1. Fahamu Usiyoyajua

Buibui mjane mweusi: Wadudu wanaokulana

Sifa njema zote anastahiki Mola Muumba wa mbingu na nchi na vilivyomo baina ya mbingu na ardhi. Ni Hakika yenye hakika kuwa Allah ndiye peke anayestahiki kuabudiwa kwani yeye ndiye Muumba wa kila kitu, Jua na Mwezi, bara na bahari, na wanyama wa bara na baharini. Ni yeye pia anayeruzuku viumbe wote aliowaumba.

Katika kuendelea kubainisha ukubwa wa viumbe wa Mwenyezi Mungu kupitia viumbe wake, leo tunamzungumzia kiumbe wa ajabu aitwaye buibui mjane. Huyu ni mdudu mweÅkung’aa… na weusi huzidi hung’aa kadri anavyokua.

Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana kwa lugha ya kigeni huitwa, ‘black widow spider.’ Jina la kisayansi la buibui mjane

mweusi ni ‘Latrodectus’ na anaweza kuishi kati ya mwaka mmoja hadi miaka mitatu, kulingana na aina.

Hata hivyo, dume la mdudu huyu linakuwa na rangi nyekundu isipokuwa tumboni huwa na rangi nyeupe. Kiumbo, huyu ni mdudu mdogo mwenye urefu wa wastani wa sentimita 3.8. Na wapo takriban aina 31, na aina zote hizo wanapatikana katika maeneo mbalimbali ya dunia maeneo yenye baridi kali kule katika ncha ya Kaskazini.

Baadhi ya maeneo ambayo wadudu hawa wanapatikana ni Amerika ya Kaskazini, Ulaya, Australia na Afrika hasa Kaskazini,Vingawa hata kwetu Tanzania wapo. Wapo buibui wenye rangi tofauti tofauti ila huyu mjane mweusi ndiyo maarufu zaidi.

Buibui mjane mweusi ni mdudu mdogo lakini ana sumu kali inayodhuru mishipa ya fahamu (neuro toxin). Allah, Mbora wa Uumbaji., amewajaalia kuwa na tezi kubwa ambazo hutoa sumu hiyo inayoweza kudhuru wanyama wakubwa na wakati mwingine hata binadamu. Husemwa kuwa, kuumwa na buibui jike ndiyo kuna madhara zaidi kwa binadamu.

Maelezo haya yanatisha lakini jambo la kufariji ni kuwa ni nadra sumu ya kiumbe huyu kusababisha kifo ingawa inaweza kmtesa mtu.

Uzazi na chakula

katika mambo ya kushangaza Zaidi kwa buibui huyu ni ile tabia ya jike akimalizwa kupandwa tu huwa anamla dume. Tabia hii kitaalamu inaitwa ‘sexual carnibalism.’ Ni kitendo hicho cha jike kula dume ndiyo kilichopelekea kuitwa buibui mjane kwani anakosa mwenza kila baada ya kumaliza kupandwa.

Angalizo ndugu yangu msomaji.Siyo aina zote za buibui huwa wanakula madume yao hapana! Ni aina hii tu ya mjane mweusi ndiyo mwenye tabia hiyo. Tabia hii ilithibitika kwenye maabara walipofanyiwa uchunguzi.

Mjane mweusi anataga kwenye hariri. Mayai yanatoka yakiwa yamefunikwa na ngozi nyembamba (sacks), na huwa kwenye sacks 4-9. Kila sacks inakuwa na mayai 20 mpaka 900.

Kwa upande wa chakula,buibui mjane mweusi mweusi anakula wadudu wadogo wakiwemo inzi, mbu, panzi, tuta(bittle), na katapila.

Mambo usiyoyafahamu kuhusu buibui mjane

  • Watoto wa buibui huyu wakishazaliwa na kukua kidogo, wanaweza kumla mama yao tena mzima mzima.
  • Licha ya kuwa hatari, buibui mjane mweusi hapendi kumuuma binadamu. Hufanya hivyo kujilinda tu ikiwa hana pa kukimbilia.
  • Akizidiwa akawa hana namna ya kujiokoa, hujilaza katika hariri zake na kujifanya kama amekufa (play dead). Jiulize, nani amempa akili hiyo?
  • Buibui mjane mweusi haoni vizuri ila anategemea zaidi mitetemo au mitikisiko ya kwenye ardhi. Mitikisiko hiyo inawaonya kuhusu viumbe. Kadri mtikisiko unavyokuwa mkubwa, anajua kiumbe ajaye naye ni mkubwa.
  • Ili kujilinda asiliwe na buibui jike, buibui dume huwa hakurupuki kumpanda jike. Anaangalia kwanza ameshakula!? Dume likijiridhisha ameshakula ndiyo anakwenda kumpanda. Ikitokea jike ameshakula huwa hamli dume hata anapopandwa.
  • Namna dume la buibui linavyojua kama jike ameshakula au bado ni wa kipekee sana. Ni kupitia zile hisia za kemikali katika hariri ndiyo anajua kama kuna mdudu ameliwa.
Show More

Related Articles

Back to top button
Close