2. Ncha ya Kalamu

Nani Aliyeuza Ardhi Ya Wapalestina?

SEHEMU YA 20 Wiki iliyopita tulianza kuangalia kadhia ya Palestina baada ya Vita ya Pili ya Dunia na jinsi Mfalme Abdallah wa Jordan alivyokuwa akijaribu kuiweka Palestina chini ya Shirikisho la Jordan, Syria na Lebanon. Sasa endelea…

Waarabu na kadhia ya Palestina

Kama kulikuwa na matumaini waliyokuwa nayo Wapalestina kuhusu kupata haki yao ya kujiamulia mambo yao, basi yaliwekwa mikononi mwa nchi za Kiarabu. Mnyukano kati ya mataifa ya Kiarabu ulikuja kuwagharimu Wapalestina ardhi yao. Nchi hizo zilikuwa katika mivutano kati yao kupigania uongozi wa mataifa ya Kiarabu, nafasi ambayo ilikuwa ya heshima kubwa mbele ya medani za kimataifa. Nchi ya kwanza kuonesha dhamira ya kutaka kuwa kiongozi wa nchi za Kiarabu, na kwa maana hiyo nchi za Kiislamu , ni nchi ndogo ya kifalme ya Transjordan (Jordan) chini ya Mfalme Abdallah bin Sharifu Hussein bin Ali wa ukoo wa Banu Hashim. Abdallah alikuwa akidai hayo kutokana na kuiunga mkono Uingereza na washirika wake katika vita na kuwa kwake mrithi wa aliyekuwa kiongozi wa Waarabu – Sharifu Hussein bin Ali. Pia alidai kuwa aliahidiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza, Winston Churchil, kuwa angemfanya Abdallah kiongozi wa Syria. Abdallah hakuficha azma yake mbele ya viongozi wengine wa nchi za Kiarabu ya kutaka awe kiongozi wa Waarabu wote na apewe Palestina iwe chini ya milki yake itakayojumuisha Jordan, Syria na Lebanon. Aliiweka wazi azma hiyo katika mikutano rasmi ya wakuu wa nchi za Kiarabu jambo lililowatia wasi wasi watawala wenzake wa nchi za Kiarabu. Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Iraq, Nuri Pasha AlSaid, alikuwa na azma yake vile vile. Yeye alitaka kuundwa kwa alichokiita, ‘Greater Syria’ au Syria Kuu itakayojumuisha Palestina, Syria, Lebanon na Iraq huku akiwaahidi Wayahudi uhuru wa kujiamulia mambo yao ndani ya Palestina katika maeneo yenye Wayahudi wengi. Al-Said aliwaambia Wayahudi kwamba wangeweza kuwa na shule zao, hospitali zao, sera zao, serikali za mitaa na hata ulinzi wao lakini chini ya ‘Serikali ya Pembetatu yenye Rutuba’, jina la eneo alilotaka kulitawala Nuri Pasha Al-Said. Msimamo wa tatu ulioneshwa na Misri. Waziri Mkuu wa wakati huo, Mustafa Al-Nahhas Pasha, alichukua msimamo unaowapendeza Wayahudi. Al-Nahhas na chama chake cha Wafd hawakuwa na azma ya kuitawala ardhi ya Palestina na walipendekeza kwamba makubaliano yoyote yale ni lazima yawahusishe Wayahudi. Pasha alifikia hata kupendekeza kwamba Wayahudi waalikwe katika mikutano ya nchi za Kiarabu, na suala la Palestina lizungumzwe kati yao. Msimamo huu uliwapendeza sana Waingereza na Wamarekani na tangu hapo Misri ikawa kipenzi cha nchi za Magharibi. Kwa upande wake, Mfalme Farouk wa Misri, alipinga msimamo huo wa Waziri wake Mkuu ambaye alikuwa amewekwa madarakani na Waingereza.Mfalme Farouk aliiona hiyo kama fursa ya kumuondoa madarakani AlNahhas kwa tuhuma za kuwasaliti Waarabu. Kwa upande wake, Mfalme Abdulaziz bin Saud wa Saudi Arabia hakuwa na azma kama ile ya Mfalme Abdallah wa Jordan na Waziri Mkuu Nuri Al-Said wa Iraq. Mfalme Ibn Saud alionesha wazi kuwa hayuko tayari kukubali madai ya Wayahudi kupewa ardhi Palestina. Mapema mwaka 1943, Ibn Saud alionya kwamba nchi za Magharibi kuunga mkono madai ya Wazayuni kupewa ardhi Palestina kutaharibu uhusiano wa nchi hizo na nchi za Kiarabu. Aliweka wazi msimamo wake kwamba wahamaji Wayahudi wanapaswa kurudi Ulaya au waende Marekani. “Kwa vyovyote vile, Waarabu