6. Malezi

Mifano 6 ya malezi mabaya

Ni uungwana wa kitaaluma kuanza kuandika makala kwa kuelezea maana ya dhana yako kuu unayoijadili. Katika makala haya, dhana yangu kuu ‘malezi mabaya. ’

Hapa, nikitaja malezi mabaya ninazungumzia mfululizo wa matendo mbalimbali ya mzazi ambayo huenda anayafanya kwa nia njema ya kumjenga mtoto katika tabia njema lakini kinyume na matarajio, matendo hayo ya mzazi, humharibu mtoto na kumfanya awe na tabia mbaya.

Mara nyingi mzazi hushindwa kung’amua athari hasi zinazojitokeza kwa mtoto zinazotokana na udhaifu wa malezi anayompa kwa sababu mzazi hufanya anayoyafanya kwa nia safi. Si hivyo tu, aghlabu, hata mzazi anapoona viashiria vya tabia mbaya kwa mwanae, atatafuta sababu nje ili tu kujifariji kuwa si yeye aliyesababisha.

Katika makala haya nitataja baadhi ya matendo wafanyayo wazazi ambayo ni mfano wa malezi mabaya na ambayo yanaweza kumharibu mtoto.

Kutompa moyo, kumkosoa

Mtoto amefanya jambo baya na kukiri makosa, lakini unamsema na kumsimanga nusu saa nzima. Unasahau kuwa alishaonesha ujasiri wa kukiri makosa na kuomba msamaha, jambo ambalo linapaswa kupongezwa. Mwisho, wake haoni tofauti ya kukiri kosa a kuomba radhi na kutokiri.

Kama hiyo haitoshi unamsema mtoto mbele za watu.  majirani, watoto wenzake na kadhalika jambo linalomuumiza hisia na kujihisi amekuwa kituko na kukosa thamani. Unafikia wakati unamchapa makofi.

Wazazi wa aina hii hawaishii hapo, mara nyingi hukosoa muda wote. Badala ya kumwambia mtoto.”Safi sana. Leo umeamka mapema sana mwenyewe bila kuamshwa,” mzazi anamwambia: “Leo Jua mvua itanyesha! Au unawawahi wavuta bangi wenzako huko?” Yaani muda wote ni sauti ni kukosoa tu.

Kutoonesha hisia, mapenzi

Wazazi wanatakiwa kuwaonesha watoto mapenzi na kuwajali. Umewahi kujiuliza kwa nini mwanao wakati fulani anafanya vituko mbele yako, hasa unapokuwa bize, hasa mbele za watu? Jibu ni rahisi. Mtoto anataka kukuvuta upate kumfuatia na kumjali. Wataalamu wanasema watoto wanafanya hivyo kwa sababu wanajihisi kukosa mapenzi, kujaliwa au jotojoto au wazazi.

Mzazi anatakiwa ajitahidi awe karibu na mtoto pale mwanae huyo anapomuhitaji. Wakati fulani mtoto anarudi nyumbani akiwa ameumizwa hisia, amekatishwa tamaa, amesimangwa na watu. Kinyume chake pia huweza kutokea. Yaani mtoto anaweza kurejea nyumbani akiwa na furaha kupitiliza. Katika hali zote mbili mtoto anamuhitaji mzazi aidha ili aliwazwe na kupewa moyo au ili apate mtu wa kushirikiana naye katika furaha yake hiyo.

Kuonesha mapenzi na kujali kunajumuisha pia kuongea na mtoto kuhusu mambo mbalimbali kwa hoja. Wapo wazazi ambao hukataa maombi ya mtoto na wakiulizwa kwa nini husema: “Kwa sababu nimeamua.”

Hili sijawabu jema. Muoneshe mtoto kwa nini huwezi kumpatia alichoomba.

Kumlinganisha

Katika mambo yanayoudhi na kukatisha tamaa kwa watoto ni kumlinganisha na mtoto mwingine kimasomo au katika mambo mengine. Wazazi wengine hujisahau hadi kufikia hatua ya kumsifu mtoto mwingine na kuonesha yu bora zaidi kuliko mwanae.

Ijulikane kuwa Mwenyezi Mungu amempa kila mtoto kipawa chake. Huyu anaweza zaidi hili, huyu anaweza jingine. Mpe moyo mwanao awe bora zaidi lakini kamwe usitamani awe kama mwingine.

Ni jambo zuri mtoto kuwa na mtu anayempenda na kumtamani, yaani kama kiigezo (role model)lakini kumlimgansisha mtoto na mwingine, hususan watoto wa rika lake, ikiwemo majirani, wanafunzi wenzake ni alama ya malezi mabaya.

Kuonesha mfano mbaya

Watoto hujifunza tabia, aidha mbaya au nzuri, kutoka kwa wazazi. Ukiona mwanao anafanya jambo baya, hebu tulia kidogo ujichunguze kwani anaweza kuwa amejifunza jambo hilo kutoka kwako.

Ukiona mtoto anakula amesimama au anatembea, labda huo ndiyo mwenendo wa wazazi. Watoto pia hudanganya kwa sababu wanasikia wazazi wakifanya hivyo. Mama anaweza kumwambia mtoto, akija fulani mwambie sipo. Baba ameenda kutembea na mwanae, kisha anamwambia mtoto, usimwambie mamako tulipitia mahali fulani. Mtoto huiga uongo huu na kuona ni jambo la kawaida.

Kumdekeza mno

Kuna wazazi wanadekeza mno watoto. Kila mtoto anacholilia, hupewa. Mzazi hawezi kabisa kusema hapana. Jambo hili lina madhara kwa sababu mtoto anaweza kujenga tabia ambayo mzazi hataweza kuidhibiti baadae, hiyo ni tabia ya kulazimisha apate kila atakacho.

Kosa jingine ni kumlinda mtoto kupita kiasi. Kumlinda mtoto kupita kiasi kunaweza kumfanya akose ujasiri wa kujaribu mambo, ikiwemo hata kushindwa kutengeneza marafiki wapya.

Kutozingatia dini

Kosa jingine la kimalezi ni kutozingatia dini. Hakuna kitu kikubwa katika malezi kama kuingiza katika moyo wa mtoto hofu ya Mwenyezi Mungu na kumfundisha maadili ya dini tukufu ya Kiislamu.

Ikumbukwe kuwa, kwa mujibu wa Uislamu, lengo kuu la kuumbwa kwetu ni kumuabudu Mwenyezi Mungu pekee; na ibada ya Mwenyezi Mungu inajumuisha kumtii yeye katika kila kipengele cha mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu kiuchumi, kijamii, kisiasa, kimahusiano na kadhalika.

Madhara ya malezi mabaya

Madhara ya malezi mabaya ni mengi. Mojawapo ni kumfanya mtoto akose huruma kwa watu wengine. Haya yanaweza kuwa matokeo ya moja kwa moja ya mtoto kukosa misingi mizuri ya dini. Jambo jingine linalochangia hali hiyo ni mtoto kukosa mapenzi ya wazazi na kuhisi hawamjali.

Madhara mengine ya malezi mabaya ni mtoto kukosa ujuzi wa kuingiliana na watu, hususan kujenga marafiki wapya. Hii zaidi hutokea kwa watoto ambao wamedekezwa sana na ambao wazazi wao

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close