2. Afya

Dalili na magonjwa yanayohusiana na ujauzito

Mpenzi msomaji karibu tena katika muendelezo wa makala yetu ya dalili na magonjwa mbalimbali yanayohusiana na ujauzito.

Kwa kujikumbusha, katika makala iliyopita tuliangazia kwa undani dalili tofauti zinazoashiria uwepo wa ujauzito. Dalili hizo ni pamoja na kukosa hedhi, maumivu ya kichwa, kupata kiungulia, mabadiliko ya matiti, kupata homa na kutapika, kupata choo kidogo mara kwa mara, maumivu ya mgongo na nyonga, kukosa choo, kutoka chunusi, kuongeza uzito, kukosa usingizi pamoja na kupata msongo wa mawazo. Ndugu msomaji, katika makala hii tutajadili kwa undani ugonjwa wa shinikizo la damu la ujauzito, dalili pamoja na madhara yake kwa mama na mtoto.

Shinikizo la damu ni moja kati ya magonjwa yanayoweza kujitokeza kwa mama mjamzito ambaye hakuwa na tatizo hili kabla ya kushika mimba. Kwa kawaida, tatizo hili huanza wakati mimba ikiwa na umri wa miezi mitano na hudumu hadi mwisho wa 40 baada ya kujifungua.

Maana na aina za shinikizo la damu

Shinikizo la damu limegawika katika makundi tofauti. Makundi haya yanajumuisha shinikizo la damu la kawaida (PIH), shinikizo la damu sugu (chronic HTN), shinikizo la damu linaloambatana na kuharibika kwa figo (preeclampsia) na shinikizo la damu linaloambatana na kifafa au kupoteza fahamu (eclampsia/kifafa cha mimba). Ikiwa hautachukuliwa hatua, ugonjwa huu huweza kuleta madhara makubwa sana kwa mama na mtoto, ikiwemo kusababisha vifo kwao.

Watu waliohatarini kupata ugonjwa huu

Si kila mjamzito hupata ugonjwa wa shinikizo la damu. Ugonjwa huu huweza kujitokeza zaidi kwa wanawake ambao wameshika ujauzito kwa mara ya kwanza, wenye umri chini ya miaka 18 au miaka zaidi ya 35, wenye mimba ya mapacha, waliowahi kupata tatizo hili kwenye mimba za nyuma, wakina mama waliyo na kisukari pamoja na wakina mama walio na magonjwa ya figo.

Shinikizo la damu la kawaida

Kwa kitaalamu ugonjwa huu hujulikana kama ‘PIH’. PIH ni hali ya kuongezeka kwa shinikizo la damu baada ya miezi mitano ya ujauzito (ikiwa litakuwepo kabla ya miezi hii litaitwa shinikizo la damu sugu). Ingawa shinikizo hili huwa kubwa, halisababishi madhara mengine katika viungo vya mama mjamzito. Utaona dalili chache tu kama maumivu ya kichwa na moyo kuenda mbio.

Shinikizo la damu la na madhara katika figo

Ikiwa shinikizo la damu la kawaida halitachukuliwa hatua, huweza kuharibu figo.Hali hii hujulikana kama ‘preeclampsia’ na hujitokeza baada ya miezi mitano ya ujauzito. Dalili kuu za shinikizo la damu linaloambatana na madhara katika figo ni kuvimba miguu na kukojoa mkojo wenye mapovu mengi. Pia tatizo hili hujitokeza zaidi kwenye mimba za kwanza.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close