1. Fahamu Usiyoyajua

MAMBA: Reptilia aliyeumbwa kuwinda na kuogelea

Safu hii wiki hii inakuletea habari za mamba, mnyama aina ya reptilia, mwenye umbo kubwa na anayeishi majini na nchi kavu. Mamba wanapatikana  katika Bara la Afrika, Asia, Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, na Australia

Mamba wapo wa aina nyingi. Kuna alligators, cainmans, gharial. Bahati mbaya hatuna majina ya Kiswahili ya aina hizo za mamba. Mbali ya aina hizo, kuna mamba wanaopatikana kwenye maji matamu (crocodlylus Niloticus) na kuna wanaopatikana kwenye maji chum-
vi (crocodylus porosus) ingawa hawa si wengi.

Mamba aina ya alligators na gharical wana muonekano sawa, lakini wataalamu wanasema wapo tofauti katika familia za kibaiologia (maumbile yao). Mamba wote wanaishi nusu majini nusu nchi kavu (semi Aquatic) na pia wanaishi kimakundi. Karibia Mamba wote wanapatikana katika nchi za joto, isipokuwa aina ya alligator. Kawaida mamba huwa hawapendi baridi.

Inaelezwa kuwa, mamba ni wanyama ambao wapo hatarini kutoweka kwani mpaka sasa kuna takriban aina 14 za mamba ambao hawapo tena. Mamba wa maji chumvi ni wakubwa sana kuliko hawa wa maji matamu lakini pia mamba dume ni wakubwa kuliko majike.

UZAZI

Katika uzazi, mamba wanataga mayai kuanzia 7 hadi 95, kulingana na aina. Mamba hutotolewa siku 80 na kutotoa kwao pia hutegemea hali ya hewa. Joto likiwa kubwa wanatotoa mapema. Mamba wanapotaka kutaga, wanakwenda ardhini,yaani nje ya maji, na kuchimba shimo kisha hufukia mayai yao kwamchanga kwa ajili ya ulinzi.

CHAKULA
Kwa upande wa chakula, mamba ni ‘carnivorous’ yaani anakula wanyama wengine. Mamba anakula wanyama wadogo wadogo wenye uti wa mgongo kama vile swala na digidigi. Mamba pia wanakula viumbe wasio na uti wa mgongo wakiwemo aina fulani ya minyoo.

Mambo 15 usiyoyafahamu kuhusu mamba

 • Ukichunguza maumbile ya mamba, ameumbwa kwa ajili ya kushambulia na kuogolea.
 • Urefu wa mwili wake unamsaidia kuogolea na miguu inamsaida kupiga mbizi.
 • Miguu ya mamba ina ngozi iliyoshikana kama ile ya bata (webbed) ambayo inawasaidia kuondoka ghafla na kukata kona ghafla.
 • Miguu ya mamba pia huwasaidia kutembea katika maji ya kina
  kifupi.
 • Mdomo wa mamba una kiungo fulani karibia ya koo kinachozuia maji yasiingie ndani pale anapofungua mdomo.
 • Mamba ana aina kadhaa za misuli mdomoni inayomsaidia kufungua mdomo na kufunga. Katika kufunga mdomo, misuli yake ina nguvu sana kiasi kwamba akikubana, hutoki. Hata hivyo, mamba akibana mdomo, ukimfunga hata kwa kamba nyembamba, ni ngumu
  kufungua.
 • Ana uwezo na kasi kubwa ya kushambulia ukiwa karibu naye. Ukiwa umbali wa mita moja, kwa mfano, kukukamata ni rahisi sana, yaani ni kama kufumba na kufungua macho. Hakika, huwezi kumuepuka au kumkimbia. Hata nyoka pia wana tabia hii.
 • Meno ya mamba yaking’oka yanaweza kuota tena hata mara 50
 • Mamba huweza huishi miaka hadi 35.
 • Mamba wanakaribiana sana na ndege kuliko wanyama kwa kuwa wanataga
 • Mamba wanaona vizuri sana usiku kuliko mchana na ndio maana hupendelea sana kuwinda usiku. Hii ni faida kwao kwani idadi kubwa ya viumbe wanaowawinda hawaoni vizuri usiku.
 • Tumbo la mamba lina tindikali (acid) sana kuliko kiumbe yoyote mwenye uti wa mgongo. Lina uwezo wa kumeng’enya vitu vigumu kama mifupa, pembe na kwato.
 • Licha ya kwamba huvuta hewa ya oksijeni, mamba wanaweza kukaa ndani ya maji muda mrefu.
 • Kitoto cha mamba kikiwa ndani yai kinapokaribia kutoka huwa kinapiga kelele. Vitoto hivyo pia vina meno ya kutoboa yai na hivyo kujitotoa. Mama naye akisikia wanalia anaenda kusaidia.
 • Vitoto vya mamba vikishajitotoa, mama yao anawachukua kwa kuwabeba mdomoni na kuwapeleka kwenye maji.
  Mamba ni wazuri sana katika
  kunusa harufu na kusikia pia

 

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close