5. Fatawa

Mtu asiyeweza kufunga daima

Swali: Mimi nina umri wa zaidi ya miaka 70. Hivi sasa nimepitwa na Ramadhani kadhaa, na sijazilipa kwa sababu ya maradhi. Je, kwa utu uzima wangu ninalaz- imika kulipa hizi funga na kutoa fidia au nifidie tu? na kipi kiwango cha pishi kwa kulinganisha na kilo?

JawabU: Kama una matu- maini ya kupona unalazimika kulipa funga. Allah anasema: “Kwa aliye mgonjwa au aliye safa- rini, na atimize hesabu katika siku zijazo…” (Qur’an, 2: 185). Na kama uliacha kulipa funga kwa uzembe, na ulikuwa na fursa ya kutosha ya kulipa na hukufanya hivyo, hapo itakulazimu kulipa funga, kulisha masikini kwa kila siku, pamoja na kutubu kwa Al- lah kwa kuchelewa kulipa. Kad- halika, jua kuwa inakuwajibikia kutoa nusu pishi kwa kila siku uli- yochelewa kuilipa mpaka ikaing- ia Ramadhani nyingine bila ya udhuru.

Ama kiwango cha fidia ya fun- ga kwa aliye na udhuru wa kishe- ria wa kutofunga ni pishi moja (sawa na kilo mbili na nusu takriban). Sababu za kisheria za ruhusa ya kutofunga ni pamoja na utu uzima au maradhi yasiyo- tarajiwa kupona kwa uthibbitisho wa daktari (specialist) mtaalam na muaminifu. Na fidia yenyewe, kama tulivyosema, ni kulisha chakula kinachopendwa kwenye mji, kuanzia tende, mchele au vinginevyo. Watapewa fidia hiyo mafakiri na masikini. Pia inajuzu hata kumpa masikini mmoja.

Alikula baadhi ya siku za Ramadhan na hajalipa

Swali: Mimi nilifungulia kwa ugonjwa baadhi ya siku, na sikuweza kuzilipa kwa sababu ya maradhi niliyonayo. kafara yake ni nini? na si hivyo tu bali hata Ramadhan hii nayo si- wezi kufunga? Hii nayo ka- fara yake nini ?

JawabU: Mgonjwa anayesumbuliwa na maradhi anaruhusiwa kula, na wakati wowote atakapopata ahuweni atalipa deni linalomkabili. Allah anasema: “Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini basi atimize hesabu katika siku nyingine,” (Qur’an 2: 185). Madamu ulikula ndani ya Mwezi wa Ramadhan kwa kuumwa, Wala huna tatizo. Nasema hivyo kwa sababu mgonjwa na msafiri huacha ku- funga kwa ruhusa waliyopewa na Allah, na Allah hupenda kuona ruhusa aliyoitoa kwa waja wake inatumiwa.

Alifungulia na siku chache baada ya Ramadhan akafariki

Swali: kuna mtu aliumwa na hadi kuzidi- wa na maradhi na hivyo kushindwa ku- kamilisha funga, baa-

da ya siku 22, yaani al- ibakisha siku nane. ki- sha siku chache kabla ya kumalizika kwa Ramadhani alifariki. kwa siku alizoziacha tunawajibika kumfanyia kitu gani?

JawabU: Kuhusu huyo mtu aliyeumwa ndani ya Mwezi wa Ramadhani na kulazimika na ali- acha kufunga kwa sababu ya ma- radhi, na kisha kukutwa na umauti; huyo halazimiki kufanya kitu kwa siku alizoziacha kwani hakupuuza na wala hakuacha ku- funga kwa uzembe, bali kwa kuz- idiwa na maradhi. Katika mazin- gira haya, mtu huyo halazimiki kufanya chochote, kwa neno la Allah: “Allah haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo,” (Qur’an, 2: 286).

Mtu aliyekufa na deni la funga

Swali: kuna Muislamu al- ifariki wakati akiwa na deni la Ramadhani, je, anaweza akafungiwa au kulipiwa chakula? na en- dapo kama funga yenyewe ni ya nadhiri na si Ramad- hani, kwenye matukio mawili haya kutakuwa na hukumu gani?

JawabU: Ama kuhusu funga ya Ramadhani, mtu atakapokufa na huku akiwa anadaiwa siku za funga ya Ramadhani ambazo hakuzifunga kwa sababu ya ku- umwa, mtu wa aina hii atakuwa na moja ya hali mbili. Hali ya kwanza: ikiwa maradhi yaliende- lea na hakuweza kufunga mpaka alipokufa, halazimiki kufanya chochote, halipiwi funga wala ha- tolewi chakula, kwa sababu kili- chomfika ni udhuru kwake.

Hali ya pili: Endapo kama ali- pata ahueni kwa maradhi yaliyo- msibu na kumfanya ashindwe kufunga, mpaka akakutwa na Ra- madhan nyingine, na hakuwahi kufunga, na baada ya Ramadhani nyingine akafariki, basi katika mazingira kama haya italazimika alipiwe chakula kila siku kwa nia- ba yake.

