1. Fahamu Usiyoyajua

Canada lynx: Paka wa maeneo ya baridi kutoka Amerika ya Kaskazini

Naam ndugu yangu msomaji, hakika Allah, Mbora wa Uumbaji ana utukufu wa hali ya juu. Utamaizi hayo kwa kutazama viumbe mbalimbali alivyoviumba katika ulimwengu wake huu. Juma hili, nakuletea taarifa za mmoja katika viumbe wa Allah, jamii ya paka aitwaye canada lynx.

Canada lynx ni paka wa saizi ya kati anayepatikana katika bara la Amerika ya Kaskazini kuanzia Alaska, Canada na Marekani. Mnyama huyu anafahamika pia kwa jina Jla kisayansi la Lynx Canadensis.

Paka huyu ana ana manyoya marefu na mengi. Masikio yake ni Pembe tatu na kwa juu kuna vinywele virefu vyenye rangi nyeusi. Pia, ana mkia mfupi sana kiasi unaweza utadhani umekatwa lakini si hivyo bali ndiyo maumbile yake.

Usoni, canada lynx ana mashurubu marefu. Pia, namna mnyama huyu ameumbwa kuakisi mazingira aliyopo kwa maana ya kuhimili baridi. Hapo ndiyo utaona uhodari wa Allah katika uumbaji wake.

Kila kiumbe ambaye Allah amemuumba anaendana na mazingira yaliyopo ndiyo maana utashangaa kuna viumbe wengine wanahimili sehemu za joto na wakipelekwa sehemu za baridi hawawezi kuishi na wengine wanahimili sehemu za baridi wakipelekwa sehemu za joto hawawezi kuishi. Mfano wa wanyama hawa ni canada lynx.

Canada lynx ana urefu wa sentimita 48 hadi 56 na uzito wa kilogramu 5 hadi 17. Pia, myama huyu ana meno 28. Allah amejaalia kuwa umri wa kuishi wa wanyama hawa kuwa ni miaka 15.

Chakula na uzazi

Wataalamu wa elimu ya viumbe wanasema canada lynx ni katika viumbe wanaokula nyama (carnivorous). Wanyama hawa pia hupendelea sana kuwinda sungura wa barafu, hasa nyakati za usiku.

Katika uzazi, canada lynx anazaa na kunyonyesha. Kawaida, canada lynx, huzaa watoto kuanzia mmoja hadi nane; na akishazaa ananyonyesha watoto wake kwa muda wa majuma 12.

Canada lynx pia ni katika viumbe ambao wana kipindi maalum cha kupandana. Kipindi hicho ni mwezi wa tatu hadi wa nne.

Mambo 10 usiyoyafahamu kuhusu canada lynx

  • Kupungua na kuongezeka kwa canada lynx kunategemeana sana na wingi wa sungura. Sungura wakipungua, na hawa paka nao wanapunguza kuzaa. Vilevile, sungura wakiwa wengi, paka hawa nao huzaliana kwa wingi.
  • Inasemekana canada lynx nao hufugika. Inatajwa kuwa, wapo watu wanaowafuga kama paka wa nyumbani.
  • Adui mkubwa wa canada lynx ni binadamu. Hii ni kwa sababu binadamu humuwinda mnyama huyu kwa ajili ya ngozi yao. Jambo jema ni kuwa, kuna sharia za kuwalinda kwa sasa.
  • Canada lynx hupendelea sana kuishi kwenye misitu minene; na huko ndiko wanakopatikana sungura ambao ndiyo chakula chao pendwa.
  • Licha ya miguu yake kuwa mirefu, canada lynx hawezi kutembea haraka (kwa kasi). Hata anapowinda, hukamata zaidi kwa kunyata.
  • Canada lynx ni miongoni mwa paka waogeleaji muogeleaji wazuri sana na ni fundi wa kupanda miti.
  • Wanapokula, canada lynx wanaweza kuhifadhi chakula kwa matumizi ya baadae (akiba).
  • Madume ya canada lynx yanapenda kukaa peke yao.
  • Canada lynx ni hodari sana katika kuwinda nyakati za usiku, labda kwa sababu uwindaji wao ni wa kunyatia.
  • Mara nyingi canada lynx akifanikiwa kumkamata sungura anambana kichwani kwa mdomo wake na kisha anarudi naye nyuma kule alipotoka tayari kwenda kumla.
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close