4. Jamii

Utukufu Wa Ustaarabu Wa Kiislamu Kimaadili

Na Sheikh Muhammad Amir Othman

Ustaarabu wa Uislamu ume fanya makubwa mengi kwenye karne zilizopita, hasa katika upande wa maadili, Nikuombe uambatane nami ili tubaini maana ya ustaarabu. Neno ustaarabu kilugha linamaanisha kuanzisha kikundi cha watu katika maeneo ya mijini, yaani kwenye maeneo ya miji, sawa ikiwa mijini au vijijini. Lakini kwa wanahistoria, watafiti na wataalamu wa mambo ya kijamii, maana ya ustaarabu ni pana. Ustaarabu umekuwa ni msamiati unaojumuisha maendeleo ya binadamu kwenye nyanja zote. Ustarabu na maendeleo huwa hayashamiri isipokuwa kwa watu waliotulizana na kuwa na utulivu mijini. Na ili kufikia maendeleo na ustawi kuna njia kadhaa:- Ni kurejea kwenye ufunuo. Yaliyofikiwa na akili na tafiti za kielimu Yanayovunwa na binadamu kwa njia ya tafiti, uzoefu na majaribio, pamoja na uchunguzi wa kina ikijumuisha hitilafu na kasoro: Ama mfumo wa ‘kimaadili’ umebainishwa na mwanazuoni bingwa Abu Hamid Al-Ghazaliy aliposema: “Maadili ni umbo lililojikita kwenye nafsi. Maadili hutoka kwenye nafsi kwa urahisi na bila ya kufikiri, na ikiwa umbo litatoa tabia nzuri na zinazokubalika kiakili na kisharia, huitwa tabia njema, na ikiwa vinayotoka ni vitendo vibaya, hapo umbo huitwa tabia mbaya”. Ama kuhusu suala la ‘elimu ya maadili’ kwa maana yake pana, wasomi wa kisasa wameeleza: “Ni mkusanyiko wa kanuni unaoziongoza tabia za mwanadamu na kuratibiwa na wahyi katika kupanga maisha ya mwanadamu na kuratibu mahusiano ya mwanadamu na wengine katika kufikia lengo la kuwepo kwake hapa duniani kwa namna njema”. Na kuna wataalamu wametoa ufafanuzi wa aina tano nazo ni: Maadili ya mtu binafsi, kama vile: uadilifu, usafi wa moyo, ukweli nk. Maadili ya kifamilia, kama vile kuwatendea wema wazazi na wanandoa kuishi vema, kuunga udugu nk. Maadili ya kijamii, kama vile: kutimiza amana, kutekeleza ahadi, kupatanisha, kuwatendea wema mafakiri nk. Maadili ya kitaifa, kama vile kushauriana, haki, kutimiza ahadi nk. Maadili ya kidini, kama vile k u m t i i n a k u m s h u k u r u Mwenyezi Mungu, kuridhika na qadar na maamuzi yake, k u m p e n d a , k u m u o g o p a , kumtegemea nk. Mfumo wa kimaadili katika Uislamu una kanuni zinazoikinaisha akili, kuuridhisha mwili na moyo, na hakuna katazo lolote la kisheria isipokuwa lina sababu ya kukatazwa. Mwenyezi Mungu anasema: “Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya,” (Qur’an, 17: 32) Na anasema: “Enyi mlioamini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa. Hakika Shetani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mung u n a k u s w a l i . B a s i j e , mmeacha?” (Qur’an, 5:91). Na hivi ndivyo maadili ya Kiislamu yanavyokubaliana na akili na maadili salama. Na maadili katika Uislamu hayana muda na hayatokani na maslahi binafsi, na kwa kuwa maadili hutegemea hisia za kimaumbile za mtu, na hufasiriwa na mfumo wa vitendo, hisia na kauli. Uislamu ukamfanya mwanadamu kuwa ndiyo asili ya maadili. Na maadili hulenga kufanikisha hadhi ya mwanadamu kwa kuzingatia mazingira na uwezo wake, na vyote alivyowepesishiwa kutoka mbinguni, ardhini, na kwenye vitabu alivyoteremshiwa na kupitia kwa Mitume aliyotumiwa na ambayo huthibitisha utu wa mwanadamu, na humuandaa na amali njema ambazo huhukumiwa na itikadi sahihi. Na hivi ndivyo ustaarabu wa Kiislamu ulivyodumu kuwa mfano wa kuigwa na mwanadamu.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close