6. Malezi

Jamii yashauriwa kusaidia watu wenye mahitaji maalum

Jamii nchini imetakiwa kujenga utamaduni wa kusaidia wagonjwa na watu wenye mahitaji maalumu ili nao wajihisi ni sehemu muhimu ya jamii. Wito huo umetolewa hivi karibuni na Amir wa Umoja wa Wahadhiri wa Kiislamu hapa nchini, Sheikh Rajabu Salum katika kongamano la kida’awa lililofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Mabatiani uliopo manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam.

Sheikh Salum alisema kuwa jamii ya watanzania imekuwa haina utaratibu wa kuwatembelea na kuwasaidia wagonjwa na watu wenye mahitaji maalumu, hali ambayo inawafanya watu hao wajione kama waliotengwa na hivyo kukata tamaa ya maisha.

Sheikh Salum alisema: “Watu wenye mahitaji mbalimbali ni wengi; kuna watoto wa mitaani, yatima, wazee na wagonjwa ambao wapo hospitalini na majumbani. Sasa tujenge utamaduni wa kuwatembelea na kutoa chochote tulichojaliwa ili kuwasaidia.”

Pia Sheikh Salum aliongeza:
Wagonjwa wengi hukata tamaa ya maisha wakidhani kwamba maradhi yanayowasumbua hayawezi kutibika hivyo ni jukumu letu kuwatembelewa na kuwafariji ili waondokane na dhana hiyo.”

Aidha Sheikh Salum alizitolea wito taasisi na jumuiya mbalimbali kutumia sehemu ya faida katika shughuli zao ili kusaidia watu hao na kupata thawabu kwa Mwenyezi Mungu.

Akizungumzia umuhimu wa kuwatembelea wagonjwa na kuwajali yatima, Sheikh Rajabu alisema hizo ni katika ibada muhimu ambazo waislamu wamesisitizwa kuzipupia na ndio maana Mtume Muhammad (rehema na amani zimshukie) aliishi nyumbani kwake na yatima na wala hakuwatenga kwa kuwahifadhi kwenye nyumba maalum kama tufanya

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close