Matukio

Tuikumbuke srebrenica baada ya miaka 24!

Miaka 24 imepita tangu mauaji ya kimbari ya zaidi ya Waislamu 8000, wakiwemo watoto, vijana, wazee, wanawake na wanaume, wenye umri kuanzia chini ya miaka 7 mpaka zaidi ya miaka 70, kwenye mji wa Srebrenica, Bosnia, mikononi mwa jeshi la Serbia.

mauaji yale ya kimbari yalikiuka kwa kiasi kikubwa “heshima ya ubinadamu, uhuru, demokrasia na usawa” huku NATO ikiwa imebaki kimya na kutofanya maamuzi, licha ya kuwa na taarifa kamili kwamba mauaji ya kutisha ya kimbari yangetokea siku chache zijazo.

Miaka 24 imepita tangu mauaji ya kimbari ya zaidi ya Waislamu 8000, wakiwemo watoto, vijana, wazee, wanawake na wanaume, wenye umri kuanzia chini ya miaka 7 mpaka zaidi ya miaka 70, kwenye mji wa Srebrenica, Bosnia, mikononi mwa jeshi la Serbia.

Julai 11, mwaka 1995, miaka mitatu tu tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Bosnia, wapiganaji wa Kiserbia, wakiongozwa na Jenerali Ratko Mladic, waliingia kwenye mji wa Mashariki wa Srebrenica, baada ya mji huo kutangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni eneo salama, ‘linalolindwa’ na askari 600 wa jeshi la kulinda amani kutoka Uholanzi, waliowekwa pale na Umoja wa Mataifa.

Wakiwa hawana ‘uwezo’, ‘hawataki’ au ‘wamepuuza’ tu, walinzi wale wa amani waliowekwa na Umoja wa Mataifa, waliwaruhusu wapiganaji wa Serbia kuingia kwenye ‘eneo salama’ ambalo halikuwa na silaha na kufanya mauaji ya kutisha ya raia, wakisaidiwa na hali ya kutojali ya Jumuiya ya Kimataifa.

Katika kumbukizi ya miaka 24 ya mauaji haya ya kutisha mwishoni mwa karne ya 20, mauaji ya kinyama mabaya zaidi kuwahi kutokea katika ardhi ya Ulaya tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametaka kulaaniwa kwa uhalifu huu wa kutisha, pamoja na hali ya kutochukua hatua ya Jumuiya ya Kimataifa. Amesema: “Jumuiya ya Kimataifa, na hususan Umoja wa Mataifa, umekubali sehemu yake ya lawama na umefanya juhudi kubwa ya kujifunza kutokana na mafunzo yaliyopatikana kufuatia kushindwa kwake kuchukua hatua.”

Katika taarifa iliyotolewa na Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Jumuiya ya Ulaya na Kamishna, Johannes Hahn, mauaji yale ya kimbari yalikiuka kwa kiasi kikubwa “heshima ya ubinadamu, uhuru, demokrasia na usawa” huku NATO ikiwa imebaki kimya na kutofanya maamuzi, licha ya kuwa na taarifa kamili kwamba mauaji ya kutisha ya kimbari yangetokea siku chache zijazo.

Ikumbukwe kuwa, ni baada ya ahadi ya Jumuiya ya Kimataifa ya kuwalinda raia kutangazwa, ndipo wapiganaji wa Bosnia waliokuwa wakiulinda mji huo waliposalimisha silaha zao. Hali hii ilitoa mwanya wa kutokea kwa mauaji ya kimbari yasiyo na upinzani wa Waislamu, ambapo taarifa zinasema kulikuwa pia na matukio mpaka 50,000 ya ubakaji na udhalilishaji wa kingono.

Waathirika wa unyama huo bado wanafukuliwa kutoka kwenye makaburi ya pamoja yaliyofichwa maeneo mbalimbali mpaka leo. Taarifa zilizokuwa za siri za CIA zinafichua kwamba Uingereza na Marekani zilijua kuhusu mauaji haya ya kimbari ya Waislamu mjini Srebrenica wiki sita kabla. Wakati wa kumbukizi ya miaka 22 ya mauaji ya kimbari ya Srebrenica mwaka 2017, Mkurugenzi wa Shirika moja Kiislamu la Misaada kutoka nchini Uingereza, CAGE, bwana Moazzam Begg, alisema: “Mwaka 1994, nilifanya safari yangu ya kwanza kati ya nyingi ya kupeleka misaada kwa watu wa Bosnia na Herzegovina na kuwasaidia kuuhami Uislamu. Kama walivyokuwa wengi wengine, niliogopeshwa mno na mauaji, mateso na ubakaji wa watu wengi, uliofanywa dhidi ya Waislamu wa Bosnia, katika kambi maalumu za mateso kama Omarska, Trnopolje na Uzamnica”

Haya yote yalitokea kabla ya mauaji ya watu 8000 pale Srebrenica – mahali ambapo Waislamu wa Bosnia waliotawanyika kutokana na vita, walitafuta hifadhi kwa sababu palishatangazwa kuwa ni eneo salama, chini ya ulinzi wa askari wa Uholanzi walio katika Umoja wa Mataifa.

Leo, katika ulimwengu wa baada ya “Ugaidi wa ISIS”, ni ukumbusho unaohitaji mazingatio makini, kwamba mauaji makubwa zaidi ya kimbari dhidi ya raia wasio na hatia barani Ulaya, tangu vita Kuu ya Pili ya Dunia, yamefanywa na watu wanaojinasibisha kama wafuasi wa Ukristo na Usekula Pamoja na hasara kubwa isiyoelezeka iliyowapata waathirika wa vita vya Bosnia na jamaa zao, hatupaswi kusahau kwamba wale ambao leo wanajidai kuwa watetezi wakubwa wa haki za binadamu na utawala bora, walisimama tu na kuangalia wakati binadamu wakiangamizwa! Pengine kwa tafsiri yao, Waislamu siyo binadamu!

Show More

Related Articles

Back to top button
Close