4. Jamii

Athari ya Funga Katika Maadili ya Muislamu na Kujenga utu

unapozichunguza ibada zote ambazo mwenyezi mungu ameziwajibishia viumbe vyake, utagundua kuwa, zote zina Lengo moja, naLo ni kujenga na kuimarisha uhusiano na utangamano wa moja kwa moja kati ya mja na muumba wao.

Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu, na re- hema na amani zimfikie bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na jamaa zake, Maswahaba zake na wote wamfuatao kwa wema. Ama baada ya hayo, ibada katika Uislamu zina athari kubwa katika kuzirekebisha nafsi, kuzitakasa na uchafu na kurekebisha tabia. Na ibada ya funga ni miongoni mwa ibada zenye mchango mkubwa un- aoonekana katika kurekebisha tabia ya Muislamu, kuisafisha roho yake na kumfanya awe mtumishi mzuri kwenye dha- mana aliyokabidhiwa. Unapozichunguza ibada zote ambazo Mwenyezi Mungu ameziwajibishia viumbe vyake, utagundua kuwa, zote zina lengo moja, nalo ni kujenga na kuimarisha uhusiano na utan- gamano wa moja kwa moja kati ya mja na Muumba wao. Na kupitia ibada ndiyo un- aweza kumtofautisha muisla- mu anayefuata amri za dini yake na asiyefuta. Na ibada kwa hapa duniani zinafanana sana na vituo vya maisha, ambapo binadamu hupata fursa ya kusimama na kunong’ona mubashara na Mola wao mlezi, kwa njia ya kumuomba. Na mara nyingi binadamu anaposakamwa na kuzongwa na mambo hukim- bilia kwenye ibada na huji- pamba na uchaMungu na huji- tahidi kuwa na msimamo na kujitahidi kuzishinda anasa na kujiepusha na matamanio yanafsi. Aidha, ibada ni kiungan- ishi kati mja na Mola, na pia ibada ni nyenzo njema inayo- muunganisha mtu binafsi na jamii, na ibada pia humuandaa mtu binafsi na kumtayarisha katika mapambano na kuzika- bili changamoto za maisha. Na tunapoiangalia funga tu- naikuta ni alama miongoni mwa alama za Kiislamu zilizo tukufu na zilizo na athari kubwa katika maisha ya Muis- lamu, ya kiroho, kitabia, na ki- jamii. Na hiyo imesababishwa na tabia ya Mwezi wa Ramadhani kuwa ni msimu adhimu mion- goni mwa misimu ya heri. Naf- si ndani ya mwezi wa Ramad- hani, husafika na huwa karibu na Mola, milango ya pepo hu- funguliwa, na ndio mwezi uli- yoteremka Qur’an kwa Mtume Mtukufu (rehema na amani ya Allah iwe juu yake), Na Qur’an ndiyo muongozo wa watu na kipambanuzi baina ya haki na batili na ni ubainifu wa njia ya kheri. Aidha, ibada ya funga ni miongoni mwa ibada kongwe zilizotekelezwa na umati zilizo- pita. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Enyi mlio- amini! Mmelazimishwa ku- funga kama walivyolazimish- wa waliyokuwa kabla yenu ili mpate kumchaMungu,” (Qur’an, 2:183). Funga ni chuo cha kiislamu ambacho humlea mwanadamu kwenye nyanja zote, za kimwili, kiroho, kitabia na pia kijamii. Na funga ina falsafa na faida nyingi kwa upande wa mtu binafsi na jamii kwa ujumla. Miongoni mwa falsafa za funga ni kuwaonea huruma masikini kwani mtu aliyefunga anapo- hisi makali ya njaa hupata fur- sa ya kuwakumbuka kila mara na kuwaonea huruma watu wenye shida. Na mara nyingi huruma kwa binadamu hucho- moza kutokana na machungu. Na funga ni darasa la kivi- tendo linaloilea nafsi kivitendo kiasi kwamba wakati wowote inapotokea tajiri kumuonea huruma masikini na mwenye njaa, ndipo utu wa mtu wa ndani huchomoza. Na ibada ya funga humzoe- sha Muislamu kuwa na tabia ya subira kwa aina zake