1. Fahamu Usiyoyajua

Sababu za matatizo ya kiuchumi na suluhisho lake

Nchi zote duniani hufanya juhudi kubwa katika kujenga uchumi imara na kuletea maendeleo kwa watu wake. Nimeeleza katika makala iliyopita mitazamo miwili tofauti kuhusu suala la maendeleo.

Kujenga uchumi imara na kuleta maendeleo iwe kwa misingi ya Kiislamu au vinginevyo ni kazi ngumu na yenye kuhitaji umakini mkubwa kwa upande wa viongozi na wanaoongozwa.

Nina maana kuwa, si jambo la viongozi pekee kusema hiki na hiki tunachofanya ndiyo maendeleo au ndiyo ukuaji wa uchumi. Ikitokeya hivyo, wananchi wana kila sababu ya kuhoji aina hiyo ya maendeleo inayosemwa na viongozi wao.

Na jambo hili la wananchi kuhoji limekuwa likijitokeza mara kadhaa kwa sababu mbili; ya kwanza, kuko- sekana ushirikishwaji wa wanan- chi katika majadiliano ya maende- leo wayatakayo na uchumi imara wanaoutaka (lack of public partici- pation). Katika hili, je watendaji wa serikali wanakusanya maoni yetu na kuyafanyia kazi?

Ya pili, tabia ya viongozi na wana- siasa kuhodhi maamuzi ya matumizi ya rasilimali mbalimbali katika mae- neo yao (dominance of political elite in decision making on resource uti- lization).

Mambo haya mawili yanahitaji kusahihishwa. Ili kufanikiwa kusa- hihisha mambo haya, tunahitaji kujiuliza tatizo au matatizo ya kiu- chumi yanayowakabili watu wetu ni ya sampuli gani?

Wachumi kama Lionel Robins wanaona kuwa chanzo cha tatizo la kiuchumi la watu wetu ni uhaba wa rasilimali (scarcity of resourc- es). Wataalamu hawa wanasema, wananchi wana mahitaji mengi lakini rasilimali za kukidhi mahitaji hayo ni chache.

Lakini kwa upande wa wachumi wa Kiislamu, matatizo ya kiuchumi yanayowakabili watu wetu yanachu- kuwa katika sura kadhaa.

Kukosekana kwa fursa sawa

Binadamu ni viumbe vya Allah na wote wanahadhi na mahitaji sawa ya msingi katika kuendesha maisha yao ya kila siku.

Mfano, binadamu wote wanahitaji kula, kunywa, kupata elimu, kupata ajira, kupata matibabu, kupata fursa za kujiongezea mapato, kugombea nafasi za uongozi, kutoa maoni na ushauri, kudai haki katika vyombo vya sheria na kadhalika.

Tatizo la kiuchumi kwa watu wetu hujitokeza pale mamlaka fulani inapokua haitoi fursa sawa (Lack of equal opportunities) kwa watu wote kujipatia mahitaji yao.

Mfano, tulieleza wiki iliyopita mifano kadhaa kuhusu fursa za mikopo kutoka Baraza la Uweze- shaji Kiuchumi ambazo haziwapi fursa Waislamu kunufaika kutokana na kuambatanishwa na masharti ya riba, ingawa sehemu ya fedha za Waislamu ndiyo zinazoendesha mifuko hiyo kwa kupitia kodi mbalimbali. Katika fursa za ajira serikalini, Waislamu wamekuwa wanalala- mika kuwa ni wachache mno mion- goni mwao wanaopewa fursa hizo. Kadhalika, katika fursa za elimu ya juu, kuna malalamiko kuwa idadi ya Waislamu ni mdogo kuliko wengine.

Kwa ujumla inapotokea kuwa watu hawana fursa sawa za kujipa- tia mahitaji yao, hilo ni tatizo linalohitaji umakini mkubwa kulitatua na inawezekana. Haya sio mambo ya kupuuza bali yatakiwa kuyafanyia kazi kwa umakini mkubwa.

Ubora wa maisha

Binadamu kwa uhalisia wake ni mjumuiko wa kiwiliwili na roho. Hivyo, ubora wa maisha ya binadamu upo katika kujengewa uwezo wa kiimani (spiritual) na uwezo wa kuyamudu mazingira yake (materials).

