2. Ncha ya Kalamu

Nani Aliyeuza Ardhi Ya Wapalestina?

SEHEMU YA 23,Utangulizi: Toleo lililopita tuliona yaliyojiri Mashariki ya Kati baada ya mwaka 1945. Tulisimama kwa kuuliza swali, je Saudi Arabia iliingia vitani kuilinda Palestina kama ilivyoahidi? Nini kilitokea baada ya sarakasi zote hizi kuhusu hatima ya Palestina?. Sasa endelea…

Kitisho cha Saudi Arabia kwamba ikibidi itaingia vitani kuipigania ardhi ya Palestina kilipata mtihani wake wa kwanza kwa kuundwa Kamati ya Pamoja ya Uingereza na Marekani kuhusu Palestina. Miezi miwili baada ya Rais Harry Trumann wa Marekani kutangaza Marekani itawapa hati za kusafiria wahamiaji laki moja wa Kiyahudi walionusurika katika makucha ya Hitler waingie Palestina, tangazo hilo lilipingwa na nchi za Kiarabu ikiwepo Saudi Arabia. Hali hii ilimpelekea Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Ernest Bevin kuchukua hatua. Novemba 13 mwaka 1945, Bevin alipendekeza kuundwa kwa Kamati ya Pamoja Kati ya Uingereza na Marekani kushughulikia hatima ya ardhi ya Palestina. Wakala wa Kiyahudi (Jewish Lobby) na mataifa ya Kiarabu kupitia Arab League wakajiandaa kutoa maoni yao. Wapalestina wenyewe pia walipewa nafasi ya kutoa maoni yao mbele ya kamati hiyo. Mataifa ya Kiarabu yalikuwa na wasi wasi kwamba uwepo wa Marekani kushughulikia kadhia ya Palestina ni tishio kwa maslahi yao. Kamati hiyo ilitembelea miji mikuu ya nchi za Kiarabu na hata ardhi ya Palestina. Kama tulivyoona kwamba mataifa ya Kiarabu yalikuwa yanatofautiana kimtazamo kuhusu kadhia ya Palestina, hivyo basi kamati hiyo ilipotembelea nchi mbalimbali za Kiarabu ilipata maoni tofauti. Kwa mfano, ikiwa nchini Iraq, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nje ya nchi hiyo wa wakati huo, Dkt. Muhammad Jamali, aliieleza kamati hiyo ukaribu wa nchi yake na Palestina na kwamba Palestina iwe sehemu ya Iraq. Nchini Saudi Arabia nako, serikali ya nchi hiyo ilisema Mayahudi ni maadui zetu wakubwa mahali popote pale na kwamba ugomvi kati ya Waislamu na Wayahudi ni wa miaka zaidi ya elfu moja nyuma. Mfalme Ibn Saud alimalizia kwa kusema ingawa Waarabu hawana ugomvi na nchi za Magharibi, lakini kama Wayahudi watatawala Palestina, Waarabu wako tayari kuingia vitani. Ripoti ya kamati ya pamoja ya Uingereza na Marekani kuhusu kadhia ya Palestina ilitolewa Mei Mosi, siku yenye mafungamano na ibada za Kimasonia, na ilileta mlipuko katika nchi za Kiarabu kama ilivyokuwa kwa ile ripoti ya Tume ya Peel (Peel Commission Report) miaka tisa kabla. Sehemu ya ripoti hiyo ilisema: “Kwa kuwa Wayahudi 100,000 kutoka nchi za Ulaya wako tayari kuhamia Palestina, katazo la kuzuia Wayahudi kuhamia Palestina lililotolewa mwaka 1939 kupitia White Paper, liondolewe na waruhusiwe mara moja.” Wakati huo huo, Palestina isiwe ya Wayahudi wala Wapalestina (Warabu)!!! Taifa moja la Wayahudi na Wapalestina liundwe na kwamba mpaka hayo yatakapotimia na Palestina kupewa uhuru wake, ardhi ya Palestina iendelee kuwa mikononi mwa Uingereza kwa udhamini wa Umoja wa Mataifa (UNO). Ripoti hii haikumfurahisha mtu yeyote zaidi ya Wayahudi na Wazayuni waliokuwa nyuma ya mpango mzima wa kuikalia ardhi ya Palestina. Katika kujibaragua, Rais Trumann wa Marekani hakuonesha kama atasaidia kugharimia wahamiaji hao wa Kiyahudi. Uingereza nayo katika hadaa yake, ikatoa kauli kali kupinga ripoti hiyo huku nyuma ya pazia ikichekelea matokeo ya kamati hiyo. Kwa upande wa mataifa ya Kiarabu kupitia Arab League wakiongozwa na Katibu Mkuu, Abdul Rahman Hassan Azzam, Iraq, Misri, Saudi Arabia na mataifa mengine ya Kiarabu yalipinga ripoti hiyo. Kauli kali kali na hata maandamano katika baadhi ya nchi za Kiarabu zilitolewa hususan kuhusu vipengele vitatu vya ripoti hiyo; kuruhusiwa wahamiaji wapya, ardhi ya Palestina kuendelea kukaliwa, na Palestina kuwa nchi ya mataifa mawili – Waarabu na Wayahudi. Pamoja na ripoti hiyo kupingwa na Waarabu, kitu cha ajabu ni kwamba Wayahudi ndani ya Palestina walianza kuasi dhidi ya utawala wa Uingereza. Makundi mawili ya kigaidi ya Kiyahudi – Irgun na Stern, yalianza kushambulia vituo vya ulinzi vya Waingereza. Makundi mengine ya wanamgambo wa