2. Afya4. Jamii

Undani wa vichocheo vya mwili na sababu za kukosa uwiano

Vichocheo vya mwili au ‘hormones’ ni aina za kemikali zinazotengenezwa na tezi tofauti katika mfumo wa vichocheo vya mwili.

Kemikali hizi hubeba ujumbe mbalimbali ambao huviamuru viungo vyote vya mwili kufanya kazi tofauti katika nyakati tofauti. Kemikali hizi pia hubeba ujumbe mwingi wa kuviamuru na kudhibiti matendo yote yanayotokea katika viungo vyote vya mwili kama vile kuongeza au kupunguza mapigo ya moyo.

leo tutaelezea kiundani vichocheo vya mwili ikiwa pamoja na kuona dalili na magonjwa mbalimbali yanayohusiana na kukosa uwiano wa vichocheo vinavyoathiri shughuli mbalimbali za miili yetu.

Tezi zinazotengeneza vichocheo

Tezi za mwili au ‘endocrine glands’ ni viungo vinavyopatikana katika sehemu tofauti za mwili na kazi zake kuu ni kutengeneza, kuhifadhi na kutawanya vichocheo katika mishipa ya damu.

Katika miili yetu kuna aina kuu saba za matezi ambayo hutengeneza vichocheo vyote katika mwili. Tezi hizi ni pamoja na tezi ya adrenali, tezi za uzazi (ovari na korodani), tezi ya pituitary, tezi za thairoidi na parathairoidi, tezi ya haipothalamasi, tezi ya pineali pamoja na tezi za kongosho.

Ndugu msomaji, tezi zote hizi hutengeneza vichocheo mbalimbali ambavyo vinaathiri katika viungo tofauti vya mwili.

Sayansi ya vichocheo kwa ufupi

Ingawa kuna aina saba tu za tezi, aina nyingi sana za vichocheo zinatengenezwa na tezi hizi. Kama tulivyojionea katika utangulizi, vichocheo ni kemikali maalumu ambazo hubeba ujumbe maalum kwenda sehemu maalum. Kwa lugha rahisi tunaweza kusema vichocheo ni kama funguo ambazo hufanya kazi katika kufuli maalumu.

Kuharibika kwa uwiano wa vichocheo

Kwa kawaida tezi za mwili huruhusu kiwango maalum cha vichochezi kulingana na mahitaji ya mwili. Kukosekana kwa uwiano wa viwango vya vichocheo katika muda muafaka huweza kutokana na kuwepo kwa matatizo katika tezi husika na kupelekea tezi hizi kutengeneza kiwango kikubwa sana au kidogo sana cha vichocheo. Mara nyingi viwango hivi ambavyo havikutolewa katika uwiano sahihi huleta athari za moja kwa moja katika mwili.

Mbali na kuwa matatizo ya tezi huharibu uwiano wa vichocheo; pia yapo matatizo mengine yanayoweza pia kupangua uwiano wa vichocheo. Matatizo haya ni pamoja na msongo wa mawazo (hasa wa muda mrefu), ugonjwa wa kisukari na utapiamlo, uzito mkubwa wa mwili, baadhi ya madawa (hasa dawa za kupanga uzazi), baadhi ya sumu, kemikali na mionzi, baadhi ya saratani na pia matatizo katika vinasaba. Hivi vyote vinaweza kusababisha kupanguka kwa uwiano wa vichocheo.

Baada ya uwiano wa vichocheo kupanguka kwa sababu mbalimbali, mwili huanza kutengeneza dalili tofauti kulingana na aina husika ya kichocheo.

Dalili za kuharibika kwa uwiano wa vichocheo

Kama tulivyodokeza awali, dalili za kupanguka kwa vichocheo hutegemea na aina ya tezi na vichocheo husika. Kwa ujumla, dalili za kukosekana kwa uwiano wa vichocheo ni pamoja na kuongezeka au kupungua uzito bila sababu, kutoka jasho jingi bila sababu, kukosa usingizi, ngozi kuwa kavu, mabadiliko ya shinikizo la damu, hasira zisizo na sababu, uchovu, kukosa hamu ya kula, kuvimba shingo, kunyonyoka nywele, kukosa hamu ya tendo la ndoa, kupata msongo wa mawazo na wasiwasi wa mara kwa mara.

Hata hivyo, dalili hizi zinaweza kutofautiana baina ya mtu na mtu, kutegemeana na jinsia ya mgonjwa.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close