1. Fahamu Usiyoyajua

Mdudu Hatari Lakini Haumi

Msomaji wa Fahamu Usiyoyajua, juma hili ninakujuza tabia za mdudu aitwaye, ‘Nairobi Fly.’ Huyu ni jamii ya wadudu wanaopenda kuviringisha kinyesi, kwa Kiswahili ‘Tuta wale,’ kwa Kiingereza ‘Beettle’ lakini wadigo wanamuita Chidundu.

Nairobi fly ana miguu sita; kulia mitatu na kushoto mitatu, lakini haruki. Pia, ana antenna mbili. Wadudu hawa, kwa mbele wana rangi nyekundu na nyeusi, na ukubwa wao ni kati ya milimita 6-10. Ni wadudu wadogo, ukizingatia milimita 10 ndio sawa na sentimita moja.

Mwili wa Nairobi fly umegawanyika sehemu tatu, kama walivyo wadudu wengi, yaani kichwa chenye rangi nyeusi, katikati kwenye rangi nyeusi na nyekundu na mkiani ana rangi nyeusi. Wadudu hawa wanaishi nje ya nyumba kwenye majani ila wanapenda zaidi sehemu zenye umande na mwanga wa taa na ndio maana usiku wanapenda kuingia kwenye majumba.

Wadudu hawa wanapatikana sana Afrika ya Mashariki ingawa ni wengi zaidi nchini Kenya. Nairobi fly pia wanapatikana kwa wingi Liberia, ambako watu huko wanawaogopa sana.

Mwaka 1998, Nairobi Fly walizaliana  kwa wingi sana. Pia, Novemba 2007, katika kaunti ya Kitui Mashariki, watu wengi waliugua ugonjwa wa ngozi na kutibiwa hospitali kutokana na Nairobi Fly. Hii maana yake wadudu hawa wana madhara kwa binadamu.

 

Maajabu saba ya Nairobi fly
  • Licha ya kuwa mdudu hatari, Nairobi Fly hawaumi wala hawadungi ila mwili wake una kemikali ya sumu mbaya. Akikudandia kisha ukamminya, mwili wake unatoa kemikali hiyo ya sumu inayoathiri ngozi na kupata wekundu, mbabuko na mchubuko unaoonekana zaidi kwa watu weupe. Ugonjwa huu kitaalamu unaitwa, ‘Peadurus Dermatitis.’
  • Mara nyingi Nairobi fly akikudandia, sehemu zinazoathirika zaidi ni shingoni, usoni na kwenye mikono.
  • Unapomminya mdudu huyu unaweza usione dalili yoyote ya ngozi kuathirika kwa saa 12-24.
  • Ikitokea amekudandia kisha ukababuka ni hatari kidogo kwa sababu ngozi ina bacteria ambao wanaweza kuingia ndani (Secondary Bacterial Infection).
  • Majimaji ya Nairobi fly yakiingia jichoni yanaweza kuleta shida hasa ukiumwa kisha ukafikicha jicho. Jicho linaweza kuwa jekundu na kuvimba. Katika hili, msomaji utambue kuwa kuna maambukizi ya macho yanayosababishwa na virusi na mengine yanasababishwa na bakteria. Pia, shida nyingine ya macho nyingine husababishwa na mzio (allergies).
  • Nairobi fly wanazaliana kwa wingi na kuongezeka idadi wakati wa msimu wa mvua kwa hiyo maeneo yenye wadudu hao kwa wingi wanapaswa kuchukua tahadhari mapema.
  • Ikitokea Nairobi fly amekudandia, usimshike kwa mkono wala usimminye bali mpulize tu. Hakikisha unamtoa pole pole kwenye ngozi kuepuka majimaji yake.
Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close