1. Fahamu Usiyoyajua4. Jamii

BASILISCUS: Mjusi anayetembea juu ya maji

Ndugu yangu msomaji, hakika Mwenyezi Mungu Aliyetukuka ni Mmoja na wa Pekee. Hakuna kinachoweza kufananishwa na Mwenyezi Mungu, hakuzaa kwamba anaweza kurithiwa, na wala hakuzaliwa kwamba anaweza kushirikishwa na wengine. Hakuna mwingine kama Yeye. Hana anayelingana naye, wala mpinzani, na hana mwenza wa kuandamana naye.

Mwenyezi Mungu hapitiwi na usingizi wala halali. Yeye ni Muumba wa vitu vyote, ikiwemo mwanadamu na pia viumbe wote ambao baadhi tumekuwa tukiwajadili katika safu hii.

Juma hili Acha tukaone ukubwa wa Mwenyezi Mungu kwa kumtazama kiumbe wake anayeitwa ‘basiliscus,’ ambaye mjusi anayeshangaza sana ukiangalia namna anavyoishi na maumbile yake. Mjusi huyu kitaalamu anaitwa Basilisk na anapatikana katika bara la Amerika ya Kati na Amerika ya Kusini.

Mjusi huyu anapenda kuishi pembezoni mwa mito na katika mapori makubwa yanayopatikana katika nchi zilizomo katika mabara hayo mawili. Mjusi huyu ana rangi ya kahawia na krimu na pia amejaaliwa kuwa na mdomo mkubwa. Madume ya mijusi hii wamejaaliwa kuwa na kifua kipana kidogo kuliko majike.

Anapokuwa mkubwa, urefu wake kutoka mkiani hadi kichwani ni takriban sentimita 76 ambazo ni karibu futi 2.5. Jike la Mjusi huyu anaweza kufikia uzito wa hadi gramu194. Ajabu ni kuwa mkia wa mjusi huyu unachukua karibu asilimia 75 ya mwili wake wote.

Wataalamu wa elimu ya viumbe wanaeleza kuwa, mjusi huyu ana uwezo wa kukimbia wa kilometa kwa saa anapokuwa juu ya maji. Licha ya kutambulika zaidi kwa kutembea juu ya maji, yeye pia ni hodari sana katika kuogelea na kupanda miti. Allah, Mbora wa uumbaji amemjaalia mjusi huyu uwezo wa kuzama chini ya maji na akatulia kwa muda wa hadi nusu saa.

Wataalamu hawajabainisha mijusi hawa wapo wa aina ngapi, ila wanakiri kusema wapo wa aina nyingi. Umri wao wa kuishi ni miaka saba ila umri huu ni kwa wale wa kufugwa. Kwa upande wa wale wa porini, umri ni mdogo zaidi kwa sababu ya hatari wanayokumbana nayo ya kushambuliwa na kuliwa na viumbe hatari.

Chakula, uzazi na adui zake

Mjusi basiliscus hula wadudu wadogo akiwemo bilimbisa kimba (bittle). Pia, mijusi hawa wanakula minyoo, maua, inzi, mayai na samaki wadogo. Kwa upande wa uzazi, mijusi basiliscus wanataga mayai kati ya 10 na 20. Pia, kwa kawaida hutaga kwa mafungu. Hii ina maana, kama atataga mayai 20, hatagi maya hayo yote muda mmoja. Anaweza kutaga mayai manne au matano, kisha akataga sehemu nyingine mayai matano au zaidi …hivyo hivyo… mpaka anafikisha 20.

Allah amejaalia baadhi ya viumbe kuwa ni chakula kwa viumbe wenzao. Kama ilivyo kwa mjusi huyu kuwa anakula viumbe wadogo niliokutajie awali, naye pia huliwa na wengine. Maadui wakubwa wa mjusi huyu ni ndege aina ya tai na baadhi ya wanyama.

Mambo10 usiyoyajua kuhusu basiliscus

  • Sababu inayomfanya mjusi basiliscus kukimbia nchi kavu na kutembea juu ya maji ni vitisho kutoka kwa adui zake.
  • Mwenyezi Munu amemjaaliwa mjusi huyu kuwa na miguu ya mbele na ya nyuma, lakini akitembea juu ya maji anatumia miguu ya nyuma.
  • Miguu ya mjusi basiliscus ni mipana na watafiti wengi wanasema chini ya miguu hiyo kuna vitu fulani kama sponji linatoa povu. Wataalamu wanasema, ni hali hiyo ya miguu yao ndiyo inayowafanya wasizame wanapotembea juu ya maji.
  • Wanapokuwa wadogo wanaweza kwenda umbali mrefu zaidi juu ya maji kuliko wanapokuwa wakubwa. Inatajwa kuwa mjusi basiliscus mdogo anaweza kukimbia umbali wa hadi wa mita 20.
  • Licha ya kuishi ndani ya maji mjusi basiliscus anaweza pia kuishi ardhini ambako ndiko hasa kwenye makazi yake ya kudumu. Mjusi basiliscus ana tabia pia ya kujificha chini ya majani kukwepa adui zake.
  • Wataalamu wa elimu ya viumbe wanamuelezea mjusi huyu kuwa ni bingwa wa kujificha anapoona adui, na kwamba anapokuwa nje ya maji anaweza kujituliza sehemu kwa muda mrefu bila hata kutikisika sehemu yoyote ya mwili wake
Show More

Related Articles

Back to top button
Close