2. Afya

Mlo wa tende Unavyosaidia Kuandaa Futari Kamili

Kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (amani na rehema ya Allah zimshukie), mfungaji anatakiwa afungue kwa tende, maji au maziwa, halafu aswali Magharibi na baada ya hapo aendelee kula (futari kamili). Tukizingatia aina ya virutubisho (nutrients) vinavyopatikana katika mlo wa tende, tutaweza kuandaa mlo bora kabisa ambao tutaula baada ya mtu kukata swaumu kwa tende. Pia, kuzifahamu tende kutatusaidia kufanya uchaguzi sahihi wa matunda mengine tunayoweza kuyatumia pale tutakapo kosa tende, maji au maziwa kama vyakula vya kuanza kufuturu.

Ushahidi wa tende

Anas (Allah amridhie) ameele- za kuwa Mtume Muhammad (amani na rehema ya Allah zimshukie), alikuwa akifungua kwa tende mbichi zilizokomaa (fresh) kabla ya kuswali (Maghar- ibi), kama hizi hazikuwepo alifun- gua kwa tende zilizowiva na ku- kauka (mbivu), na kama hizi haz- ikuwepo alikunywa mafunda machache ya maji (Tirmidhiy na Abu Daud).

Faida ya tende

Kufuturu kwa tende ni jambo lenye faida kubwa kiafya kwa mfungaji. Maendeleo ya elimu ya sayansi yanatusaidia kuongeza ufahamu wetu juu ya thamani kubwa ya kilishe ya tende kwa bin- adamu. Kwa hiyo, ni matarajio yetu kuwa kila msomaji wa makala hii atajifunza kuhusu tende na kuanza kuzitumia, isipokuwa wagonjwa wa kisukari.

Tende ina sukari

Tende ina asilimia 60 mpaka 70 ya sukari aina ya glucose na fructose. Mtu akila tende, aina hii ya su- kari hunyonywa na utumbo na ku- unguzwa na seli na hatimaye ina- toa nguvu kwa haraka. Kwa mfun- gaji swaumu, nguvu hii humpa fu- raha na akili yake inatuama kwa haraka. Ndiyo kusema, haifai ku- futuru kwa vyakula vigumu kama vile hindi la kuchoma au ugali.

Tende ina vitamini

Tende pia ina vitamini aina ya C kiasi cha gramu 3, na kiasi kidogo cha vitamini B-complex. Tende zikiwa hazijawiva sana na mbichi (fresh) ndiyo zina vitamini nyingi zaidi. Aina hii ndiyo aliyokuwa anaitumia sana Mtume wetu (am- ani na rehema ya Allah zimshuk- ie). Watu wanahimizwa kujenga tabia ya kula matunda ambayo hayajaiva sana ili kupata vitamini zaidi. Matunda yaliyoiva sana yamepungua vitamini zake. Kinga ya mwili Vitamini mbalimbali huweze- sha mwili kuwa na kinga ya kupambana na maradhi. Pia baa- dhi ya vitamini zinasaidia kuima- risha mbegu za kiume na kuongeza uwezekano wa kutunga mimba. Yaani mbegu za kiume zinasa- firishwa kwenda katika nyumba ya uzazi kwa msaada wa baadhi ya vi- tamini.

Protini na madini

Tende ina protini kiasi cha asil- imia 2.5 na madini asilimia 2.1 (Calcium, Phosphorus, Chuma). Protini ni muhimu kwa ukuaji na ukarabati wa mwili na viungo vilivyo ndani yake. Kwa waoto wa- dogo protini ni muhimu sana kwa ukuwaji wa watoto hao. Mafuta kidogo Tende ina kiasi kidogo cha ma- futa (0.4%) ili kukidhi haja ya mwili na haina aina mbaya ya ma- futa inayoitwa cholesterol. Mafuta yana kazi nyingi mwil- ini, zikiwemo kutoa nguvu na kutengeneza vitu fulani. Choles- terol pia ina kazi muhimu katika mwili, ila mafuta hayo yasiwe mengi. Yakiwa mengi, yanasababi- sha maradhi kama vile ya moyo, kiharusi (stroke), unene na presha.

Nyuzi nyuzi

Zaidi ya neema hizo alizoumba Allah, tende ina nyuzi nyuzi za kil- ishe (dietary fibres) kiasi cha asil- imia 3.9%. Nyuzi nyuzi hizi zina faida kubwa katika mwili wa mwa- nadamu. Kwanza zinanyonya sumu kutoka tumboni na kuitoa nje pamoja na kinyesi. Pili, tende zinasaidia mtu kupa- ta choo kikubwa mara kwa mara na hivyo kumnusuru na tatizo la kukosa choo na ugonjwa wa kansa ya utumbo.

Tende kama dawa

Kwa upande wa faida ya tende kama dawa kwa ufupi ni kuwa tende inasaidia kuondoa tatizo la tumbo kuuma.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close