Matukio

Nunueni tiketi ‘Misk ya Roho’ mapema kuepuka usumbufu

Ikiwa imesalia takribani wiki moja na nusu kufanyika kwa kongamano la pili la Misk ya roho hapa nchini, Waislamu wamehimizwa kukata tiketi mapema ili kuondokana na usumbufu wa kinyang’anyiro cha tiketi siku ya mwisho.

Uzoefu wa makongamano yaliyopita unaonresha kuwa, baadhi ya watu waliosubiri kukata tiketi siku za mwisho walikosa tiketi na hivyo kujikuta wakijuta. Akizungumzia maendeleo ya mauzo ya tiketi, Meneja Mauzo, Limbanga Limbanga alisema watu wengi tayari wamejitokeza kununua tiketi zao, na kwamba iwapo kasi ya ununuzi wa tiketi ikiendelea kama ilivyo sasa, kunaweza kuwa na uhaba katika siku za mwisho.

Waislamu waje mapema kununua tiketi ili wawe na uhakika wa kuja kupata maneno mazuri ya walinganiaji waliobobea katika tamasha hili la pili la Misk ya Roho,” alisema Limbanga.

Kwa nini kiingilio?

Akijibu hoja za baadhi ya watu kwa nini kongamano hili ni la kulipia, Limbanga alisema, kiingilio cha shilingi 5,000 kimewekwa ili kuwapa Waislamu fursa ya kutoa sadaka zao na kuchangia gharama za maandalizi ya tukio hilo kubwa la Afrika Mashariki linalobeba ujumbe mtukufu wa dini tukufu ya Uislamu.

Pia, Limbaga alisema ikumbukwe kuwa kwa watakaokuja kwenye tamasha hilo watapewa chakula, ambacho gharama yake huenda ni kubwa kuliko hata hicho kiingilio. Kadhalika, Limbaga alisema wale watakaobaki nyumbani bado pia wanaweza kufuatilia kongamano hilo kupitia runinga na redio, ikiwemo Imaan.

Namna ya kupata tiketi

Limbanga aliendelea kuwakumbusha Waislamu vituo zinapopatikana tiketi za kongamano hilo kuwa ni Kanzu Point, Anezylitta Design (City Mall), GGS Bolts & Nuts (Livingstone Kariakoo), Ibn Hazm Book Store-(Kinondoni Mtambani), Car Centre (Morocco-Kawawa Road), Yakub Jewellers (Mikocheni Shoppers Plaza), Taste Me (Dar Free Market), Street Soul (Mlimani City), Masjid al-Jumaa (Gongo la Mboto) na Masjid Al-Irshaad (Tandika Chitoha).Vituo vingine ni Magomeni Kichangani (Piga namba 0714541957), Mbagala Rangi tatu Sokoni (0715328512) na Buguruni kwa Mnyamani (0655 611 248).

Hata hivyo, Limbaga alisema, kwa urahisi zaidi, mtu anaweza kununua tiketi kupitia mitandao ya simu ya Tigo Pesa kwa namba 0718 000 433 na M-Pesa kwa 0742 877 775 huku jina la namba hizo Tajmohamed Shaaban. Akitoa maelezo juu ya namna ya kununua tiketi mtandaoni, Limbaga alisema, mtu anachotakiwa kufanya ni kutuma pesa kiasi cha shilingi 5,000/= kwenda katika moja ya hizo namba mbili (aidha ya tigo au ya voda) kisha atume namba yake ya simu na majina yake kamili kwenda kwa namba hiyo hiyo, na baada ya hapo atapokea ujumbe mfupi wenye namba yake ya tiketi. Baada ya kupokea ujumbe huo, mtu anatakiwa kuutunza ujumbe huo mpaka siku ya kongamano.

Naye Meneja Makongamano wa Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF), akizungumzia kongamnao hilo linalosubiriwakwa hamu, alisema:

Maandalizi yanaendelea vema mpaka sasa, hivyo Waislamu wajiandae kupata ujumbe mzito juu ya dini yao siku hiyo.”

Taj anaongeza kuwa Waislamu hawana budi kuhudhuria kongamano hilo kwani lina tija kubwa sana kwao katika kuijua dini yao ili waishi maisha yanayofuata muongozo wa Uislamu na kuwa na maisha mema Akhera.

Misk ya roho 2018

Kongamano hili la pili la Afrika Mashariki lijulikanalo kama Misk ya Roho 2018 /1440H limebeba anuani ya maudhui ijulikanayo kama “Utukufu Wake…” na litafanyika Octoba 28, 2018 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Imetajwa kuwa watu watakaohudhuria kongamano hilo watanufaika kwa mada mbalimbali zitakazowasilishwa na masheikh ambazo kwa kiasi kikubwa zitazungumzia Utukufu Wa Mfalme Wa Wafalme (Allah), jinsi ya kumpwekesha, kuyajua majina na sifa zake na jinsi ya kuyatumia katika maisha ya kila siku ili kupata kufaulu.

Masheikh walioalikwa kuhudhurisha mada siku hiyo ni Sheikh Dourmohamed Issa kutoka Tanzania, Sheikh Ally Jumanne kutoka Tanzania, Sheikh Abdulrahman Mhina (Baba Kiruwasha) kutoka Tanzania. Wengine ni Sheikh Yusuf Abdi kutoka Kenya, Sheikh Jamaldin Osman kutoka Kenya, Sheikh Zuberi Bizimana kutoka Burundi, Sheikh Ally Kajura kutoka Rwanda na Sheikh Muhammad Abduweli kutoka Uganda.

Kongamano hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa 2 asubuhi na kuisha saa 11 jioni ambapo litaambatana na anasheed pamoja na huduma ya chakula na vinywaji kwa wahudhuriaji. Kwa undani zaidi wa habari za kongamano hilo zinapatikana katika tovuti ya TIF kwa anuani ya www.islamicftz.org/miskyaroho pia mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na Twitter @Islamicftz au simu namba 0653 949 306 (Wanaume tu) au 0625 628 542 (Wanawake tu).

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close