2. Afya

Kufunga Kunapunguza Athari za Uzee

SAN FRANCISCO

Kufunga kwa siku tano kila mwezi kunaweza kupunguza athari ya kuzeeka na kusaidia kupambana na baadhi ya maradhi kama shinikizo la damu, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti mpya yaliyotangazwa hivi karibuni. Utafiti huo uliofanyika huko San Fransisco, Marekani ulishirikisha watu 100 ambapo nusu walikula kama kawaida kwa sehemu kubwa ya mwezi lakini katika siku tano mfululizo walipunguza kula kama watu wanaofunga, zoezi ambalo walilifanya kwa miezi sita mfululizo. Washiriki hao wengi wao walikuwa ni wenye uzito mkubwa. Washiriki wengine 50 kati ya 100 walikula kama kawaida. Mwisho wa utafiti huo, kundi la waliokuwa wakipunguza kula kwa siku tano walipunguza wastani wa kilogramu 2.6. Kupungua uzito haikuwa faida pekee bali pia watafiti waligundua kuwa shinikizo la damu pia lilipungua. Utafiti huo ulifadhiliwa na Taasisi ya Taifa ya Uzee na Taasisi ya Taifa ya Kansa na matokeo yake kuchapishwa katika Jarida moja liitwalo, ‘Journal Science Translational Medicine’. Utafiti huo uliongozwa na wanasayansi kutoka katika Chuo cha Southern California.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close