6. Malezi

Wanafunzi waaswa kutumia mitandao kwa mambo mema

Wanafunzi wa kidato cha sita wametakiwa kuitumia mitandao ya kijamii katika mambo mema na kuacha kufatilia mambo yaliyo nje ya maadili ya Kiislamu. Aidha, wanafunzi hao pia wametakiwa kujiepusha na migogoro isiyo ya lazima dhidi ya walimu wao.


mitandao ya kijamii ikitumiwa vema itawasaidia kujifunza masomo yao kiteknologia zaidi na hasa katika kipindi hiki ambapo nchi ikielekea kwenye uchumi wa viwanda


Sheikh Chega

Wito huo umetolewa na Sheikh Said Chega akimuwakilisha mgeni rasmi Sheikh wa Mkoa wa Pwani, Hamisi Mtupa katika mahafali ya wanafunzi ya kidato cha sita wa Kiislamu kutoka shule nne zilizopo katika eneo la Zogowale Kata ya Misugusugu, kijiji cha Zogowale katika halmashauri ya Kibaha mjini mkoani Pwani.

Sheikh Chega aliwaambia vijana hao kuwa mitandao ya kijamii ikitumiwa vema itawasaidia kujifunza masomo yao kiteknologia zaidi na hasa katika kipindi hiki ambapo nchi ikielekea kwenye uchumi wa viwanda. Kwa upande wake, mgeni mwalikwa Haji Mrisho, Mkurugenzi wa Pamoja Foundation aliwataka wanafunzi hao kujiepusha na migogoro isiyo ya lazima na walimu wao kwani watakapojiingiza kwenye migogoro watakosa ushirikiano wa kimasomo na walimu wao hali itakayowapelekea kufeli mitihani yao. Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Zogowale Tatu Mwambale amewapongeza viongozi wa Tamsya mkoani Pwani

Wanafunzi waaswa kutumia mitandao kwa mambo mema kwa kushirikiana na wanafunzi wa kidato cha sita katika kuandaa mahafali hayo kwa kuunganisha shule nne za sekondari zilizopo mkoani Pwani ikiwepo Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Zogowale, Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Kilangalanga, Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Kibaha na Shule ya Sekondari ya Lafsanjani Soga ya wasichana

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close