1. Fahamu Usiyoyajua

Bimbirisa Kimba [Beetle] Mdudu maarufu kwa kuviringisha kinyesi

Naam Ndugu yangu mfuatiliaji na msomaji wa safu hii ya ‘Fahamu usiyoyajua’, juma hili nataka nikufahamishe mambo mengi yamuhusuyo mdudu mwenye majina mengi. Baadhi ya Waswahili humuita, bimbirisa kimba, wadigo humuita ‘chidundu’. Pia wapo muitao ‘tuta.’ Waingereza wao humuita ‘beetle.’

Hawa ni wadudu walio maarufu sana. Wana miguu sita; kulia mitatu, kushoto mitatu, ingawa Allah Aliyetukuka amewatofautisha na wadudu wengine katika mbawa. Tunajua kuwa, wadudu wengine wana mbawa laini, hali ni tofauti kwa bimbirisa kimba. Hawa ni wadudu ambao Allah Aliyetukuka amewajaalia mbawa ngumu kuliko wadudu wowote.

Bimbirisa kimba ni wadudu wenye rangi za kung’ara sana. Yaani kama ana rangi nyeusi inakuwa ya kung’ara sana, kadhalika kama ni wa rangi ya samawati [bluu] au pinki na nyenginezo. Rangi yoyote iwayo hung’ara sana. Hawa ni wadudu ambao wanapatikana duniani kote, isipokuwa ncha ya Kaskazini na Kusini.

Pia, wadudu hawa hawapo baharini, lakini unaweza kuwakuta pembezoni mwa bahari. Wataalamu wanatueleza kuwa, wadudu hawa wapo wengi, takriban laki nne, na kwamba wenyewe ni asilimia 40% ya wadudu wote na ni asilimia 25% ya viumbe vyote.

Uzazi na chakula

Katika uzazi, bimbirisa kimba wanataga, na mayai yao yanapitia hatua nne yaani yai kisha kiwavi kisha pupa na mwisho bimbirisa kimba [beetle]. Kwa upande wa chakula, bimbirisa kimba wanakula mimea, minyoo wadogo na fangasi [utandu/ ukungu].

Mambo sita kuhusu Bimbirisa kimba

Bimbirisa kimba wana rangi mbalimbali za kupendeza lakini pia wapo wale ambao wana rangi inayofanana na mazingira waliyopo, yaani wanabadilika. Kama kwenye mchanga wanakuwa na rangi hiyo nk. Wazungu wanaita camouflage.

Wadudu hawa ni maaarufu tangu enzi za utawala wa Firauni na walikuwa wakitumika kwa mambo mbalimbali, ikiwemo kuwachora kama mapambo.

Bimbirisa kimba anapobeba kile kinyesi si kwamba ndio anategemea kile kama chakula Laaa! Bali huwa anakipeleka shimoni kwa ajili ya kutagia, ingawa kinyesi hicho ndio chakula cha kiwavi chake.

Dume la bimbirisa kimba linakuwa na taya kubwa kuliko jike.

Wadudu hawa hawapatikani kwenye bahari lakini wanaweza kupatikana katika maji baridi [matamu].

Jike linapatwa na dume kupitia harufu.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close