3. Kimatiafa

UNICEF: 2016 Ulikuwa Mwaka Hatari kwa Watoto Syria

Watoto nchini Syria walikuwa na wakati mbaya mwaka jana ambapo wengi wao waliuawa kuliko miaka yoyote ile tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, linasema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia Watoto Duniani (UNICEF). Mwaka jana, takribani watoto 652 waliuawa, kati yao watoto 255 waliuawa ndani au karibu na shule ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ya watoto waliouawa mwaka 2015, ilisema taarifa ya Unicef. Takwimu hizo zinajumuisha vifo vilivyothibitishwa ikiamanisha kuwa huenda idadi ikawa kubwa zaidi ya hiyo. Unicef inaamini kuwa zaidi ya watoto 850 waliandikishwa ili kupigana vita vya mwaka jana. Idadi hii ni mara mbili ya mwaka 2015, ripoti inasema hiyo. Watoto walioandikishwa waliwekwa mstari wa mbele wa mapigano, walitumika kunyonga, kujitoa muhanga na kulinda magereza. “Kiwango hiki cha mateso hakijawahi kutokea,” alisema Geert Cappelaere, Mkurugenzi wa Unicef, kanda ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika akiwa mji wa Homs, Syria. Mamilioni ya watoto Syria wanavamiwa kila siku, maisha yao yameharibiwa vibaya.” Watoto zaidi ya milioni 6 kwa sasa wanaishi kwa kutegemea misaada ya kibinadamu kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimedumu kwa wiki sita. Baadhi ya watoto Milioni 2.3 wamekimbia nchi lakini walioathiriwa zaidi ni Milioni 2.8 walionasa katika maeneo yasiofikika kirahisi na 280,000 wanaoishi kwenye mzingiro wa kijeshi, Unicef inaripoti.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close