Kiyahudi – Haganah na Jewish Agency – yalipinga hatua hiyo ya Irgun na Stern lakini huku yenyewe yakijizatiti vilivyo kwa vita ambavyo Wazayuni walijua haviko mbali kutokana na kauli za viongozi wa nchi za Kiarabu na pia kwa kujua kuwa Wazayuni watapewa Palestina kupitia Umoja wa Mataifa (UNO). W a z a y u n i w a l i k u w a wameamini Marekani ndiyo itakayowasaidia kuikalia ardhi ya Palestina na waliwatuhumu Waingereza kwa kuwapendezesha Warabu na kuwasaliti Wayahudi. Wayahudi walifanya hivyo pamoja na kwamba ni Uingereza ndiyo iliyoasisi suala la Wayahudi kupewa ardhi ya Palestina kupitia tamko la Balfour (Balfour Declaration) la mwaka 1917. Kuanza kuuawa kwa wanajeshi na polisi wa Uingereza na makundi ya kigaidi ya Wazayuni ya Irgun, Haganah, Stern na Jewish Agency kuliwalazimu Waingereza kuchukua hatua kurejesha amani na utulivu. Shambulio la Kwanza la Wazayuni Serikali ya Uingereza iliamua kuwakamata viongozi wengi wa Jewish Agency na wale wa Irgun, Haganah na Stern. Mwezi mmoja baadaye, Wazayuni wakafanya shambulio kubwa la bomu katika Hoteli ya King David mjini Jerusalem ambayo ilikuwa kama makao makuu ya utawala wa Waingereza Palestina. Shambulio hilo la Wazayuni dhidi ya Waingereza ambao waliwafadhili na kuwasaidia kuingia Palestina lililotokea Julai 22 mwaka 1946 liliustaajabisha ulimwengu. Shambulio hilo lililotekelezwa na kundi la kigaidi la Irgun Zva’I Leumi liliharibu kabisa jengo la hoteli hiyo na kuua watu 91, Waingereza 28, Waarabu 41, Wayahudi 17 na watu wengine watano. Hilo ndiyo shambulio lililotoa mwelekeo wa Wazayuni kwamba wasingekuwa tayari kuondoka Palestina hata kama ni kwa kupigana na mikono iliyowafadhili ya Waingereza na hata Wamarekani (kama ilivyotokea kwa shambulio la ndege za kivita za Israeli kwa meli ya kivita ya Marekani SS Liberty Juni 8, mwaka 1967). Shambulio hilo lililopangwa na Menachim Begin na David Ben Gurion, Wazayuni wawili waliokuja kuwa Mawaziri Wakuu wa Israeli, liliweka msingi wa taifa la Israeli kuwa ni taifa la kigaidi. Waarabu na kitisho cha Maisha ya Hind bint Utba mke wa Abuu Sufian Wazayuni Wakati haya yakitokea katika ardhi ya Palestina, mataifa ya Kiarabu chini ya Arab League yalikutana kujadili hatima ya Palestina. Waarabu walikubaliana kwa ujumla kwamba ushirikiano kati yao na UNO ndiyo njia muafaka. Viongozi wa Misri, Syria, Yemen na Saudi Arabia walitoa tamko la pamoja kutambua UNO kama msuluhisi wa mgogoro wa Palestina badala ya Uingereza. (Tazama Khallil: ‘The League of Arab States: A Study in Dynamics of Regional Organization’ Uk224-26). Masikini Waarabu hawakujua kwamba Umoja wa Mataifa (UNO) ni serikali ya kutawala dunia iliyoundwa na Wazayuni katika maandiko yao ya kale yaitwayo ‘The Protocol of The Learned Elders of Zionism’. Kwa hiyo kwa mataifa hayo ya Kiarabu kuwa na imani kwamba umoja huo ndiyo utakaotatua mgogoro wa Palestina dhidi ya Wazayuni ilikuwa ni sawa na kuota ndoto za mchana au ni sawa na kumuamini chui amtunze ndama. Mkutano mwingine wa mataifa ya Kiarabu ulifanyika mjini Bludan, Syria. Katika mkutano huo, kauli kalikali za kimapambano zilitolewa hususan na Syria na Iraq. Jamal wa Iraq alitoa maneno makali akisema “Muda wa maneno umekwisha na Marekani na Wayahudii hawaelewi isipokuwa kauli ya nguvu.” Nyuma ya pazia, serikali ya Iraq iliungana na Misri, Lebanon na Saudi Arabia ambazo zilikuwa na msimamo tofauti. Waziri wa Misri alisema “Ikiwa tutawaamrisha watu wetu wapigane, tutakuwa tunawaangamiza tu kwa sababu Wayahudi wanawazidi Wapalestina kijeshi.” Mjumbe wa Saudi Arabia, Yusuf Yasin alisisitiza umuhimu wa kutumia njia za kidplomasia kutatua mgogoro wa Palestina akidai kwamba ni muhimu kuangalia uhalisia wa nguvu za Waarabu na Wayahudi zikoje. Msimamo wa tatu ulikuwa kusubiri mpaka Waingereza watoke Palestina kisha kuanzisha mapambano ya silaha. Msimamo huu uliungwa mkono na Syria, Jordan na Wapalestina wenyewe. Katika hali hii, ilikuwa vigumu kwa Waarabu kukabiliana na Wa y a h u d i kwa sababu W a a r a b u w a l i k u w a wamega – wanyika na h aw a k u w a na msimamo mmoja. Itaendelea

Show More

Related Articles

Back to top button
Close