1. Habari1. TIF News

Kuelekea Kongamano la Misk ya Roho

WAISLAMU Nchini wametakiwa kuunga mkono na kuwa mstari wa mbele kujitolea katika masuala ya Dini na sio kubeza baadhi ya mada zitakazowasilishwa na Masheikh mbalimbali kwenye Makongamano ya Dini.

Hayo yameelezwa na Sheikh Nurdin Kishki katika kipindi Maalumu kilichoangazia Kongamano la kwanza la afrika Mashariki chini ya Taasisi ya The Islamic Foundation la Misk ya Roho litakalo fanyika siku ya Jumapili ya Tarehe 26 mwezi Novemba Mwaka 2017 Katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam kilichoruka Mubaashara katika vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Taasisi ya The Islamic Foundation iliyopo Mjini Morogoro

Aidha  Sheikh Nurdini kishki amewataka Waislamu kuunga mkono katika jitihada zinazofanywa na Taasisi za Dini ya Kislamu ikiwemo Taasisi ya TIF zinazouendeleza Uislamu mbele ili kuufahamu Uislamu wao Kiusahihi.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Matukio mbalimbali ya Taasisi ya TIF Tajmohamed Abbas na Sheikh Nurdin Kishk wamezungumzia kuhusiana na uwasilishwaji wa mada zitakazo wasilishwa katika Kongamano la Miski ya Roho wameelezea jinsi ya kuwa na Ikhlaas na umuhimu wa elimu na thamani ya amani kwa kuwaondoa utondoti baadhi ya watu wanaona kuwa mada hizo zimezoeleka na hapa wanabainisha.

Katika Hatua nyingine Mwenyekiti Aref Nahdi amelizungumzia suala la gharama za ukodishaji wa ukumbi wa Diamond Jubilee ambao ndio utakaofanyika Kongamano la Misk ya Roho na kuwataka waislamu kutokuona uzito kutoa shilingi 5000 za kununua tiketi yakuingilia ukumbini

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close