3. Kimatiafa

Syria Yanyonga Watu 13,000

  • Ni katika gereza la mateso

S hirika la Kimataifa la Haki za Binadamu (Amnesty International) limeripoti kuwa Serikali ya Syria imewanyonga jumla ya watu 13,000 kwa kipindi cha miaka minne tangu hapo mwaka 2011. Shirika hilo linadai kuwa matukio hayo ya unyongaji yalifanyika katika jela ya kijeshi ya Saydnaya kaskazini mwa mji wa Damascus kuanzia Septemba mwaka 2011 hadi Decemba mwaka 2015 huku watu wanaoshikiliwa wakisema kuwa gereza hilo ni machinjio. Kutokana na hali hiyo, shirika hilo limetoa wito kwa nchi ya Marekani na Urusi kutumia ushawishi wao ili kuhakikisha kuwa Serikali ya Rais Bashar Al – Assad inaruhusu wachunguzi huru kuingia ndani ya gereza hilo. Amnesty inasema kuwa ndani ya gereza hilo kuna vitendo vya uhalifu dhidi ya binadamu. Taarifa ya Shirika hilo inasema kuwa kati ya watu 20-50 wamekuwa wakinyongwa nyakati za usiku kila wiki na wengine kufariki kutoka na mateso ikiwemo kunyimwa chakula, maji, dawa na huduma za afya. Wanaoshikiliwa wanadhani kuwa wanasafirishwa katika magereza ya kiraia na hawajui kama watanyongwa na wanaofariki huzikwa katika makuburi ya pamoja, liliripoti shirika hilo. Wanaume na wanawake wamekuwa wakibakwa, huku wanawake wakilazimishwa kukiri makosa kwa vitisho vya kubakwa mbele ya ndugu zao, ripoti hiyo inasema. Taarifa hizo zimepatikana kutokana na mahojiano ya baadhi watu wakiwemo wafungwa wa zamani na walinzi wa jela hiyo. Serikali ya Syria inayoungwa mkono na utawala wa Kishia wa Iran na Urusi, imekuwa ikipambana makundi ya wapinzani kutokana madhehebu za Kisunni ambayo yanapinga utawala wa Assad wanaouita kuwa ni wa kidhalimu.

 

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close