3. Kitabu Nilichokisoma

Tabia za mfano za marafiki wa Allah: Kitabu kinachofunza tabia za Kiislamu

Tabia za Mfano za Marafiki wa Allah’ ni kitabu kilichoandikwa na Othman Nuri Topbash na kufasiriwa katika lugha ya Kiswahili na Ibrahimu Kabuga. Allah awalipe kwa juhudi walizozifanya. Kama inavyojulikana, Waumini wa dini ya Kiislamu tunamchukulia Mtume Muhammad (rehema na amani za Allah zimshukie) kuwa ni kiigizo chema. Vilevile, Waislamu wanajifunza kutoka kwa Masw a h a b a a m b a o n i warithi wa Mtume. Katika muktadha huu, kitabu kinaeleza k u w a m a r a f i k i w a Mwenyezi Mungu ni warithi wa Mitume, na w a o h u e n d e l e a kutekeleza kwa vitendo muongozo wa Mtume na maadili yake kamili kwa ajili ya wanadamu wote. K i t a b u k i n a z i d i kueleza kuwa marafiki wa Mwenyezi Mungu ni watu wanaoheshimika sana kwa wale amb a o h a w a k u w a o n a Maswahaba wa Mtume Muhammad (rehema n a a m a n i z a A l l a h zimshukie) kwa kujifunza kutokana na matendo yao ya mfano. Zaidi, kitabu hiki ‘Tabia za Mfano wa marafiki wa Allah’ kinaeleza kuwa marafiki wa Mwenyezi Mungu ni njia za baraka na rehema kwa majirani zao. Na wao, marafiki wa Allah, ni mikono ya huruma inayokumbatia makundi yote ya jamii. Tabia za marafiki wa Allah Katika namna ya mpangilio wake, kitabu kinazitaja tabia za marafiki wa Allah kwa sura (mada) kwa kutoa ushahidi wa aya za Qur’an, mafundisho ya Mtume na matendo ya Maswahaba. Zifuatazo ni chache miongoni mwa tabia nyingi zilizotajwa katika kitabu ‘Tabia za Mfano za Marafiki wa Allah’. Subira na uvumilivu Marafiki wa Allah huwa na Subira na uvumilivu mbele ya wajing a n a w e ny e t a b i a mbaya. Hakika wao, marafiki wa Allah, wan aw a k i l i s h a v i ge z o halisi na mifano hai kwa ajili yetu hivyo tunapaswa kuchukua mifano kutokana na tabia zao adhimu. Kitabu hiki kinaeleza subira na uvumilivu aliokuwa nao Mtume Muhamad (rehema na a m a n i z a A l l a h zimshukie) kutokana na mateso na ukatili aliopata katika kipindi cha uhai wake. Licha ya hali hizo, Mtume Muhamad (rehema na amani ya Allah zimshukie) alikuwa mvumilivu na hakuacha kutoa ujumbe wake kwa wanadamu. Mtume Muhammad (rehema na amani ya A l l a h z i m s h u k i e ) alikuwa akijua kuwa anazitafuta radhi za Mola wale. Kitabu kinanukuu aya ya Qu’ran iliyoshushwa kutokana na kadhia hii: “Wala usiwatii makafiri na wanafiki na usijali udhia wao nawe mtegemee Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa mtegem e w a ,” ( Q u r ’ a n , 33:48). Kitabu kinaeleza matendo ya tabia za marafiki wa Mwenyenzi Mungu ni kuwa madhubuti dhidi ya majanga, subira ya kuvunjiwa heshima na kusimama imara dhidi ya misukosuko yenye kushangaza. Kitabu kinasema mwanzo wa elimu ni uvumilivu na mwanzo wa hekima ni kuishi vizuri na watu. Kitabu kinaeleza tabia za marafiki wa Allah ni kuukabili ubaya kwa wema, Mengi yamezungumziwa katika nukta hii lakini tuangalie nukta isomekayo kusamehe katika wakati sahihi. K i t a b u k i n a f u n z a kwamba kusamehe kila aina ya makosa haipaswi kuchukuliwa kuwa ni jambo sahihi, bali msamaha unahusika tu pale ambapo kosa linalokuwa limetendwa ni katika mambo binafsi. Mathalani kitabu kinaeleza kuna makosa ya uhalifu unaotendwa dhidi ya jamii, dini na mambo matukufu ambao hauwezi kuvumiliwa. Katika hali kama hii, adhabu inatakiwa ili kuwarekebisha wahalifu, kutenda haki na kubainisha haki na batili. Kitabu kinaenda mbali na kueleza jinsi maisha ya Mtume wa Allah yalivyokuwa yamejaa usamehevu. Mtume Muhammad (rehema na amani ya Allah zimshukie) siyo tu aliwasamehe waliomkosea katika mambo binafsi bali pia aliwatendea wema. Hii ndiyo mifano ya kuigwa kama kitabu, ‘Tabia za Mfano za Marafiki wa Allah,’ kinavyotufunza.

Tags
Show More
Back to top button
Close
Close