6. Malezi

Malezi ya kifikra husaidia kupambana na tabia ya ukufurishaji

Malezi mazuri yana mchango mkubwa katika kupambana na fikra kali na potovu. Malezi pia yana mchango mkubwa katika kujenga familia, ambayo ni kiini na ustawi wa jamii nzima.

Ijulikane kuwa, jamii huundwa na familia kadhaa. Hivyo basi, familia zinapokuwa bora, na jamii huwa bora zaidi. Kinyume chake, familia zinapofisidika, jamii nayo huharibika. Uislamu umezingatia sana familia kwa sababu ndio jiwe la msingi la jamii.

Familia ndio sehemu ndogo zaidi ya mjumuiko unaounda jamii na taifa. Familia huanzishwa na mke na mume ambao baadae huwa baba na mama wakiletwa pamoja na kiunganishi kizito na kitakatifu kiitwacho ndoa. Kupitia ndoa, mume na mkewe wanaanza maisha yao pamoja, wanapata watoto na hivyo kukiandaa kizazi kipya kitakachobeba bendera ya umma wa kesho.

Kwa kweli, familia ina mchango mkubwa katika ujenzi wa jamii muda wowote na mahali popote. Familia huweka mikakati ya mustakbali na kumwelekeza kila mmoja wa wanachama wake kwenye wajibu wake na majukumu yake. Hivyo, familia ikitekeleza wajibu na majukumu yake, umma wote huwa na hali nzuri na kuepukana na fikra potovu za takfir, uadui, ufisadi, uharibifu huepukwa.

Qur’an Takatifu imesisitiza umuhimu wa familia na malezi mema na ikafanya sababu ya kujiokoa na madhara na maovu duniani na Akhera.

Mwenyezi Mungu anasema: “Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa.” [Qur’an, 66:6].

Aya hii inadhuhirisha kuwa Uislamu unahimiza kuwatunza watoto na kuwakuza katika malezi yanayoafikiana na mafundisho wa dini hiyo. Aya hii pia inawakumbusha wazazi majukumu yao, hasa kwa watoto wao.

Wazazi wanatakiwa kuwalea watoto wao kwa msingi wa Imani, kumuabudu Mwenyezi Mungu na kufuata itikadi iliyo sawa. Pia, watoto wafundishwe kuepukana na misimamo mikali na fikra potufu sambamba na kushikamana na mwenendo, maadili na tabia njema.

Malezi ni jukumu kubwa na muhimu. Shughuli ya malezi ni sawa na kuunda kizazi kizima kinachoweza kuboresha hali na kuleta maendeleo na mafanikio ama kusababisha uharibifu na ufisadi mkubwa. Malezi sharti yatokane na mafunzo ya dini, na wala yasiende kinyume na maamrisho ya dini.

Pia, kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu familia inatakiwa kuelewa na kutambua namna bora na inayofaa ya kulea watoto wake kati ya aina tatu za malezi tunazozifahamu. 

Mfumo wa kwanza wa malezi ni ule wa kuwatishia watoto, kuwahofisha na pengine hata kuwapiga. Athari ya mfumo huu ni kusababisha watoto kukosa imani na utulivu. Kinyume na fikra ya wazazi kuwa wanawasaidia watoto, ukweli ni kuwa wanafanya kosa kubwa la kutowasikiliza au kuwapa nafasi ya kuejieleza mbele yao. Malezi ya aina hii huzalisha watoto ambao ni watukutu na kuwa hatari kwa jamii nzima.

Mfumo wa pili wa malezi ni ule wa miamala laini ikiwemo kumpa mtoto kila analolitaka bila ya kujali linafaa au halifai. Mfumo huu huzalisha watoto wa mama na kuzalisha vijana wasioweza kutambua majukumu na wasiowajibika kwa wajibu yoyote kwani kazoea uzembe na kufanyiwa kila analolitaka bila ya kuweka juhudi zake hata kidogo.

Mfumo wa tatu ni ule wa malezi ya wastani ambao uko katikati, hauhofishi watoto wala kuwapa kila kitu bure.

Katika mfumo huu, familia inasifika kwa uwastani katika mambo yake yote. Familia inakuwa na mchango mikubwa katika jamii na umma wake. Hii ni familia inayozuia kuenea kwa fikra zisizo sawa na kupambana na misimamo mikali.

Kwa msingi huo, Uislamu unawajibika kutekeleza majukumu kwa mfumo wa wastani, bila upungufu wala ziada, hasa katika malezi ya watoto ambao ndio taifa la kesho na viongozi wa baadae

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close