1. Fahamu Usiyoyajua4. Jamii

KING KOBRA: Nyoka mkali akichokozwa

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka ndiye aliyeumba ulimwengu wote na viumbe vyote bila usaidizi wa yoyote, na Yeye ndiye anayeuendesha ulimwengu huu. Kwa hivyo, Yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa kwa sababu hakuna yoy– ote aliyemsaidia katika uumbaji.

Kuna viumbe wengi ulimwenguni, tunaowafahamu na tusiyowafahamu ambapo kila uchwao wavumbuzi wanaleta taarifa ya uvumbuzi wa viumbe wapya. Katika safu hii, leo tutamtazama nyoka aitwaye
‘King Kobra.’ King Kobra ni nyoka ambaye aliye katika kundi la ‘elapidae’, nyoka wenye ngozi nzito kiasi. Wataalamu wa elimu ya viumbe husema kuwa kuna zaidi ya aina 200 za kobra, wakiwemo Indian kobra, Egyptian kobra, Cape kobra, blacknecked spitting cobra , Monocled kobra na huyu King kobra ambaye ndiye mkubwa zaidi.

King Kobra wanapatikana zaidi Asia tu, huwezi kuwakuta Amerika, Ulaya wala Afrika. Katika Bara la Asia, King Kobra hupatikana sana India, Myanmar,Vetnam, Tailand na Kusini mwa Asia.

Miongoni mwa nyoka wenye sumu, huyu ndiye mkubwa kuliko wote. Nyoka huyu anaweza kufikia urefu wa kati ya futi 18.5 hadi 18.8 sawa na mita 5.6 hadi 5.8.

Madume ya nyoka hawa ni wakub– wa kuliko majike, tofauti na nyoka wengine. Nyoka wengi, majike huwa ni wakubwa kuliko madume.

Kule Asia,hasa katika nchi za India na Srilanka, king kobra na baadhi ya nyoka wengine, ni alama kubwa katika dini za kibudha na kihindu. Nyoka huyu anatukuzwa, ana hadhi ya juu na hauliwi. Uislamu unaziangalia dini hizi kuwa ni dini potofu na ni za kishirikina.

Lakini katika dini ya Kiislamu, tunamtazama king kobra na nyoka wengine kama viumbe wengine na hawana utukufu wowote ule.

TABIA

King Kobra anapata hisia kwa kutumia ulimi wake kwani Allah, Mbora wa Uumbaji hakumjaalia kuwa na pua. Kwa maana hiyo, huvu– ta harufu kutumia ulimi.

King Kobra amejaaliwa kuweza kuona umbali hata wa kufikia mita 100, sawa na urefu wa kiwanja cha mpira. Nyoka huyu hana masikio lakini anafahamu kupitia chini ya ngozi (earth born vibration) kwa maana anahisi.

Inapotokea amemgonga kiumbe anaye mla, basi huanza kumla kabla hata hajafa. Hata hivyo, hii pia ni kawaida ya nyoka wengi kutokula mizoga. Nyoka huyu, hula kiumbe muda mfupi tu, na hatafuni bali hummeza mzima mzima.

King kobra anawinda wakati wa mchana na mara chache usiku. Nchi– ni Ugiriki, nyoka anayewinda mchana huitwa nyoka mla nyoka.Licha ya hatari aliyokuwa nayo, huyu king kobra, akikutana na binadamu huwa anamkimbia, lakini binadamu atamfuata, nyoka huyu huwa hatari.

Allah amemjaalia king kobra uwezo wa kuinuka theluthi ya mwili wake. Pia, anaweza kukugonga kisha akatulia hapo hapo, ila jua kuwa akifanya hivyo huwa anaacha sumu nyingi zaidi.

King Kobra anapenda kujificha na anapenda kukaa kwenye pori nene. wengi wanao umwa na nyoka huyu ni wale wenye tabia ya kucheza naye.

King Kobra ni nyoka ambaye hana hasira ndiyo maana wanamtumia sana kucheza naye. Lakini ijulikane kuwa,vifo vinavyotokana na nyoka huyu ni vichache mno ukilinganisha na vifo vya ajali au majambazi wanaoua watu wa kawaida. King Kobra ni nyoka pekee anayelinda mayai yake na ana andaa kiota chake mwenyewe. Hubaki pale mayai yake mpaka yatotolewe na kwa kuwa ni mkali hakuna mnyama atakayesogea. Jike huwa linazaa mayai 20–40.

CHAKULA NA ADUI YAKE

King kobra anakula ndege, panya na wadudu wengine lakini chakula chake kikubwa ni panya.Licha ya hatari ya king kobra kutokana na sumu yake kali, hana ujanja anapokutana na mnyama anayeitwa nguchiro.

NAMNA YA KUJILINDA NAYE

Wataalamu wanatuambia, unapo– kutana na king kobra, njia mojawapo ya kujilinda na nyoka huyu ni kwan– za, rudi nyuma, kisha vua shati lako au kofia umtupie chini baada ya hapo yeye huwa rahisi kushughulishwa na kile alichotupiwa kuliko wewe.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close