hawatowaruhusu Wayahudi kuwa na nchi Mashariki ya Kati kwa mujibu wa Qur’an” (Life Magazine, Desemba 30, 1943- mahojiano na Mwanamfalme Faisal bin Abdilaziz Al-Saud). Wamagharibi na msimamo wa Waarabu Maneno makali ya Ibn Saud hayakupita bila mazingatio kwa upande wa Marekani na Uingereza, vinara wawili wa siasa za Mashariki ya Kati. Serikali zote mbili ziliamua kupooza hali ya joto kwa kuahirisha hatma ya Palestina mpaka baada ya kumalizika Vita vya Pili vya Dunia. Marekani ilionesha kama vile imerudi nyuma kuhusu kadhia ya Palestina, lakini kiukweli ilikuwa ndiyo kwanza inajitosa katika kadhia ya Palestina kwa hatua ambayo iliipiku Uingereza kuhusu siasa za Mashariki ya Kati kuanza wakati huo hadi leo. Kwanza, Marekani ilikuwa ikipewa shinikizo kubwa na kongamano la Wazayuni nchini Marekani (American Jewish Lobby) ambalo ndilo linaloamua siasa za Marekani zama zote. Marekani ilichukua hatua ambazo ziliingiza katika kinyang’anyiro na Uingereza kuhusu eneo la Mashariki ya Kati. Kwanza, mwezi Januari mwaka 1944, Bunge la Wawakilishi (Congress) la Marekanii lilipitisha azimio linalounga mkono kuundwa kwa taifa la Wayahudi katika ardhi ya Palestina. Tamko hilo lilisomeka: “The United States would take appropriate measures to support free immigration of Jews so that they may ultimately reconstitute Palestine as a free and democratic Jewish Commonwealth”. Tafsiri: “Marekani itachukua hatua stahiki kuunga mkono na kusaidia uhamiaji huria wa Wayahudi (kwenda Palestina) ili hatimaye waweze kuifanya Palestina kama mali ya pamoja ya Wayahudi iliyo huru na ya kidemokrasia.” Msimamo huu ulitegemewa kuibua hisia kali miongoni mwa Waarabu hasa ukitilia maanani maneno ya Mfalme Abdulaziz wa Saudi Arabia mwaka mmoja nyuma kwamba Waarabu hawatoruhusu kuundwa kwa taifa la Wayahudi katika ardhi ya Palestina. Msimamo wa Waarabu dhidi ya Marekani Baada ya kulisoma azimio hilo la Bunge la Wawakilishi la Marekani katika gazeti la New York Times (linalomilikiwa na Wayahudi), Waarabu waliliona azimio hilo kama sera ya kuwaondoa Waarabu wote kutoka ardhi ya Palestina na kuijaza Wayahudi. Haraka haraka, Mfalme Abdulaziz bin Al-Saud akaanzisha kampeni ya wakuu wa nchi za Kiarabu kuandika barua kupinga msimamo huo wa Marekani. Kw a k u a n z i a n a y e y e mwenyewe, Ibn Saud aliwataka Maafisa wa Shirika la Uchimbaji Mafuta nchini Saudi Arabia (Amrico) kuhakikisha kwamba maslahi ya nchi za Kiarabu kuhusu ardhi ya Palestina yanalindwa. Aliwaambia maafisa hao mjini Jeddah nchini Saudi Arabia: “Kama Marekani na Uingereza hawataunga mkono msimamo wa nchi za Kiarabu kuhusu kadhia ya Palestina, watapoteza uhusiano wao na Saudi Arabia. Waarabu watapigana hadi mtu wa mwisho kuilinda Palestina,” (The Great Powers in the Middle East, 1941-1947). Kufuatia azimio la Bunge la Marekani, hata mawaziri wakuu wa nchi za Iraq, Misri na Lebanon walilipinga azimio hilo na wakaongeza kusema kwamba uhusiano kati ya Marekani na nchi hizo utakuwepo tu pale Marekani itakapojiweka mbali na Wazayuni. Mfalme Ibn Saud alipokutana na Rais Roosevelt wa Marekani mwezi Februari mwaka 1945, alijaribu kumweleza rais huyo wa Marekani aelewe unyeti wa kadhia ya Palestina. Roosevelt alizungumza mengi na Ibn Saudi lakini Ibn Saud hakunyenyekea mbele yake. Lilipokuja suala juu ya Palestina, Ibn Saud alikuja juu k i a s i k w a m b a mazun – gumzo kati y a k e n a Roosevelt hayakuendelea tena. ( J a m e s Byrnes, All in One Lifet i m e , u k .

Show More

Related Articles

Back to top button
Close