1. Fahamu Usiyoyajua

Pundamilia: Mnyama mpole, mwenye huruma

Pundamilia, kitaalamu anajulikana kama ‘equids’ na kwa wanaopenda mbwembwe za lugha ya kiingereza, pundamilia huitwa, ‘zebra’, dume hujulikana kama ‘stallin’, na jike hufahamika kama ‘mare’. Huyu ni mnyama mwenye uwezo wa kuishi hadi miaka 20.

Inasemekana chimbuko la pundamilia hasa ni Kusini mwa Afrika; nao hupendelea zaidi kuishi kwenye maeneo ya mbuga na nyika. Maeneo mahususi ambayo pundamilia mara nyingi hupatikana ni kama vile ukanda wa mbuga, savana, ukanda wa misitu, kwenye vichaka vya miiba, milimani na kwenye vilima vya pwani.

Pundamilia ana uwezo wa uwezo mkubwa wa kusikia, kuona na kukimbia kwa haraka, kiasi cha kilometa 65 hadi 70 kwa saa. Mtoto wa pundamilia huweza kukimbia saa moja tu baada ya kuzaliwa. Pundamilia wana miraba mingi myeusi ya mkato usoni na miguuni, na pia ni wanyama wanaofahamika sana kwa rangi yao ya pekee ya michirizi myeupe na myeusi.

Upekee wa michirizi na tabia za pundamilia unawafanya kuwa miongoni mwa wanyama wanaofahamika sana kwa binadamu. Michirizi yao huwa na mpangilio tofauti kwa kila pundamilia mmoja. Zaidi ya hayo, wataalamu wa masuala ya viumbe wanaamini kuwa asili ya pundamilia ni mwenye ngozi nyeusi ila tu kafunikwa na mistari ya rangi nyeupe.

Mistari ya pundamilia humsaidia kujificha kutokana na maadui zake. Inaweza kuwa rahisi sana kumuona pundamilia katika maeneo ya kawaida ya binadamu, lakini awapo porini hasa kukiwa na mwanga mwingi au giza, si rahisi kwa adui kumuona. Mistari hiyo pia huhuisha ulinzi dhidi ya maadui zake kwani adui hawezi kumchukua pundamilia mmoja katika kundi lake kwa urahisi. Wastani wa urefu wa wanyama hawa ni kati ya futi 3.5 hadi 5 hadi mabegani, na pia wana wastani wa uzito wa kati ya kilo 200 mpaka

Wanyama hawa wana uwezo mzuri wa kuona na kusikia. Pia, pundamilia, hulala hali ya kuwa wamesimama. Pundamilia wana nywele ndefu shingoni. Pia wana nywele ndefu kati ya masikio na ukwato, kama walivyo farasi na kihongwe ambao ni katika jamii yake. Pundamilia ana miguu myembamba na mirefu kiasi. Wembamba huu wa miguu humuwezesha kutembea kwa urahisi na vilevile kukimbia.

Pundamilia ni mnyama jasiri asiyeogopa kupambana na adui zake kwa mateke. Adui wa pundamilia mara nyingi ni simba, fisi, mbwa mwitu na binadamu ambaye humwinda kwa ajili ya nyama na ngozi. Mara tu wanapovamiwa, pundamilia hukimbia upande mmoja na mwingine katika mfumo wa zigzag ili kumchanganya adui.

Pundamilia ni mnyama mpole, mtulivu, mwenye huruma na apendaye ushirikiano

Pundamilia ni wanyama wenye kuchangamana sana na mara nyingi huonekana kwenye makundi madogo na hata makubwa. Pundamilia ni mnyama anaependa umoja na ushirikiano na wanyama wengine. Mara nyingi utamkuta na swala, twiga, nyumbu nk. Hata hivyo, pundamilia jike, mara nyingi, hubeba mimba akiwa na umri wa miaka mitatu na baada ya mwaka mmoja ndama wa pundamilia huwa amezaliwa.

Tabia ya kushangaza ya mnyama huyu ni kuopenda kwake kuishi katika kundi la familia yenye pundamilia watano hadi ishirini [20]. Kundi hilo la familia linajumuisha pundamilia dume mmoja, majike kadhaa pamoja na wadogo. Pia, katika kundi, dume ndilo huwa na dhamana ya kuilinda familia hiyo dhidi ya maadui.

Pundamilia ni mnyama mpole, mtulivu, mwenye huruma na apendaye ushirikiano. Mmoja wao akiugua, pundamilia kushindwa kutembea kwa haraka. Kundi la familia hiyo hupunguza mwendo ili kumsubiri mwenzao mgonjwa. Aidha, iwapo pundamilia mmoja katika familia akipotea, familia huchukua jukumu la kumtafuta kwa siku kadhaa.

Hata hivyo, familia zenye pundamilia watano hadi 20 wakati mwingine huweza kuungana na familia nyingine na kufanya kundi kubwa na kila kundi huwa na mpangilio wake. Aidha, baadhi ya madume ya pundamilia yasiyo na familia pia huweza kuungana na kuunda kundi la ‘makapera’.
Pundamilia wazee hushabihiana kwa kiasi kikubwa lakini madume na majike mara nyingi hutengana na familia zao na kuunda familia nyingine.

Pundamilia huwa makini sana wakati wa mchana; na wakati wa usiku hupendelea kula sehemu zenye nyasi fupi ili kujikinga na maadui.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close