1. Fahamu Usiyoyajua

ARMADILLO: Mamalia mwenye joto hafifu Zaidi

Naam ndugu yangu msomaji, juma hili nataka tukamtazame kiumbe anayefahamika kama Armadillo. Huenda wengi wetu hatumfahamu kiumbe huyu kwa sababu tu haonekani katika maeneo yetu.

Armadillo hupendelea kuishi katika maeneo yenye joto na unyevunyevu. Wanyama hawa wanajulikana kwa miili yao midogo yenye rangi ya hudhurungi (zambarau) na mkia mrefu na mgumu, kichwa kirefu, macho madogo meusi, masikio marefu yaliyoelekea juu na miguu minne; miwili mbele na miwili nyuma.

Miili ya Armadillo imefunikwa kwa gamba gumu ambalo huwasaidia kujikinga dhidi ya mashambulizi ya wanyama wakali. Kichwa cha Armadillo kinafanana kidogo na panya, lakini wenyewe wanashabihiana na Kakakuona.

Wanyama hawa wanasifika kwa tabia yao ya kuchimba mashimo kwa kutumia kucha za miguu yao ya mbele na kisha kuingia ndani yake ili kujilinda na wanyama wakali.

Kwa mujibu wa wataalamu wa elimu ya viumbe, kuna takriban aina 20 za Armadillo na aina zote hizo zinapatikana katika nchi za Amerika ya Kusini na Kaskazini. Armadillo hulazimika kutafuta maeneo ya udongo wenye kichanga ili kupata wepesi wa kuchimba na kujipatia chakula chao pamoja na sehemu ya kulala.

Chakula na uzazi

Katika chakula, Armadillo hula wadudu jamii ya amfibia au reptilia kama konokono na funza kwa zaidi ya asilimia 90. Armadillo pia hula mimea, minyoo na mchwa.

Uzazi wa Armadillo huanza mwanzoni mwa msimu wa joto. Armadillo hubeba mimba inayodumu kwa miezi miwili hadi mitatu. Armadillo huchukua miezi 4 kurutubisha yai kabla ya kuzaa. Yai lililorutubishwa hugawanyika katika hatua nne za ukuaji wa mimba na kutoa mapacha wanne.

Watoto wa Armadillo huanza kujitegemea kuanzia miezi 6 hadi 12 baada ya kuzaliwa. Kwa kawaida Armadillo huzaa mtoto mmoja hadi 12 kwa uzao mmoja.

Mambo 6 usiyoyajua kuhusu armadillo

  • Armadillo wana uwezo wa kuchimba ardhini, hasa maeneo yenye udongo wa kichanga na wadudu wengi ili kujipatia chakula pamoja na sehemu ya kulala.
  • Armadillo wana uwezo wa kubeba bakteria wanaoambukiza ukoma kwa wanadamu (Mycobacterium leprae). Hata hivyo, si rahisi binadamu kupata maambukizi ya ukoma kutoka kwa Armadillo. Wanasayansi wanaamini kuwa mtu hawezi kuambukizwa ukoma na Armadillo isipokuwa kwa kumhudumia mnyama huyo mara kwa mara.
  • Miili ya Armadillo imefunikwa kwa gamba gumu ambalo huwasaidia kujikinga dhidi ya mashambulizi ya wanyama wakali.
  • Wanyama hawa hutumia muda wao mwingi kulala na hutafuta chakula wakati wa asubuhi na jioni. Kwa kawaida Armadillo hulala kwa saa 16 kila siku ndani ya mashimo yao.
  • Wakati wa uzazi na msimu wa baridi Armadillo hukusanyika katika vikundi ndani ya mashimo yao ili kupata joto jingi mwilini.
  • Kwa mujibu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Uhifadhi wa Asili (IUCN), wanyama aina ya Armadillo hawapo hatarini kutoweka.
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close