Hii ni kwa sababu alizembea kulipa mpaka ikaingia Ramad- hani nyingine na kufikwa na kifo. Na kwenye suala hili la kujuzu ku- fungiwa, kuna hitilafu baina ya wanazuoni. Ama kuhusu funga ya nadhiri atafungiwa na ndugu zake kwa neno la Mtume (rehema na amani ya Allah imshukie): “Mtu atakayekufa na deni la fun- ga ya nadhiri, walii wake atam- fungia.”

Alifungulia siku 15 miaka 27 iliyopita

Swali nina miaka 50 na nilipitwa na fun- ga kwa siku 15. Funga hiyo niliyoikosa ilito- kea mara tu baada ya kuzaa mmoja wa wa- toto wangu miaka ishirini na saba iliyopi- ta, na sikuweza kulipa

kwa mwaka huo. Je, ninaweza kuilipa hivi sasa? na je, ninapata dhambi?

Jawabu: Katika hali hiyo, un- alazimika kufanya toba kwa Allah Aliyetukuka kwa kuchelewa kuli- pa, na unawajibika kulipa siku ul- izozitaja pamoja na kulisha masi- kini nusu pishi ya chakula pendwa cha mji kila siku.

Hakufunga na hakulipa kwa miaka mingi

Swali: kuna mwaka nili- fungulia nilipojiwa na siku zangu, na sikuweza kufun- ga hadi sasa, na imeshapita miaka mingi. Sasa ninataka kulipa siku za funga nili- zoziacha, lakini sikumbuki ninadaiwa siku ngapi, ni- fanyeje?

JawabU: Unalazimika ku- fanya mambo matatu: Mosi, fan- ya toba kwa Allah kwa uzembe wa kuchelewa, na kujuta kwa yaliyo- pita kwa kuzembea, na uazimie kutoirudia tena tabia hii. Allah anasema:“Na rudini, enyi Wau- mini kwenye kumtii ili mfaulu” (Qur’an 24: 32). Huku kuchelewesha ni uovu na kufanya

toba kwa Allah ni wajibu.
Pili: Uharakishe kulipa funga,

kwa kiasi unachokumbuka, kwa sababu Allah haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kile inachokiweza. Zile siku unazodhani uliziacha ndizo unazolazimika kuzilipa. Kama unadhani ni siku kumi, basi utalipa siku kumi. Na kama utadhani ni zaidi au chini ya siku kumi, funga zile zinazojiri kwenye dhana yako.

Tunasema hivyo kwa sababu ya neno la Allah: “Allah haikalifi- shi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo,” (Qur’an 2: 286), na kwakauliyakeAllahTa’ala: “Basi mcheni Allah kama mwezavyo,” (Qur’an, 64: 16).

Tatu: Kila siku utalisha masi- kini kama una uwezo wa kufanya hivyo na unaweza ukampa masi- kini mmoja. Na kama mhusika ni fakiri na hawezi kulisha chakula, hapo halazimiki zaidi ya kufanya toba. Na chakula kilicho wajibu kulisha kila siku ni nusu pishi ya chakula cha mji, ambacho ni sawa na kilo moja na nusu.

kulipa funga kwa aliyefungulia kwa sababu ya mimba

Swali: nilikuwa mjamzi- to katika kipindi cha Ram- adhan na sikufunga, na baadae nilikuja kufunga mwezi mzima na kutoa sadaka. Haukupita muda nikashika uja uzito mwingine na ilikuwa ndani ya mwezi wa Ramadhan na sikufunga, nikaja kufunga siku baada ya siku kwa kipindi cha miezi miwili, bila ya kutoa sadaka. Je, kwa tukio hili ninalazimika kutoa sadaka?

JawabU: Ikiwa uliogopa ku- funga kwa kuigopea nafsi yako au mimba yako, hapo unaruhusiwa kula, na utalazimika kulipa pekee. Suala lako katika mazingira hayo halitofautiani na mgonjwa, asiye- mudu kufunga, au anayeiogopea nafsi yake. Allah anasema: “Na mwenye kuwa mgonjwa au safa- rini basi atimize hesabu katika siku nyingine,” (Qur’an 2: 185).

Je, kutokwa na maji ya Ujauzito kunafunguza

Swali: kuna mwanamke alifikwa na Ramadhani aki- wa na mimba ya miezi tisa, na alipokuwa mwanzoni mwa mwezi alitokwa na maji, na si damu. aliendelea na funga na huku maji maji yakimtoka, na hali hii ilim- tokea miaka kumi iliyopita. ninachouliza: Je, huyu mwanamke analazimika kulipa kwa kufunga na huku maji maji yanamtoka?

JawabU: Iki-wa hali halisi ni kama unavyoeleza, funga yake ni sahihi, na wala halazimiki kulipa.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close