1. Fahamu Usiyoyajua

Nyani gelada, anayepatikana Ethiopia pekee

Naam ndugu yangu msomaji wa safu hii karibu tena katika ukurasa wetu huu wa Fahamu Usiyoyajua, ambapo wiki hii tunajifunze kuhusu nyani mwenye ngozi nyekundu aitwaye kwa Kiingereza ‘The Gelada Monkey’. Ndugu yangu msomaji, nyani huyu anapatikana katika milima ya Semien huko nchini Ethopia tu, na si kwingineko kokote duniani.

Kimuonekano, nyani huyu mwenye ngozi nyekundu kifuani amejaaliwa wastani wa urefu wa takriban sentimita 62 na uzito wa kilo wastani wa takriban 18. Nyani gelada ni mkubwa na amejaaliwa manyoya mengi lakini dume wana manyoya mengi zaidi hasa kwa nyuma.

Ukimtazama usoni pamoja na miguuni, nyani hawa wamejaaliwa rangi nyeusi. Mkia wao ni mfupi tofauti na nyani wengine. Kifuani wana ngozi nyekundu isiyo na manyoya lakini kwa dume imezungukwa na manyoya meupe.

Dume huwa na majike yake lakini imewahi kuonekana dume anachepuka huku akijua anadanganya kwa kujificha. Majike hukomaa wakiwa na miaka minne hadi mitabno na madume hubaleghe wakifikisha kati ya umri wa miaka mitano hadi saba. Viumbe hawa wameonekana na kusikika kuwa na sauti mbalimbali, ila jike ana sauti fulani pale anapotaka dume limpande.

Chakula

Kwa mujibu wa wataalamu, nyani gelada ni mla manyasi na mimea (herbivorous) ingawaje baadhi husema hali mimea bali anakula manyasi tu (graminivorous).

Uzazi

Yanapokuwa katika hali ya kutaka dume, majike ndio hufuata dume. Majike yanapokuwa katika hali hiyo, rangi ya kifua inazidi wekundu na hutoka malengelenge. Dume akiona hali hiyo hunusa nyuma na kumpanda jike. Jike akipandwa, hubeba mimba kwa siku 179 sawa na miezi sita kasoro siku chache.

Mambo 11 usiyoyajua kuhusu nyani gelada

  • Uchunguzi wa angani uliofanyika mwaka 1970 ulionesha kuna nyani gelada 500,000 nchini Ethopia. Tangu wakati huo, maeneo wanayoishi gelada yameingiliwa na shughuli za za kimaendeleo za binadamu ikiwemo kilimo.
  • Nyani gelada ambao hutamkwa ‘jeh – lah – da’ wana vidole vifupi sana. Ufupi wa vidole vya nyani hao umewasaidia kupanda miamba na miti huko juu ya milima.
  • Nyani gelada wanaishi kijamaaa tena katika kundi kubwa. Kila kundi linakuwa na kiongozi ambaye ni dume.
  • Madume ya nyani gelada ni wakubwa na wana manyoya mengi zaidi kuliko majike.
  • Kiongozi wa kundi wa nyani ngeleda anapozeeka anaporwa madaraka miongoni mwa madume wanaochipukia ambao tayari wamekomaa
  • Hata hivyo, kilicho tofauti kwa nyani wa Ethopia ni kwamba, dume kiongozi anapozeeka hafukuzwi kundini kama ilivyo kwa simba bali huporwa tu yale madaraka ya kuongoza kundi, na kupewa jukumu jingine, mathalan kulinda watoto.
  • Kwa upande mwingine, kitendo cha kiongozi kuporwa madaraka na dume linalochipukia, si jambo rahisi. Mara nyingi huwa na mpambano mkali na kelele nyingi, huku wengine wakiunga mkonbo huku au kule.
  • Nyani gelada ni pekee katika familia ya wanyama hawa ambao hula majani na mbegu wakiwa wamekaa chini wakichomoa majani kwa mikono na kula.
  • Nyani gelada anapatikana nchini Ethopia pekee na si kwingine popote duniani, ingawa inatajwa kuwa zamani waliwahi kuwepo katika nchi za Congo na Tanzania. Nyani gelada wanaishi katika ukewenza, yaani dume lina haki ya kukutana na majike wengi. Pia, ingawa wanaweza kukutana muda wowote katika mwaka, wanyama hawa huzaliana zaidi wakati wa mvua. Mimba yao hudumu kwa kwa miezi 5 – 6.
  • Nyani gelada huzaa mtoto mmoja ambaye hunyonya kwa kati ya mwaka mmoja hadi mmoja na nusu. Mtoto huyo, kisha, atatalelewa na mama mpaka akifikia umri wa kujitegemea, lakini baba hushiriki kidogo sana katika malezi.
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close