1. Fahamu Usiyoyajua

Nyoka wa Baharini (Sea snake). Ana sumu kali kuliko nyoka yoyote

Hakika Allah Muumba wa kila kitu ndiye pekee anayestahiki kuabudiwa. Ameumba mbingu na ardhi, Jua na Mwezi, bara na bahari. Ni Yeye pia ndiye aliyeumba viumbe wa bara na baharini, na ni Yeye pia anayetoa riziki. Allah Aliyetukuka peke yake ndiye anayemiliki na kuendesha maisha yetu na hivyo basi ni Yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa.

Namna bora ya kumjua Mwenyezi Mungu ni kupitia viumbe wake kwani kuwepo kwa viumbe ni ishara ya kuwepo pia aliyeumba. Moja ya viumbe wa Allah ambaye tukizingatia maumbile yake tunaona utukufu wa Allah Aliyetukuka ni nyoka wa baharini, maarufu zaidi kwa Kiingereza kama ‘Sea snake’. Nyoka wa baharini, nyoka huyu ni aina mojawapo ya nyoka wenye sumu kali.

Nyoka huyu yupo katika kundi la ‘elapidae,’ ambao ni nyoka wenye meno ya mbele, na wenye sumu kali. Katika kundi hili wamo pia koboko na kobra.

Kuna aina takriban 69 za nyoka wa baharini, kwa mujibu wa wataalamu wa elimu ya viumbe. Kati yao, wapo wanaoishi kwenye maji muda mrefu na muda mchache nchi kavu. Wapo wengine ambao maisha yao yote ni ndani ya maji na hawa ndiyo wengi zaidi.

Miili yao ilivyoumbwa inaendana na mazingira ya maji. Ina maana wakati nyoka wa kawaida wana umbo la duara chini, kwa upande wa hawa wapo bapa (flat). Licha ya kuwa wanaishi baharini, nyoka hawa hawana mapezi (gills) kama ilivyo pia kwa nyangumi. Hivyo inawabidi kila mara watoke nje ya bahari kupata hewa. Mikia ya nyoka hawa wa baharini pia ni bapa na hii inatajwa ni kwa ajili ya kuwapa urahisi kuweza kupiga maji.

Miongoni mwa nyoka wa baharini, kuna aina moja aitwaye ‘hydrophis platurus’, wana sumu kali kuliko nyoka yoyote uliyewahi kumsikia.

Wengi wa nyoka hawa wana maumbile yanayowafanya washindwe kutembea ardhini. Hata hivyo, kwa huruma za Allah, licha ya hatari ya sumu yao kali, Allah amewajaalia kuwa wapole. Katika nyoka ya jamii hii ambao ni wapole ni pamoja na yule mwenye sumu kali zaidi, ‘hydrophis platurus’.

Ni aina moja tu ya nyoka hawa aitwaye ‘bict’ ndiyo angalau ni wakali kidogo na huyu ndiye anayehusika zaidi katika kuua binadamu. Bict anapatikana sana kwenye bahari yenye maji joto kama Bahari ya Hindi na Pacific.

Hata hivyo neno moja la angalizo ni kuwa, nyoka wengi hawapendi kumgonga binadamu. Hata inapotokea nyoka amemuona binadamu na ikawa binadamu hajamuona, basi mara nyingi nyoka atamkwepa mtu huyo. Hata wale wanaogongwa na nyoka, aghalabu ni kwa sababu waliwakanyaga kwa bahati mbaya au walioonesha kutaka kuwadhuru. Ni hivyo hivyo kwa nyoka wa baharini.

Makala moja ya runinga niliyoiangalia hivi karibuni, ilionesha kuwa, wengi ambao waligongwa na nyoka wa baharini ni wavuvi ambao walikuwa wakivua samaki. Uzazi Katika uzazi, kama ilivyo desturi ya nyoka wengi, nyoka hawa wa baharini nao hutaga, ingawa hawa wana tofauti kidogo, kwani mayai yao yanaanguliwa tumboni (ovoviviparous). Na kuna Hata aina chache ya samaki wa baharini ambao wanataga nchi kavu (oviparous).

Mambo 5 usiyoyajua kuhusu nyoka wa baharini

  • Samaki wa baharini wanapokuwa ndani ya maji huwa hawaoni vizuri.
  • Mara nyingi Mtu anapoumwa na nyoka hawa, meno hubakia katika sehemu aliyong’atwa Utafiti mmoja wa mwaka 2018 inaonesha hakuna kifo cha mwanadamu kilichoripotiwa kutokana na nyoka hao.
  • Sumu ya nyoka hawa inafanyakazi polepole – kuanzia nusu saa hadi saa kadhaa. 
  • Baada ya kuumwa na nyoka hawa, baadhi ya dalili zinazoweza kujitokeza ni pamoja na mwili kukakamaa, kutokwa jasho, misuli kuuma, macho kugeukageuka juu chini na kushindwa kuhema vizuri.
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close