Matukio

Kumbukizi ya Misk ya Roho ya 2017

Mnamo Novemba 26, 2017, historia iliandikwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee kwa kufanyika kwa kongamano kubwa la kwanza lililojumuisha masheikh mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki. Masheikh hao walikutanishwa katika jukwaa moja na kukonga nyoyo za Waislamu sio tu wa Afrika ya Mashariki bali duniani kote kwa ujumla ambao walifuatilia tukio hilo kupitia vyombo vya habari.

Misk ya Roho ni nini?
Misk ya Roho ni Kongamano la Kidaawah la Afrika Mashariki ambapo taasisi yetu pendwa ya
The Islamic Foundation (TIF) huwaalika masheikh na walinganiaji mbalimbali kutoka nchi za Afrika
Mashariki yaani Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa jamii.

Mada za kongamano
Mada kuu tatu zilizosheheni katika kongamano hilo ni Jinsi ya kuwa na Ikhlaas, umuhimu wa elimu, na thamani ya amani.

Masheikh waalikwa
Masheikh walioalikwa ni Sheikh Nurdin Kishk na Sheikh Salim Barahiyan kutoka Tanzania, Sheikh Yusuf Abdi na Sheikh Juma Amir kutoka Kenya, Sheikh Ibrahim Kyebanja kutoka Uganda, Sheikh Maboyi Jamali kutoka Rwanda na Sheikh Zuberi Bizimana
wa Burundi.

Wageni Mashuhuri
Sambamba na masheikh waalikwa, wageni mashuhuri waliopata wasaa wa kuhudhuria ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir; Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Al-Kaabi; Rais wa taasisi ya Al-Hikmah, Sheikh AbdulQadir Al-Ahdal na kijana machachari aliyemlingania Rais wa Kenya Uhuru Kenyata awe Muislamu, Omar Muhammad.

Mafanikio
Hakuna kitu kizuri kama watu wakikusanyika kusikiliza neno la Mungu, kupewa daawah na kusikiliza mawaidha kutoka masheikh wao. Waislamu na wasio Waislamu walikusanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee tangu alfajiri, kuja kushuhudia kongamano hilo na kufukizwa Misk ya Roho zao. Kongamano hilo lili chukua siku nzima mpaka saa 12 jioni, lakini Waumini walibaki ukumbini kumsikiliza mpaka sheikh wa mwisho. Kongamano la Misk ya Roho ni moja ya njia za kujenga umoja, upendo na amani miongoni mwetu, na pia ni jukwaa (platform) la kukuza vipaji kwa vijana wa Kiislamu wanaoshiriki kwa namna mbalimbali. Lakini pia ni sehemu inayowakutanisha watu mbalimbali wa kada tofauti ambao wanapata kujuana kwa kukaa pamoja siku nzima. Kongamano hili ilikuwa ni fursa kwa Waislamu ya sio tu kusikiliza mawaidha na nasheed, lakini pia kukaa pamoja siku nzima, kula chakula, kuswali, kujuana na kufurahi kwa pamoja, na hivyo kujenga urafiki.

Kwanini uhudhurie Kongamano la pili la Afrika Mashariki?
Kama tulivyoona, faida walizopata waliohudhuria Kongamano la Kwanza la Afrika Mashariki ni kielelezo tosha kuwatija inayopatikana kwa kuhudhuria makongamano haya ni kubwa sana na ni vizuri kuhudhuria mwaka huu ili tuendelee kunufaika na elimu zinazopatikana. Kama haukupata fursa ya kuhudhuria Misk ya Roho ya mwaka jana, mwaka huu usikubali kukosa. Ukisikia tiketi zinatangazwa, wahi ujipatie yako mapema, usisubiri mpaka mwisho kwani tiketi huisha kwa haraka sana.Njoo ujumuike na maelfu ya Waislamu wakisikiliza meneno ya kuwafusha Misk ya Roho zao. Kwa maelezo zaidi kuhusu Kongamanano la 2 la Afrika Mashariki wasiliana nasi kwa barua pepe: event@islamicftz.org

Tags
Show More

Sabrina Bayseir

The Islamic Foundation Volunteer

Related Articles

Back to top button
Close
Close