6. Malezi

Maajabu ya watoto

Katika makala iliyopita, tuliona jinsi Mtume (rehema na amani ya Allah imshukie) Watoto ni viumbe wa kipekee. Hivi karibuni nilikuwa napitia tafiti mbalimbali kuhusiana na watoto, na nikagundua mambo kadhaa ambayo yatakushangaza kuhusu viumbe hawa wachanga ambao ndiyo kwanza wanaanza safari yao ya maisha. ya kisharia katika kugawa mali za Hunain. Katika makala hii tunaangazia zaidi maudhui hiyo.

Huwa na usingizi muda mwingi

Watoto hulala kwa masaa 5400, karibu takriban asilimia 70 ya muda wote, katika mwaka wao wa kwanza. Ukizingatia kuwa, mwaka una masaa 8760 muda huo wanaolala huonekana kuwa ni mwingi sana. Lakini kumbuka kuwa, watoto hulala kwa masaa machache mfululizo, yaani huamka amka kila badaa ya kipindi kifupi hususan katika miezi mitatu ya mwanzo.

Wanazaliwa waogeleaji

Inatajwa kuwa watoto, kiasili, wanazaliwa wapiga mbizi. Na ujuzi huu wa asili wa uogeleaji huja wenyewe wanapotumbukizwa ndani ya maji.

Kama walivyo samaki, watoto wanaweza kupumua na kumeza kwa wakati mmoja kwa miezi michache ya mwanzo. Wanajifunza ujuzi huu wakiwa tumboni na huupoteza ujuzi huo afikishapo miezi sita.

Watoto huzaliwa na mifupa 300

Watoto wanazaliwa na mifupa 300, ambayo ni asilimia karibu 94 au asilimia 50 zaidi ya ile ya watu wazima Watu wazima wana mifupa 206. Watu hujiuliza, mifupa mingine hupotelea wapi wanapokua wakubwa? Jibu ni kuwa, inaungana wakati wa ukuaji.

Watoto hawana mfupa mgumu wa goti

Watoto hawana mfupa mgumu wa goti. Ni katika kipindi cha ukuaji ndiyo kitu kilichopo badala ya mfupa huo hukomaa na kuwa mfupa. Inatajwa kuwa, watoto huzaliwa hivyo ili kurahisisha mchakato wa kutoka tumboni kwa mama wakati wa kuzaliwa.

Rangi ya kwanza kuitambua ni rangi nyekundu

Wataalamu wanasema, watoto huanza kutambua rangi wafikishapo miezi 18. Wafikishapo miaka miwili, watoto wanaweza kutambua walau rangi moja ua mbili, mara nyingi zile wazipendazo zaidi. Pia, kwa mujibu wa wataalamu rangi ya kwanza ambayo watoto aghlabu huitambua ni nyekundu, na rangi ya mwisho watoto kuitambua ni bluu na zambarau.

Watoto hukua haraka

Uzito wa watoto wanaozaliwa nao huongeza mara mbili wafikishapo miezi mitano tu baada ya kuzaliwa na hufikia mara tatu yake wafikishapo mwaka mmoja. Pia, huongezeka urefiu kwa sentimeta moja hadi moja na nusu kila mwezi. Kwa uumla watoto, hukua kwa haraka sana, katika mazingira ya kawaida ya ukuaji wao na kama hamna vikwazo.

Hawatoi machozi; hupoteza nywele walizozaliwa nazo

Kwa mujibu wa wataalamu, watoto hulia lakini hawawezi kuzalisha machozi halisi mpaka watakapofikisha wiki tatu. Vilevile, wafikishapo miezi minne, kama hawanyolewa wakiwa wadogo, hupoteza nywele zao walizozaliwa nazo. Nywele mpya huota badala yake.

Baadhi ya viungo vyao ni vikubwa

Kichwa cha mtoto mdogo aliyezaliwa kinafikia ukubwa wa robo ya mwili wake wakati kwa mtu mzima kichwa ni moja ya saba ya mwili wake. Macho yao pia ni asilimia 75 ya macho yao ya ukubwani.

Pia, kinyume na fikra za wengi, alama za kuzaliwa (birthmark) siyo ugonjwa na kiukweli asilimia 80 ya watoto huzaliwa na alama hizo zenye ukubwa, umbile na rangi tofauti. Baadhi ya alama za kuzaliwa hujitokeza siku kadhaa au wiki baada ya kuzaliwa, na baadhi hupotea ndani ya miaka kadhaa.

Wanasikia kama watu wazima

Watoto wadogo waliozaliwa punde wanasikia kama watu wazima. Watashtuka kwa kila sauti waisikiayo siyo kwa sababu sauti hiyo ni kubwa bali kwa sababu ni sauti mpya. Hata hivyo, mtoto pia huweza kutambua sauti ya mama yake, hata wakati wa kuzaliwa, jambo linaloshangaza sana. Watoto pia huhisi harufu ingawa uwezo wao wa kuona ni mdogo. Mara nyingi huona vitu vya ukaribu wa umbali wa hadi sentimita 20 hadi 30 tu.

Wanakojoa kila dakika 20

Mpaka kibofu chao cha mkojo kinapokomaa, watoto hukojoa kila baada ya dakika 20. Inakadiriwa kuwa mtoto ataangaliwa ipasavyo, atatumia zaidi ya nepi 3000 kwa mwaka wa kwanza. Kwa tabia yao hii na dharura nyingine, watoto huwanyima wazazi wao hadi siku 44 za usingizi katika mwaka wa kwanza pekee. Uzuri ni kwamba, wazazi hukesha kuwashughulikia watoto kwa mapenzi makubwa na ndiyo maana hawakereki wala kukasirika.

Mengine

Katika mengine ya ajabu kuhusu watoto, ni kwamba huzaliwa na hamu ya kutia kila kitu mdomoni, kwa mujibu wa utafiti uliofanyika Ufaransa. Vilevile, watoto hucheka hadi mara 300 kwa siku, wakati mtu mzima hucheka mara 60 tu, kwa wastani. Ajabu nyingine, watoto hujifunza lugha na lafudhi ya mama akiwa tumboni. Wanasayansi kutoka Chuo cha Wurzburg watoto hujifunza lugha ya mama katika miezi kitatu ya mwisho ya ujauzito.

Na mfanono wa lugha ya mama hujitokeza katika kilio chao baada ya kuzaliwa kiasi kwamba u n a w e z a kujua mtoto wa Kiswahili, Kisomali, Kizungu, Kiarabu kutokana na namna waliavyo na wanavyocheka!

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close