1. Fahamu Usiyoyajua

Panya: Viumbe waharibifu wa mazao

Ndugu yangu msomaji, hakika Mwenyezi Mungu Aliyetukuka ni Mmoja na wa Pekee. Hakuna kinachoweza kufananishwa na Mwenyezi Mungu, hakuzaa kwamba anaweza kurithiwa, na wala hakuzaliwa kwamba anaweza kushirikishwa na wengine. Hakuna mwingine kama Yeye. Hana anayelingana naye, wala mpin-
zani, na hana mwenza wa kuandamana naye. Usingizi haumpitii, wala halali. Muumba wa vitu vyote, ikiwemo huyu panya ambaye leo tunamzungumzia.

Panya ni wanyama wadogo jamii ya mamalia walio katika kundi linalotambulika kitaalamu kama ‘muridae.’ Panya wana meno mawili ya mbele kwa kila taya na mwanya kati ya meno ya mbele na magego unaotambulika kitaalamu kama ‘diastema.’

Wataalamu wanasema kuna aina takribani 2,500 za panya duniani kote, wenye rangi, ukubwa na maumbile tofauti, na vilevile wataalamu wanasema, idadi ya panya inaendelea kuongezeka siku baada ya siku. Kwa upande wa Tanzania, kuna aina za panya si chini ya aina 20, wakiwemo panya shamba, panya michanga, panya miraba, panya wa darini, panya mbilikimo, kiruka njia, sengi na panya miiba. Katika makala hii, nitaangazia aina za waharibifu ambao wanapatikana karibu mikoa yote nchini. Hebu tuone aina hizi za panya.

AINA ZA PANYA
Aina moja wapo maarufu ya panya ni panya shamba (mastomys natalensis). Hawa ni panya waharibifu shambani hasa katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara na hupendelea kuishi porini na mashambani. Panya hawa wana uwezo wa kuzaa na kuongezeka kwa wingi katika kipindi cha muda mfupi. Jike huweza kuzaa hadi watoto 20 kwa mpigo.

Panya wa aina hii hushambulia mazao ya nafaka, mazao ya mizizi, mazao jamii ya kunde pamoja na pamba; na hushambulia siyo tu mbegu zilizopandwa bali pia miche, mazao yaliyokomaa shambani hadi yale yaliyohifadhiwa ghalani. Panya wengine wanaovamia mashamba na kuharibu mazao ni panya michanga na panya miraba. Aina nyingine ya panya waharibifu ni wa darini (rattus rattus) ambao huishi majumbani na hupendelea kukaa katika paa la nyumba. Kama ilivyo kwa panya shamba, aina hii ya panya hupatikana karibu mikoa yote ya Tanzania na huweza kushambulia mazao yaliyo ghalani kama vile nafaka, mihogo, viazi, maharage, pamba na karanga. Pia kuna panya wanaitwa panya mbilikimo. Panya hawa wanapendelea kuishi ndani ya nyumba au maghala. Wakati mwingine, panya hawa hutoka nje kutafuta chakula.

CHAKULA
Wanataalamu wanamuweka panya katika lile kundi la wanyama walao vitu vyote (omnivorous). Panya hula kila kitu lakini wanapendelea zaidi nafaka kama mahindi, mpunga na mtama; mizizi kama mihogo na viazi; mazao ya mafuta kama alizeti na karanga;jamii ya kunde kama mbaazi, na maharage; na vilevile mboga , kama vile nyanya matango, matikiti, maboga na kadhalika.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close