NAMA yaingia makubaliano na Taasisi 14, shule 21

Taasisi ya NAMA Foundation ya nchini Malaysia imeingia katika makubaliano ya ushirikiano wa kikazi na asasi za kiraia 14 pamoja na shule 21 za hapa nchini.

Utiaji saini wa makubaliano hayo mefanyika katika ofisi za An-Nahl Trust Mikocheni jijini Dar es swalaam ambapo Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya NAMA Integrated Centre for Excellence (NICE) ambayo ni taasisi mwenza ya NAMA Foundantion, Mfaume Mkanachapa, amesema lengo la makubaliano hayo ni kuzijengea uwezo taasisi hizo za kiraia pamoja na shule ili ziweze kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zao.

Mkanachapa alisema moja ya vipengele vya makubaliano hayo ni kupata walimu wenye sifa na uwezo wa kutoa taaluma bora katka shule husika.

NAMA Foundation imekuwa ikifanya kazi na asasi mbalimbali za kiraia hapa nchini na makubaliano hayo ni muendelezo wa shughuli za taasisi hiyo hapa nchini.

Akifafanua zaidi kuhusu makubaliano hayo, Mkurugenzi huyo alisema kuwa, wanategemea kuingia katika makubaliano kama hayo na taasisi nyingine hapo baadae ili elimu na utoaji huduma za kiraia hapa nchini.

Miongoni mwa asasi za kiraia zilizosaini makubaliano hayo na NAMA ni pamoja The Islamic Foundation (TIF) yenye makao yake makuu mjini Morogoro ambapo Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya TIF, Musa Buluki alitaja kuwa, hii ni hatua nzuri katika kukuza ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.

Licha ya faida nyingine, kwa mujibu wa Buluki, makubaliano hayo yatasaidia kuboresha utoaji elimu katika shule zilizoko chini ya TIF. Miongoni mwa shule zinazomilikiwa na TIF ni Sekondari ya miaka mingi ya Forest Hill ya mjini Morogoro.

Kwa upande wao, viongozi wa asasi na shule nyingine, licha ya TIF, zilizosaini makubaliano hayo wameishukuru Taasisi ya NICE na NAMA Foundation wakisema makubaliano hayo ni hatua kubwa katika utoaji wao wa huduma kwa walengwa

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close