1. Fahamu Usiyoyajua

Buibui mweusi: Wadudu wanaokulana

Sifa njema zote anastahiki Mola Muumba wa mbingu na nchi na vilivyomo baina ya mbingu na ardhi. Ni Hakika yenye hakika kuwa Allah ndiye pekee anayestahiki kuabudiwa kwani yeye ndiye Muumba wa kila kitu, Jua na Mwezi, bara na bahari, na wanyama wa bara na baharini. Ni yeye pia anayeruzuku viumbe wote aliowaumba.

Katika kuendelea kubainisha ukubwa wa viumbe wa Mwenyezi Mungu kupitia viumbe wake, leo tunamzungumzia kiumbe wa ajabu aitwaye buibui mweusi. Huyu ni mdudu mwenye rangi nyeusi ya kung’ara au kijivu giza. Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana kwa lugha ya kigeni huitwa, ‘Black Spider.’ Jina la kisayansi la buibui mweusi ni ‘hLatrodectus.’

Buibui mweusi anaweza kuishi kati ya mwaka mmoja hadi miaka mitatu, kulingana na aina. Rangi ya buibui mweusi hubadilika na kuwa nyeusi ya kung’ aa pindi anapokuwa mkubwa.

Hata hivyo, dume la mdudu huyu linakuwa na rangi nyekundu isipokuwa tumboni huwa na rangi nyeupe. Buibui ni mdudu mdogo mwenye urefu wa wastani wa sentimita 3.8.

Kwa mujibu wa wataalamu wa elimu ya wadudu, kuna takriban aina 31 za buibui weusi, na aina zote hizo wanapatikana sehemu mbalimbali duniani ispokuwa maeneo yenye baridi kali (upande wa kaskazini mwa dunia).

Wadudu hawa wanapatikana katika sehemu nyingi za Amerika ya kaskazini, Ulaya, Australia na Afrika hasa kaskazini. Kwa hapa Tanzania, kuna aina mbalimbali za buibui. Buibui maarufu zaidi nchini Tanzania anaitwa Latrodectus.

Buibui mweusi ni mdudu mdogo lakini ana sumu kali inayodhuru mishipa ya fahamu (neuro toxin). Allah, Mbora wa Uumbaji amewajaalia kuwa na tezi kubwa ambazo hutoa sumu hiyo inayoweza kudhuru wanyama wakubwa, na wakati mwingine hata binadamu. Husemwa kuwa, kuumwa na buibui jike ndiyo kuna madhara zaidi kwa binadamu.

Maelezo haya yanatisha lakini jambo la kufariji ni kuwa ni nadra sumu ya kiumbe huyu kusababisha kifo ingawa inaweza kumtesa mtu. Ijapokuwa anatisha lakini kuuma kwake ni nadra kusababisha kifo kwa binadamu ila akikudunga sumu yake itakutesa sana.

UZAZI NA CHAKULA

Katika mambo ya kushangaza zaidi kwa buibui huyu ni ile tabia ya jike akimalizwa kupandwa tu huwa anamla dume. Tabia hii kitaalamu inaitwa ‘sexual carnibalism.’ Ni kitendo hicho cha jike kumla dume ndiyo kilichopelekea jike kuitwa buibui mjane kwani anakosa mwenza kila baada ya kumaliza kupandwa.

Angalizo ndugu yangu msomaji. Siyo aina zote za buibui huwa wanakula madume yao. Hapana! Ni aina hii tu ya buibui mweusi ndiyo mwenye tabia hiyo. Tabia hii ilithibitika kwenye maabara walipofanyiwa uchunguzi.

Buibui mweusi anataga kwenye hariri. Mayai yanatoka yakiwa yamefunikwa na ngozi nyembamba (sacks), na huwa kwenye sacks 4-9. Kila sacks inakuwa na mayai 20 mpaka 900.

Kwa upande wa chakula, buibui mweusi anakula wadudu wadogo wakiwamo inzi, mbu, panzi, tuta (bittle) na katapila.

Mambo 10 usiyoyafahamu kuhusu buibui mweusi

  • Watoto wa buibui huyu wakishazaliwa na kukua kidogo, wanaweza kumla mama yao tena mzima mzima.
  • Licha ya kuwa hatari, buibui mweusi hapendi kumuuma binadamu. Hufanya hivyo kujilinda tu ikiwa hana pa kukimbilia.
  • Akizidiwa akawa hana namna ya kujiokoa, hujilaza katika hariri zake na kujifanya kama amekufa (play dead). Jiulize, nani amempa akili hiyo?
  • Buibui mweusi haoni vizuri ila anategemea zaidi mitetemo au mitikisiko ya kwenye ardhi. Mitikisiko hiyo inawaonya kuhusu viumbe. Kadri mtikisiko unavyokuwa mkubwa, anajua kiumbe ajaye naye ni mkubwa.
  • Ili kujilinda asiliwe na buibui jike, buibui dume huwa hakurupuki kumpanda jike. Anaangalia kwanza ameshakula!? Dume likijiridhisha kuwa jike ameshakula ndiyo anakwenda kumpanda. Ikitokea jike amekula huwa hamli dume hata anapopandwa.
  • Dume la buibui linajua kwa haraka kama jike ameshakula au bado. Ni kupitia zile hisia za kemikali katika hariri ndiyo anajua kama kuna mdudu ameliwa.
  • Buibui mweusi huwa hapendi sana kukaa kwenye hariri yake, bali mara nyingi hutumia hariri kama mtego akisubiri mdudu ajiingize kwenye hariri na kabla hajajitoa anakwenda kumdunga.
  • Buibui mweusi hawezi kutafuna sumu aliyoimwaga kwa mdudu. Buibui mweusi humfyonza mdudu baada ya kulainika na kuwa majimaji.
  •  Inasemekana sumu ya mdudu huyu ni kali (zaidi ya mara 15) ya nyoka anayeitwa Rattle snake
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close