2. Afya

Covid-19 Hatari Maradufu Inapokutana na Kisukari

Wakati ugonjwa wa virusi vya corona au COVID19 ukiendelea kutikisa dunia katika wimbi la tatu, Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) wagonjwa wa kisukari wameendelea kuwa waathirika wakubwa zaidi, wengi wao wakipoteza maisha. Kutokana na hali hiyo, WHO imeendelea kutoa ushauri kwa wagonjwa wa Kisukari juu ya namna kujikinga dhidi corona, maradhi ambayo yametikisa dunia kwa miaka miwili mfululizo sasa.

Hali ya Kisukari duniani

Kwa mujibu wa Dkt Gojka Roglic wa WHO, ugonjwa wa kisukari umeendelea kusambaa duniani kote katika kipindi cha miaka 30 na hivi sasa kuna zaidi ya watu milioni 400 ambao wanaishi na ugonjwa huo duniani kote.

“Kwa bahati mbaya takribani nusu yao hawafahamu iwapo wana ugonjwa wa kisukari. Hawajaenda kupima. Na wale ambao tayari wameshapimwa na kubainika, wengi wao hawana dawa au huduma za matibabu wanayohitaji,” alisema Dokta Roglic.

Janga la corona limedhihirisha kuwa iwapo wataugua COVID – 19, wagonjwa wa kisukari wako katika hatari zaidi ya kuwa mahututi na hata kufariki dunia kuliko watu wasio na kisukari. Kuna aina mbili za kisukari, ‘aina ya 1’ na ‘aina ya 2’. Ingawa aina ya 2 ndiyo imesambaa zaidi duniani, wnaouhua aina ya 1 ndiyo wako hatarini zaidi kuwa mahututi na kufariki dunia iwapo watapata corona.

Mazoezi, lishe bora ni kinga kwa mgonjwa wa kisukari

Kwa mgonjwa wa kisukari, ni muhimu sana kijifunza namna ya kujikinga na corona au ukipata huathiriki sana.

Msingi mkuu ni mazoezi na lishe bora. Wagonjwa wa kisukari wanapaswa kuwa wabunifu katika mazoezi sambamba na lishe bora ndani katika mazingira ya sasa yenye vizuizi na vikwazo kutokana na COVID-19.

Pamoja na juhudi za wagonjwa wa kisukari, serikali nazo zinapaswa kusuka mifumo ya afya kwa namna ambayo wagonjwa wanaendelea kupata dawa zao kila wakati.

Hatua za kujikinga

Kinga ni bora kuliko tiba. Kwa kuzingatia kuwa wagonjwa wa kisukari wanatambuliwa kuwa wako hatarini zaidi kuugua kuliko watu wasio na kisukari, ni muhimu wazingatie hatua zote za kudhibiti kusambaa kwa COVID-19.

Hatua zimetajwa kuwa ni pamoja na kunawa mikono, kuvaa barakoa, kuhakikisha vyumba wanamoishi vina hewa ya kutosha, kuchangamana na watu maeneo ya wazi badala ya ndani na kuzingatia umbali unaopaswa kati ya mtu na mtu.

Halikadhalika kuna chanjo ambazo zimeshap – endekezwa na wagonjwa wa Kisukari ni kundi la kipaumbele. Kwa Tanzania, bahati iliyoje kwamba tayari mataifa kuchanja na tuomeo na athari zinazo- nasibishwa na kila aina ya chanjo. Wataalamu wa Kitanzania, baada ya kuzisoma vizuri, tayari wamepndekeza baadhi ya chanjo zitumike.

Ni nini sukari?

Sukari ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu inapokuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda murefu. Sukari hutumiwa na mwili ili kupata nishati-lishe. Ili mwili uweze kutumia sukari inayotokana na chakula huhitaji kichocheo (hormone) cha insulin. Kichocheo hiki hutengenezwa na kongosho (pancreas).

Kichocheo cha insulin ndicho kinachodhibiti kiwango cha sukari katika damu. Wakati kongosho linaposhindwa kutengeneza kichocheo cha insulin au insulini iliyopo katika damu inaposhindwa kufanya kazi kwa ufanisi husababisha ugonjwa wa kisukari.

Kuna juhudi nyingi zinafanyika hivi sasa kupambana na kisukari. Kwa mfano, mapema mwaka huu, Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO lilizindua mpango mpya wa kusongesha harakati za kukabiliana na ugonjwa huo, ikiwa ni miaka 100 tangu kugunduliwa kwa Insulin.

Uzinduzi huo ulifanyika wakati wa mkutano wa dunia wa ugonjwa wa kisukari ulioandaliwa kwa pamoja na WHO, serikali ya Canada kwa msaada wa Chuo Kikuu cha Toronto.

Katika mkutano h u o, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus alielezea umuhimu wa kuchukua hatua dhidi ugonjwa wa kisukari sasa kuliko wakati wowote ule.

Dkt Ghebreyesus alisema: “Idadi ya wagonjwa wa kisukari imeongezeka mara nne katika miongo minne iliyopita. Ni ugonjwa pekee usio wa kuambukiza ambao hatari ya kufa mapema inaongezeka kuliko kupungua.”

Dkt. Tedros amesema mpango huo mpya utasaidia kuchagiza utashi wa kisiasa katika kuongeza upatikanaji na ufikiaji wa matibabu kwa wagonjwa sambamba na taratibu za uchunguzi na kinga.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close