zote. Kwa mfano, aliyefunga huwa na subira katika utii, utayari wa kujiepusha na maasi, na kuwa na subira juu ya makadirio ya Mwenyezi Mungu yanayoumi- za. Na Mtume (rehema na am- ani ya Allah iwe juu yake) ameielezea athari hii alipose- ma: “Nao ni mwezi wa subira, na subira malipo yake ni pepo,” (Ibn Khuzayma). Aidha, miongoni mwa falsa- fa za funga ni kuleta usawa kati ya matajiri na masikini. Na funga ni mfumo madhubuti wa kivitendo: “Funga huifanya nafsi ihisi udugu sahihi, upen- do wa kweli pasipo kusubiri migogoro.” Funga humzoesha Muisla- mu kuwa na nidhamu, kupen- da umoja, uadilifu, usawa, up- ole, rehema, kuimarisha uhu- siano, kukimbilia kutenda heri, na kuilinda jamii na ufisadi. Na aliyefunga anapoidhibiti nafsi yake na mambo ya kidunia, hupata fursa ya kuhisi anay- oyahisi fukara na mwenye sh- ida. Nafsi na moyo wake huwa na huruma, upole, na ukarimu. Sadaka bora ni sadaka ya katika Mwezi wa Ramadhani. Imepokewa katika Sunna kuwa: “Kutoa katika mwezi wa Ramadhani kuna fadhila kubwa kuliko kutoa katika miezi mingine.” Na hilo limeelezwa na Hadithi ya Ibn Abbas (Allah amridhie) akise- ma kuwa Mtume (rehema na amani ya Allah iwe juu yake) alikuwa mkarimu mno, na ukarimu wake ulikuwa un- aongezeka wakati wa Ramad- hani.” Unapoingia Mwezi wa Ra- madhani Mtume (rehema na amani ya Allah iwe juu yake) alikuwa anawaacha huru mateka, humpa muombaji na kumtatulia matatizo mwenye matatizo. Na funga humfundisha Muislamu adabu. Ikitokea kama kuna mtu anajionesha hadharani kuwa amefunga la- kini hana adabu za funga, ameshindwa kuudhibiti ulimi wake na kuwasema wengine, kuwavunjia watu heshima, ameshindwa kuudhibiti mko- no wake kuwaudhi wengine, kuwachukia na kuwasaliti Waislamu wenzake; basi huyo funga yake ina mapungufu.Ni bora aidiriki nafsi yake, afanye upya toba yake, na ajie- pushe na maadili mabaya, tabia, matendo, na kauli chafu. Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema: “Mtu yeyote asiyeacha maneno ya uongo na kutenda vitendo viovu, Mwenyezi Mungu hana haja ya yeye kuacha chakula chake na kinywaji chake.” Ni ipi maana halisi ya fun- ga? Ikiwa mtu anafunga kwa kuacha kula na kunywa, lakini hajizuwii kutukana, mambo machafu, ulimi mchafu, na wala hawezi kuyazuwia macho yake na mambo yaliyokatazwa na Mungu? Ibn Rajab (Allah amrehemu) anasema: kuwa baadhi ya wema waliopita wal- isema: “Daraja ya chini ya fun- ga ni kuacha kula na kunywa”. Na Jabir (Allah amrehemu) anasema: “Unapofunga na yafunge masikio yako, macho yako, ulimi wako na ujiepushe na uongo, vitu vya haramu, uache kumuudhi jirani, na siku unayofunga uwe mnyenyekevu na wala usiifanye sawa siku unayofunga na siku ya kula mchana.” Na funga ina mafunzo ya ki- malezi, ambapo huilea nafsi kuwa na tabia ya kujituma, uvumilivu, ukakamavu, na kuyavumilia yanayokera. Aid- ha, funga hutufunza kushika- mana na maadili mazuri ya ki- jamii, kama ambavyo funga hutoa mafunzo ya kiroho na kuifungamanisha na Mwenye- zi Mungu. Si hivyo tu, kama ambavyo swala, funga na dhikri, dua, kukaa itikafu msikitini na kuji- tolea humlea Muislamu kui- marisha imani; vilevile funga nayo humlea Muislamu kuwa na tabia ya subira, ukakamavu na kuyashinda nguvu matama- nio ya nafsi na humpamba na tabia na maadili mema na kuwa na tabia nzuri.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close