FeaturedProjects Department
Trending

Mwaka mwingine wa mafanikio TIF

Story Highlights
  • Knowledge is power
  • The Future Of Possible
  • Hibs and Ross County fans on final
  • Tip of the day: That man again
  • Hibs and Ross County fans on final
  • Spieth in danger of missing cut

Mafanikio makubwa yametajwa kupa tikana ndani ya amwaka mmoja uliopita katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya taasisi ya The Islamic Foundation (TIF). Hayo yameelezwa na waku rugenzi wa idara mbalimbali za taasisi hiyo na pamoja na wale wa mikoa katika mku tano mkuu wa taasisi hiyo uliofanyika Februari 11 mjini Morogoro katika ukumbi wa mkutano wa shule ya Forest Hill.

Viongozi waliwasilisha taarifa hizo mbele ya Mwe nyekiti wa taasisi, Aref Nahdi na wageni waalikwa waki wemo Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Sunna Tanza nia (BASUTA), Sheikh Ally Zuberi na Mudir wa taasisi ya Ansaar Muslim Youth Center ya jijini Tanga, Sheikh Salim Barahiyan.

Miongoni mwa mafanikio makubwa yaliyopatikana ni katika Idara ya Elimu kupitia shule za taasisi hiyo, For est Hill, Shule ya Msingi na Awali ya Morogoro, Shule ya Msingi na Awali ya Dodoma na ile ya Nusra iliyopo Mafia. Shule zote hizo, kwa mujibu wa ripoti, zimefanya vizuri sio tu kitaaluma lakini pia kimapato. Kwa sababu ya muelekeo mzuri wa shule hizo, taasisi hiyo imeendelea kuweke za zaidi katika shule hizo ili kuboresha mazingira ya kusomeshea na kujifunzia, huku pia msisitizo ukiwekwa katika malezi ya kiroho. Kwa mfano, katika shule ya Forest Hill, maboresho mbal imbali tayari yamefanyika na sasa ni zamu ya ujenzi wa msikiti, ambao uwepo wake utachochea na kuwepesisha malezi ya kidini kwa wana funzi hao. Kadhalika, shule ya Nusra ilisaidiwa kupata madawati 150 kwa ajili ya wanafunzi, ambapo katika mkutano huo mwalimu wake mkuu aliwasilisha salamu za shukrani kwa Mwenyeki ti Nahdi Katika nasaha za Mwenyekiti Nahdi kwa idara hiyo ya elimu, aliwataka wakuu wa shule za taasisi hiyo kujiepusha na ushawishi wowote wa kufanya udanganyifu.

“Pongezi walimu kwa kazi nzuri ya kufaulisha lakini msitutayarishie vihiyo,” ali sisitiza Nahdi.

TIF pia imepata mafanikio makubwa kwa upande wa programu ya da’awah kwa wasio Waislamu, inay otekelezwa kwa ushirikiano na taasisi ya iERA ambapo ndani mwaka mmoja zaidi ya watu elfu kumi walitoa Shahada ya kuukubali Uis lamu, na zaidi ya nusu ya hao ni Waislamu hai baa da ya kupata mafunzo na wamewekwa katika kanzu data wakifuatiliwa maende leo yao na kupewa usaidizi. Kadhalika, kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa iERA, Taj Mohammed Abbas, chini ya mradi huo ushirikiano wa taasisi hizo pia umewezesh wa kupatiwa mafunzo walin ganiaji na maimamu kupitia programu mbalimbali. Idara nyingine zilizowasil isha taarifa ni pamoja na Da’awah, Vyombo vya Habari, Miradi, Rasilima li Watu na Idara ya Fedha ambapo mafanikio mbalim bali yalitajwa ikiwemo ujenzi wa misikiti 14 iliyokamika na mingine zaidi 80 iliyo katika hatua mbalimbali za ujenzi, ugawaji vitabu vya tafsiri za Qur’an, utunzi wa mtaala wa kidini kwa ajili ya Mahad za taasisi hiyo na shule, maboresho ya usikivu wa radio na kadhalika.

Kwa upande wao, wakurugenzi mbalimbali wa mikoa waliopata fursa ya kuwas ilisha taarifa zao walizung umzia mahitaji makubwa ya misikiti katika maeneo yao. Baadhi ya mikoa ambayo uhitaji wa misikiti unatajwa kuwa mkubwa ni pamoja Kagera, Mara, Morogoro hususan katika wilaya za Mahenge, Kilombero na Mal inyi. Baaadhi ya wakurugenzi pia walishauri kununuliwe mitambo ya uchimbaji visi ma ya taasisi ili kurahisisha shughuli hiyo na kupunguza matumizi.

Akijibu, baadhi ya masuala katika ripoti za wakurugenzi wa mikoa, Mwenyekiti Aref Nahdi alisema mahitaji ya rasilimali ni mengi hivyo uon gozi unalazimika kutekeleza kwa mujibu wa vipaumbele na umuhimu wa miradi. Hata hivyo, aliahidi kutatua changamoto zote kama zilivyowasilishwa, kadri uwezo utakavyoruhusu.

Kutoka miongoni mwa waalikwa, alikuwepo pia miongoni mwakilishi wa Kituo cha. Masuala ya Huduma za Kifedha za Kiislamu na Ushauri Tanzania (CIFCA), Omary Sharifu, ambaye aliibua masuala kadhaa muhimu ya kuzingatiwa na TIF.Katika nasaha zake, alishauri, ni matumizi ya Sukuk kwa ajili ya kutafuta mtaji wa kuendeleza miradi ya taasisi hiyo, ikiwemo ile ya ujenzi wa hospitali za Kiis lamu. Pia, alishauri baadhi ya miradi ipelekwe maeneo yenye uhitaji zaidi, akimaan isha miji mikubwa, kama Dar es Salaam.Pia, mwakilishi huyo wa Cifca alishauri jitihada zaidi zifanyike kuwaendeleza wal imu wapya wa dini baada ya kupata mafunzo ili waju likane wapo wapi na wana tumika vipi. Pia, alisisitiza umuhimu wa kuweka nguvu zaidi katika kuwaendeleza Waislamu wapya baada ya kusilimu. Mara baada ya mkutano huo kwisha, wajumbe wali pata fursa ya kutembezwa katika miradi mbalimbali ya The Islamic Foundation katika mji wa Morogoro, ukiwemo mradi wa ujenzi wa msikiti wa kisasa utakaoingiza zaidi ya watu 3500. Michoro ya msikiti huo, teknolojia itakay otumika itaufanya msikiti huo kuwa wa kipekee Tanzania.

Related Articles

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also
Close
Back to top button