3. Kimatiafa

Ustaarabu wa Magharibi unavyotishwa na hijab!

Said Rajab K ama kulikuwa na s h a k a y o y o t e kwamba Waislamu hawatakiwi barani Ulaya, sasa jambo hilo limetungiwa sheria na Mahakama ya Ulaya. Uamuzi wa majaji wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kuwaruhusu waajiri barani humo kuwapiga marufuku wafanyakazi wao kuvaa Hijab, umekuja kufuatia harakati za muda mrefu za kuwazuia wanawake wa Kiislamu kuvaa Hijab. Sasa, Mahakama ya Ulaya, ambayo ni ya juu kabisa barani humo, imefungua mlango wa chuki dhidi ya Waislamu, ikiwalazimisha wanawake wa Kiislamu kuchagua kati ya maadili yao au kazi. Mahakama ya Jumuiya ya Ulaya (ECJ) imesema haichukulii kama ‘ubaguzi wa moja kwa moja’ iwapo kampuni ina kanuni ya ndani inayopiga marufuku mavazi yoyote yenye alama ya ‘kisiasa, kifalsafa au kidini.’ Mahakama hiyo imetoa hukumu kwenye kesi za wanawake wawili, nchini Ufaransa na Ubelgiji, ambao walifukuzwa kazi kwa kukataa kuvua Hijab zao. Sarakasi za kitaaluma zinazotumika kuhalalisha marufuku hiyo zitakuwa kichekesho, kama jambo hilo lisingekuwa zito. Ili mradi makampuni yatawapiga marufuku wanawake wote wanaovaa Hijab, basi jambo hilo halitachukuliwa kuwa ni ubaguzi! Marufuku ya Hijab, ambayo imefichwa kwenye marufuku ya alama za ‘kisiasa, kifalsafa na kidini,’ sasa ni moja tu kati ya orodha ndefu ya matukufu ya Kiislamu , ambayo yamepigwa marufuku ili kulinda maadili ya Kimagharibi. Katika majiji y o t e y a U l ay a , ukiondoa Istanbul, huwezi kusikia adhana ya nje. Tunashuhudia wazi kifo cha mfumo wa maadili wa Kimagharibi, ambao umeshindwa kabisa kushughulikia au k u k a b i l i a n a n a changamoto mpya z i n a z o l e t w a n a mazingira ya kimataifa. Viongozi haohao wa Ulaya, ambao wanajifanya kupinga ‘ubaguzi’ wa wanawake katika jamii za Waislamu, sasa hawaoni kinyongo kutumia sera za kibaguzi dhidi ya wanawake wa Kiislamu ndani ya nchi zao. Katika jitihada za kulinda maadili ya Kimagharibi, tumeona Guantanamo Bay, Belmarsh, Abu Ghraib, Bagram, Patriot Act, Sheria za kupinga ugaidi, mateso wakati wa mahojiano, udhalilishaji wa kingono, kuweka Waislamu gerezani bila mashitaka na mengine mengi yasiyopendeza kama hayo. Mpaka miaka ya hivi karibuni, wanasiasa wengi katika nchi za kisekula wamehalalisha sheria za kuwakandamiza Waislamu kwa kisingizio cha usalama wa taifa. Lakini leo, Hijab, kipande cha nguo kinachovaliwa na wan a w a k e w a Kiislamu kichwani, kwa maana ya kusitiri mwili, kinautisha ustaarabu wa M a g h a r i b i m p a k a wabunge wanalazimika kutunga sheria kukipiga marufuku! Wanaogopa kipande cha nguo!! Ndugu zangu katika imani, hiyo ndiyo nguvu ya Uislamu. Mataifa makubwa yenye nguvu za kinyuklia yanatishwa na vazi la Hijab, linalovaliwa na mwanamke wa Kiislamu! Vazi lenyewe hawavai wao wala hawalazimishwi kulivaa! Hijab tu imewapa changamoto nzito ya Kiustaarabu, mpaka wameamua kuipiga marufuku! Pamoja na propaganda zao zote mbaya dhidi ya Hijab, wameshindwa kabisa kumvua mwanamke anayejitambua wa Kiislamu vazi hili tukufu. Na huo ndiyo ubora wa ustaarabu wa Kiislamu, ukilinganishwa na Umagharibi. Hawawezi kuwavua Hijab wanawake wa Kiislamu kwa kutumia hoja wala ushawishi, bali kwa kutumia nguvu, ubabe, sheria, unyanyasaji au udhalilishaji. Nukta ya kuzingatia hapa ni kwamba hawaogopi Hijab tu kama vazi, bali wanachoogopa ni kile kinachowaamrisha wanawake wa Kiislamu kuvaa Hijab – Uislamu.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close