6. Malezi

Faida na Umuhimu wa Hijab kwa Mwanamke

Siku moja Nabii Musa (amani ya Allah imshukie) alikuwa akisafiri kuelekea Madyana. Alipofika huko alikuta kundi kubwa la wanaume wananywesha mifugo yao katika mto. Pembeni mwa mto huo kulikuwa na mabinti wawili ambao walizuiwa na kundi hilo la wanaume kunywesha mifugo yao. Nabii Musa akawauliza: “Mna nini? (Mbona hamteki maji ya kuwanywesha wanyama wenu)?” Wakasema: “Sisi hatunyweshi (wanyama wetu) mpaka wachungaji warudishe wanyama wao. Na baba yetu ni mzee sana.” Ndipo Nabii Musa akachukuwa wanyama wao na kwenda nao kisimani kuwanywesha. Baada ya kukamilisha zoezi hilo, Nabii Musa (amani ya Allah imshukie) alikaa kivulini akanyanyua mikono na kuomba: “Ewe Mola wangu! Hakika mimi ni mhitaji wa kheri yoyote utakayo niteremshia.” [Qur’an, 28:23–24]. Nabii Musa alitambua kuwa mabinti wale hawawezi kuchota maji kutokana na msongamano mkubwa wa watu katika eneo la kisima hivyo akachukuwa jukumu la kuwanywesha wanyama wao.

Mafundisho ya tukio

Katika tukio hili tumeshuhudia mabinti wawili wakichukuwa jukumu la kunyeshwa mifugo, kazi ambayo hapo awali ilikuwa ikifanywa na baba yao. Mabinti hao walikuwa wakijitenga na wanaume pindi wanapofika mtoni ili kulinda utu, hadhi na heshima yao lakini pia kuepuka kusongamana na kupigana vikumbo na wanaume.

Kwa kufanya hivyo walifunga mlango wa fitina za shetani na matamanio ya kuyaendea machafu ya zinaa. Na lau kama si Nabii Musa kuzungumza nao kwa heshima na adabu ili awasaidie basi wasingesema na yeyote.

Wanawake katika zama za Mtume Muhammad

Tunasoma katika historia (Tareikh) ya Uislamu kuwa wanawake katika zama za Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) walikuwa wakijitenga (hawachanganyiki) na wanaume, pia walikuwa wakivaa hijab kamili, yani nguo ndefu, nzito na zenye kuenea mwili mzima.

Vazi la hijab lina tija na maslahi makubwa kwa mwanamke mwenyewe na jamii nzima hasa ikizingatiwa kuwa mwanamke ni pambo ambalo wanaume hupenda kukaa nalo karibu.

Mabinti wawili tuliowataja katika tukio hili walimwambia Nabii Musa (amani imshukie) kuwa wanalazimika kwenda mtoni kunyeshwa mifugo kwa sababu baba yao ni mzee sana, lakini pia hawana ndugu wa kiume kama kaka, mjomba, baba mdogo, au baba mkubwa ambaye angefanya kazi hiyo.

Kutokana na changamoto hizo na nyingine ambazo hatukuzitaja mabinti hao walilazimika kwenda kuchunga mifugo ya baba yao ili isije kufa kwa njaa na kiu.

Haki za wanawake na vazi la hijabu

Hivi sasa kuna makundi mawili duniani yanayovutana katika kumtetea mwanamke. Kundi moja linataka mwanamke ajiheshimu kwa kufuata misingi ya sharia ya dini na jingine linataka kumkomboa mwanamke na kumfanya awe sawa na mwenye uhuru wa kufanya maamuzi yake mwenyewe hata kama yanapingana na sharia ya Mwenyezi Mungu.

Wasomi wa elimu za magharibi, wanafalsafa na watetezi wa haki za wanawake wamekuwa wakilinasibisha vazi la sitara la Hijab na kumnyima mwanamke haki na uhuru wa kuvaa.

Wakitumia ujinga wa wale wasioujua Uislamu, wanaharakati wa haki za wanawake wamekuwa wakidai kuwa hukumu zote za mavazi na stara ni za uzushi uliokuja baadae na si mambo yanayoamrishwa na Qur’an.

Baadhi ya Waislamu, kwa kuathiriwa na mawazo ya kimagharibi, nao wamekuwa wakifuata mkumbo huo na kujiingiza katika madai ya haki za wanawake kwa kuanika viwiliwili vyao, huku wakisahau kuwa kufanya hivyo ni kuhalifu hukumu za stara ya Kiislamu.

