Matukio

Mwenye matatu ameonja ladha ya Imani, Sheikh Bizimana

Imeelezwa kuwa ili mtu aonje ladha ya Imani, hana budi kumpenda zaidi Allah na Mtume wake, kuwapenda watu kwa ajili ya Allah na kuchukia ukafiri.

Sheikh Zuberi Bizimana, Mhubiri na Mlinganiaji wa dini ya Kiislamu kutoka nchini Burundi, ameyasema hayo hivi karibuni wakati wa kongamano la kida’awa la Afrika Mashariki lijulikanalo
kama Misk ya Roho.

Katika maelezo yake, Sheikh Bizimana alidokeza kuwa Muislamu wa kweli ni yule anayemtanguliza Mwenyezi Mungu na Mtume wake [rehema za Allah na amani zimshukie] katika kila kitu, ndani ya maisha yake ya kila siku. Sheikh Bizimana alibainisha kuwa, utukufu wa Allah katika uumbaji hauwezi kufikiwa na kiumbe chochote.

Binadamu hawana nguvu wala uwezo wa kuumba chochote, wanaishia kutengeneza maroboti ambayo hata hivyo hayawezi kufanya lolote,” aliongeza kusema Sheikh Bizimana na kuwataka waislamu kushikamana na mambo yenye kujenga na kuhuisha Imani.

Imani ya mja imejengwa katika mambo mawili, nayo ni kauli/maneno na matendo na kwa ajili hiyo waislamu wanatakiwa waisome dini yao ili waweze kutekeleza ibada kwa usahihi zaidi,” alifahamisha Sheikh Bizimana.

 

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close