Tatizo la kiuchumi lipo katika kutafuta njia maridhawa zenye kuweka uwiano baina ya mambo haya mawili ili binadamu huyu aweze kufikia kilele cha kuwa na utu na vitu (quality of life).

Sera za kiuchumi zenye kujenga fursa za kuwa na vitu zinapelekea watu kuwa mtu-vitu (materialist). Athari yake ni kuwa na ongezeko la wizi, rushwa, dhuluma na maovu mengine.

Sera zenye kujenga fursa za kuwa na imani zinapelekea kuwa na watu waliojitenga na ulimwengu wao (spiritualist). Athari yake ni kuwa na watu wanaojitenga na kufanya kazi.

Kwa hiyo, mambo yote haya mawili yanahitajika kwa binadamu ili kuwa kamilifu kama alivyoumbwa na Mola wake, awe na utu na vitu ili apate ustawi wa ubinadamu na mahitaji yake.

Uadilifu na haki

Tatizo la mwisho la kiuchumi kwa mtazamo wa Kiislamu ni namna gani ya kumlinda mtu mwenye rasilimali yake ikiwemo kipawa, maarifa au kitu dhidi ya wale ambao wana- taka kumnyonya au kumpokonya au kumdhulumu.

Ikishindikana kumlinda mtu huu mwenye rasilimali, maisha yake yataathirika na hivyo fursa baina ya wananchi itakosekana.

Kwa mfano, kuna wananchi wengi mno ambao wanamiliki ardhi laki- ni hawana hati miliki za viwanja hivyo. Hawa wapo katika hatari ya kupoteza mali zao kwa kudhulumiwa na wananchi wenzao au hata na watumishi wa serikali wasiokuwa waadilifu.

Mfano wa pili ni utaratibu wa kuwa ardhi yote ni ya serikali na mwenye hati amekodi tu (leasehold). Utaweza si mzuri kwani unaweza kuwawe- ka wananchi wengi katika hatari ya kupoteza mali zao baada ya muda wa kukodi kuisha (lease) na hasa ikiwa yule aliyekodishwa au mwenye hati hiyo hakuomba kuendelea kuikod- isha ardhi hiyo (lease renewal) ndani ya muda uliowekwa.

Jambo hili sio la kufikirika bali limetokeya kwa baadhi ya wananchi wa Kenya ambao walijikuta nyumba zao zikibomolewa katika mji wa Nai- robi na wamiliki wapya kwa kuwa hawakuisha (renew) hati zao! Waka- ti hawa wakikumbana na tatizo hili, baadhi ya wananchi wenzao wana hati za kudumu na sio kukodishwa (freehold).

Kwa upande wa pili iwapo sheria zetu hazikidhi aina mbalimbali za miamala au ufanyaji wa biashara hilo ni tatizo la kiuchumi na kijamii. Kwa mfano, sheria na kanuni zili- zopo za biashara ya bima ya Kiis- lamu sasa hivi hazikidhi matakwa ya biashara hiyo. Hivyo basi, kanuni mpya zinahitajika kwani ukosefu wa kanuni hizo mpya ummepelekea kukosekana bima ya Kiislamu nchini Tanzania.

Kutokana na sheria na kanuni kutokidhi mahitaji ya bima ya Kiis- lamu, sehemu ya wananchi wananufaika na sehemu nyingine hainufaiki na huduma za bima na kulipwa fidia wakati wa majanga. Hawa ambao hawaidiki ni kwa sababu moja tu ya msingi  nayo ni kuwa bima zilizopo zinaenda kinyume na mafunzo ya dini yao!

Kwa upande mwingine, sheria zenye kuingilia haki ya umiliki mali zinahitaji mabadiliko. Kwa upande wa vyombo vya mahakama lazima viwe na uwezo mkubwa wa kusikili- za kesi kwa wakati na haraka ili kila mwenye haki yake aweze kuipata na kunufaika.

Hivyo, kwa ujumla, ni suala la msingi kwa sera, sheria na vyombo vya mahakama kusimame katika uadilifu na haki.

Mwenyezi Mungu anasema “Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusima- misha uadilifu…” [Qur’an, 4:135].

Kwa kuhitimisha, matatizo yetu ya kiuchumi si uhaba wa rasilimali pekee na wingi wa mahitaji peke yake bali pia yanachangiwa na uko- sefu wa fursa sawa, ubora wa maisha yenye uwiano baina ya utu na vitu na ukosefu wa uadilifu na haki.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close