3. Kimatiafa

Warohingya Waitaka EU Kuunga Mkono Uchunguzi Wa UN

Kundi linalowakilisha jamii ya Waislamu wachache wa Rohingya nchini Ulaya limeutaka Umoja wa Ulaya (EU) kuunga mkono uchunguzi wa Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu uhalifu wanaotendewa wa Rohingya. Baraza la Ulaya la Warohingya (ERC) linasema kuwa inahuzunisha sana juu ya uamuzi wa EU wa kutounga mkono uchunguzi wa UN. Ripoti iliyotolewa inaonesha kuwa mwezi uliopita EU iliamua kutounga mkono uchunguzi wa kimataifa unaopendekezwa na kamishna wa UN juu ya haki za binadamu, alisema Zeid Ra’ad alHussein. Kwa mujibu wa Ra’ad al-Hussein, taarifa mbali mbali za haki za binadamu zinaonesha ukiukwaji mkubwa wa haki na uhalifu dhidi ya binadamu na kuhitaji uangalizi wa Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu (ICC). Wakati wa operesheni hiyo, UN na makundi ya haki yalitoa ushahidi wa unyanyasaji wa maafisa wa usalama kama vile kuua watoto na vichanga, kubaka, kupiga kikatili na kuchoma vijiji, inasema ripoti. “Tunausihi mno Umoja wa Ulaya kubatilisha uamuzi wake na kuunga mkono uchunguzi unaoendeshwa na Umoja wa Mataifa juu ya uhalifu wanaofanyiwa wa Rohingya na vikosi vya Myanmar,” inasema ripoti hiyo . Serikali ya Myanmar hairuhusu vyombo vya habari vya kimataifa kuingia eneo lililoathiriwa la Rakhine pia haitaki kutoa ushirikiano kwa UN kuchunguza mauaji, ubakaji na kamata kamata dhidi ya Warohingya. Warohingya hawatambuliki kuwa miongoni mwa makabila 135 ya Myanmar huku Serikali ikidai kuwa watu hao ni raia kutoka Bangladesh.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close