1. Fahamu Usiyoyajua

Ndege Mzuri Mwenye Madaha: Tausi

Naam ndugu msomaji wa safu hii ya ‘Fahamu Usiyoyajua,’ juma hili ninakuletea dondoo za ajabu kuhusina na ndege anayevutia machoni na mwenye madaha, tausi.

Tausi ni ndege maarufu aliyewashangaza na anayeendelea kuwashangaza watafiti kwa namna Mwenyezi Mungu Aliyetukuka alivyomuumba.

Tausi ana mdomo mrefu kiasi, manyoya mengi yaliyopambwa kwa rangi mbalimbali nzuri zenye kung’aa ajabu. Miongoni mwa rangi hizo ni kijani na samawati ( bluu), ambazo pia ndio rangi za kichwani.

Ndugu yangu msomaji hizo rangi nilizokutajia alizo jaaliwa tausi si hizi za kawaida. Ukisikia kijani basi ni kijani ya kung ’aa sana, halikadhalika samawati.

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka amewajaalia tausi kuwa tofauti kimuonekano baina ya jike na dume. Kwanza, tausi dume ana umbo kubwa ukilinganisha na tausi jike. Pia, Dume la tausi linapendeza zaidi kuliko hata jike

Dume la tausi limepambwa kichwani na kitu kama mwamvuli hivi, na pia lina mkia mzuri uliopambwa na rangi mbalimbali. Ikiwa hajatanua mkia wake huwa na urefu hadi kufikia futi sita. Pia mkia wa tausi dume una madoadoa kama macho, na madoa hayo yanaonekana vizuri pale anapotanua mkia wake. Madoa hayo yana rangi ya kijani iliyozungukwa na njano kidogo na samawati.

Kwa wapenzi wa lugha ya kigeni ya Kiingereza, tausi dume anaitwa ‘peacock’ na jike anaitwa ‘peahens.’ Vifaranga vyao vinaitwa ‘peachiks’ na wakiwa kundi wanaitwa Bevy.

Wastani wa umri wa kuishi wa tausi ni miaka 10 hadi 20. Pia, itambulike kuwa, tausi wapo wa aina tatu.

Aina mbili za tausi wanapatikana Asia: India, na Sri Lanka na aina moja ipo Afrika sehemu za Kongo.

Maajabu 15 ya tausi:
• Wanapokuwa wadogo huwezi kutofautisha kati ya jike na dume kwa sababu wanakuwa na rangi ya aina moja tena mchanganyiko.
• Licha ya manyoya yao kuwa kivutio kikubwa kwa watu lakini hawazaliwi wakiwa na manyoya. Manyoya yanaota baada ya miezi sita.
• Majike ndio wanaovutiwa na madume hasa kutokana na uhodari wao wa kuweza kutanua mkia wao kwa madaha.
• Jike pia hutanua mkia wake ila kwa malengo mengine. Mara nyingi hufanya hivyo kuwalinda watoto wake au kuwafukuza majike wenzie wasimchukulie dume.
• Majike yana vigezo vyao vya kuchagua madume, na kigezo hicho ni mikogo ya hali ya juu katika kutanua mkia wake.
• Chakula cha tausi ni wadudu, nyoka wadogo, mijusi, mbegu, matunda yanayoitwa Beris. Pia, hula maua.
• Utafiti wa karibuni katika Jarida la Tabia za Wanyama la Uingereza (British Journal of Animal Behavior) unaonesha kuwa dume la tausi linapotanua mkia wake kuna sauti ya ajabu inatoka ya kumuita jike ambayo binadamu hawezi kuisikia, ila kwa vyombo maalumu.
• Kila Baada ya miezi Tisa dume la tausi hubadilika rangi.
• Kama unayahitaji manyoya ya tausi haina haja ya kuwaua. Wenyewe wanayatoa kila baada ya mwaka na kisha yanaota mengine.
• Ingawa tausi hawapendi sana kuruka, ukweli ni kuwa wanaweza lakini hawafiki mbali.
• Mikia ya tausi wa Kongo wanapoitanua ni midogo kuliko wale wa India

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close