Jambo moja la kutia moyo ni kwamba, hivi sasa kuna idadi kubwa ya wanawake wa Kiislamu wanaojitambua na kujiheshimu wakiwemo mawaziri, walimu wa shule na wahadhiri wa vyuo vikuu wanaovaa vazi la stara la Hijab huku wakitoa mchango wao katika kulitumikia taifa.

Pamoja na mafaniko hayo, bado tuna jukumu la kulinda hadhi na heshima ya mwanamke na kupinga hila zote zinazolenga kumvua nguo.

Yanayopaswa kwa wanawake

Uislamu umejengwa katika msingi wa kulinda na kuhifadhi heshima ya mwanamke. Uislamu pia umeweka utaratibu wa kisharia wa kuyaendea mambo mbalimbali lengo likiwa ni kuilinda jamii kutokana na uharibifu unaoweza kufanyika katika hii dunia kupitia wanawake.

Mathalan, sharia ya Uislamu inawataka wanawake wa Kiislamu kusali nyumbani kwani kwa kufanya hivyo watalinda heshim a yao na kujiweka mbali na maasi . Mtume amesema:

“Msi- wazuie vijakazi wa Allah katika nyumba za Allah na sala wanazosali katika nyumba zao ndiyo bora zaidi.”

Mwenyezi Mungu ameamrisha wanawake wajisitiri kwa vazi la Hijab na amewakataza kuchanganyika na wanaume, kusafiri bila ya kuwa na maharimu na kulegeza sauti zao pindi wanapozungumza na wanaume. Mwanamke ameamrishwa kubakia nyumbani kwa ajili ya kuishughulikia familia yake (mume na watoto), na akilazimika kutoka basi atoke kwa dharura baada ya kupata idhini ya mumewe akiwa amejisitiri vizuri kwa Hijab ya kisharia.

Mtume amesema: “Hakika dunia ni tamu rangi ya kijani. Allah amewatawalisha dunia ili atazame matendo yenu. Kwa hiyo, iogopeni dunia na waogopeni wanawake, hakika fitina (mtihani) ya mwanzo kuwasibu wana wa Israil ilitokana na wanawake.” [Muslim].

Na katika hadith iliyosimuliwa na Abu Huraira (Allah amridhie) Mtume (rehema na amani ya Allah imshukie) amesema:

“Mwanadamu ameandikiwa fungu lake la uzinifu na hakuna yeyote awezaye kulikwepa hilo. Zinaa ya macho ni kutazama, masikio ni kusikiliza, ulimi ni kuongea, mkono ni kushika, mguu ni kupiga hatua (kuuendea uzinifu), moyo ni kupenda na kutamani; na katika yote hayo utupu ndiyo unaosadikisha jambo au kulikanusha.” [Bukhari na Muslim].

Pia Ibn Abbas (Allah amridhie) amehadithia kuwa alimsikia Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) akisema:

“Asikae faragha mwanamume na mwanamke isipokuwa awe na maharim wake, na wala asisafiri mwanamke isipokuwa awe na maharim wake.”

Mtu mmoja akauliza: “Ewe Mtume wa Allah! Mke wangu ametoka kwenda kuhiji nami nimejiandikis h a kwenda jihadi.” Mtume akamwambia: “ Toka uende kuhiji na mkeo . ” [Bukhari na Muslim].

Baadhi ya wanazuoni akiwamo Abu Hanifa, An– Nakha‘iy, Al –Hasan , Ath– Thawriy, Ahmad na Is–haq wamesema kuwa ni sharti mwanamke afuatane na maharim wake wakati wa safari. Kwa sababu hiyo, haifai na ni haramu kwa mwanamke wa Kiislamu kutoka nje ya nyumba yake isipokuwa kwa dharura ya kisharia.

Katika tukio hili tumeshuhudia mabinti wawili waliokwenda kuwanywesha wanyama wao mtoni wakijitenga na wanaume, jambo ambalo lilimfanya Nabii Musa (amani ya Allah imshukie) achukue wanyama wao na kwenda nao kisimani kuwanywesha.

Kitendo cha Nabii Musa cha kuwasaidia mabinti hao kilipelekea kupata hifadhi katika nyumba ya Nabii Shuaib (Baba mzazi wa mabinti hao) na hivyo kuondokewa na dhiki ya ukosefu wa sehemu ya kufikia baada ya kukimbia nchini Misri. Ikumbukwe kuwa Nabii Musa (amani ya Allah imshukie) alikimbia Misri baada ya kumuua mmoja wa watu wa kabila la Firauni

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close