2. Afya

Namna funga inatibu saratani

Karibu tena katika makala zetu zinazohusiana na faida za kiafya kinazotokana na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan. Bila shaka zipo faida nyingi tunazozijua na tusizozijua ambazo zinatokana na ibada hii tukufu.

Katika makala ya leo, tutachambua kwa undani ni kwa namna gani funga ya Ramadhan inaweza kuwa moja kati ya tiba za saratani na pia kwa namna gani funga hii inaweza kupunguza hatari ya kupata ugonjwa huu.

Chembe hai za mwili

Ndugu msomaji, ni muhimu kutambua kuwa, miili yetu imejengwa na chembe hai ndogo ambazo kisayansi hujulikana kama seli. Chembe hizi hupatikana katika maeneo yote ya mwili. Ni muunganiko wa chembe chembe hizi ndiyo hutengeneza viungo tofauti vya mwili.

Kwa kawaida, binadamu huwa na takriban chembe hai trilioni mia moja katika mwili siyo tu za aina tofauti bali pia hufanya kazi tofauti kutegemea na mahitaji ya mwili.

Licha ya kuwa chembe hizi ni ndogo sana kiasi cha kutoonekana bila ya hadubini maalum, jambo la kushangaza ni kuwa hujegwa na vijichembe vidogo zaidi (kiini, vinasaba, protini, mafuta na kadhalika) ambavyo ndivyo hudhibiti matukio yote yanayotokea katika chembe hai za mwili.

Matukio hayo yanayodhibitiwa na hivyo vijichembe ni pamoja na kuruhusu kuingia na kutoka kwa vitu mbalimbali katika seli, kudhibiti kuvunjika, uhai pamoja na vifo vya vya seli. Inakadiriwa kuwa, vifo milioni 96 vya seli hutokea kwa dakika.

Namna saratani inavyotokea

Kwa kawaida saratani zote huanzia katika chembe hai za mwili  aidha katika chembe hai moja tu au chache. Chembe hai hizi huwepo kwa idadi maalumu katika kila kiungo cha mwili. Vinasaba (genes) vilivyomo katika chembe hizi huhakikisha kuwa idadi ya chembe zinazozalishwa ni sawa kabisa na chembe zinazokufa. Hivyo, ikiwa kutatokea mabadiliko yoyote katika vinasaba (gene mutation) katika chembe hizi, chembe mpya zitakazozalishwa huyarithi mabadiliko haya na kusababisha kuharibika uwiano kati ya uzalishwaji na ufaji wa chembe hizi kwani chembe mpya zilizobeba mabadiliko huzalishwa kwa kasi zaidi kiasi cha kuishinda kasi ya ufaji.

Hali hii hupelekea mrundikano mkubwa wa seli hizi na mwishowe kutengeneza uvimbe ambao ndiyo saratani.

Mabadiliko ya chembe hai wakati wa kufunga

Kwa kawaida, kutengenezwa kwa chembe hai za mwili huwiana kabisa na kasi ya kufa kwa chembe hai hizo. Inapotokea kasi ya uzalishwaji wa chembe hizi kuwa kubwa kuliko kufa kwake, saratani huweza kutokea.

Tukiangalia kinyume chake, yaani kufa kukiwa kukubwa zaidi ya uzalishaji, kwa lugha rahisi tunaweza kusema, hiyo ni tiba ya saratani na ndiyo maana moja ya tiba ya saratani ni kuziua chembe hai kwa kutumia mionzi.  Kama tulivyoona katika makala zilizopita, wakati wa Ramadhan mwili hutumia akiba kubwa ya chakula cha ziada kilichohifadhiwa katika maeneo tofauti ya mwili ikiwemo katika chembe hai za mwili.

Wakati wa funga, idadi kubwa ya chembe hai za mwili huvunjwa (apoptosis) na kutoa malighafi ambazo hutumika katika matumizi mengine ya mwili.

Pia chembe hai hizi hujivunja na kujiua zenyewe (autophagy) na kuchukua malighafi zisizo na kasoro ili kuzalisha chembe hai mpya ambazo hazina kasoro hivyo kupelekea kuondolewa kwa idadi kubwa ya chembe hai zenye kasoro (zenye vinasaba vya saratani) na mwisho kupelekea kupungua kwa vimbe za saratani. Kitendo hiki kiitwacho kitaalamu ‘autophagy’ hupelekea kuuawa kwa bakteria na virusi ambao huenda wakawa ndiyo chanzo cha saratani husika.

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close