1. Fahamu Usiyoyajua

Capyabara:Panya mkubwa kuliko wote

Naam Ndugu yangu msomaji, juma hili nataka tukamtazame kiumbe anayefahamika kama capyabara (kitaalamu au hydrochaerus) panya mkubwa anayepatikana Amerika ya Kusini.

Panya huyu kule Brazil huitwa capivara, Colombia na Venezuela wanaitwa chiguire lakini katika Nchi za Argentina, Praguay, na Uruguay huitwa capincho. Majina yake si hayo tu, nchini Peru huitwa ronsco.

Panya hawa wanapendelea kuishi katika sehemu za Savanna na katika misitu minene kando ya mito na sehemu zenye mabwawa na maji.

Ndugu yangu msomaji, wanyama hawa wanaishi kijamaa na wanaweza kuwa katika kundi kubwa kiasi cha kufika hata mia moja, ingawa kwa kawaida huwa kumi hadi 20.

Panya hawa ni tofauti na viumbe wengi. Wao hawapo hatarini kutoweka ila huwindwa sana kwa kitoweo na ngozi yao. Inasemwa kuwa katika mafuta yao wana girisi, jambo linalopelekea kupendwa sana.

Urefu wa panya huyu ni kati ya sentimita 106 hadi 134 wakati uzito wake unafika hadi kilogramu 35 hadi 106.

Ajabu ni kuwa, majike ya panya hawa ni mazito zaidi. Jike lililowahi kuweka rekodi lilikuwa na uzito wa kilogramu 91. Umri wao wa kuishi ni miaka nane hadi 10.

Chakula

Capybaras ni katika viumbe walao nyasi na majani (herbivorous) na wakati mwingine huwa wanakula hata kinyesi. Pia, Capybaras wana tabia ya kucheua chakula walichokila kisha wanakila tena.

Maadui

Maadui wakubwa wa panya huyu ambao wanamuwinda kwa kitoweo ni nyoka hususan anakonda, tai, na chui aina zote.

Uzazi

Katika uzazi, capybaras wanabeba mimba inayodumu kwa siku 130 hadi 150. Makutano yao ni ndani ya maji ambapo jike ndiyo huita dume.

Mara nyingi Capyabara huzaa watoto wanne ingawa husemwa pia anaweza kuzaa watoto kuanzia mmoja hadi nane akiwa.

Wiki moja baada ya vitoto vya capybaras kuzaliwa huanza kula nyasi huku pia wakiendelea kunyonya.

Mambo 12 usiyoyajua kuhusu Capyabara

  • Allah Aliyetukuka amemjaalia capyabara uwezo wa kulala ndani ya maji huku pua yao wakiichomoza nje.
  • Capyabara ni waogoleaji wazuri sana. Wanaweza kuzama ndani ya maji kwa dakika hata tano bila ya kutoka.
  • Kama ilivyo kwa panya wa kawaida, meno ya capyabara yanarefuka kila wakati.
  • Capyabara wakati wa kiangazi huwa wanakula majani yanayopatikana juu ya miti mifupi. Hii ni kwa sababu nyasi huwa zinakuwa chache sana.
  • Mnyama huyu hutumika sana Amerika ya Kusini kwa nyama na ngozi, ingawa nyama ya baadhi ya maeneo ya mwili wake haifai kuliwa.
  • Capyabara ndiye panya mkubwa kuliko wote duniani.
  • Miguu yao ina ngozi nyembamba ambayo imeshikana kama bata hali ambayo huwasaidia katika kuogelea.
  • Capyabara huwa wana tabia ya kula kinyesi chao hasa nyakati za asubuhi.
  • Capyabara wana tabia ya kucheua chakula wanachokila kisha hurudia kukila. Utafiti umeonesha kuwa nyasi wanazokula ni ngumu sana ndiyo huzicheua na kuzila tena.
  • Msimu wao wa kuzaliana hutofautiana mwaka mzima kulingana na makazi wanayoishi na kupatikana kwa wenzi wao.
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close