1. Habari1. TIF News

Zoezi la ugawaji wa msaada wa chakula Morogoro

TAASISI za Dar Al Ber Society na Dubai Charity Association kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu wameshirikiana kwa pamoja na Taasisi ya The Islamic Foundation kugawa msaada wa chakula kwa kaya 29 za Mkoa wa Morogoro.

Zoezi hilo la ugawaji wa msaada huo wa chakula limefanyika katika Makao Makuu ya Taasisi ya The Islamic Foundation hapa Mjini morogoro ambapo kaya 29 zimeweza kufaidika na msaada huo ambao utaweza kulisha familia ya watu watano mpaka sita kwa kipindi cha mwezi mmoja.

chakula moro 5
chakula moro 2

Aidha wanufaika wa msaada huo ni wajane ambao ndio walengwa waliokusudiwa na wahisani hao walioko Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kushirikiana na Taasisi ya The Islamic Foundation ya Mjini Morogoro.

Kufuatia ugawaji huo wa chakula Katibu Mkuu wa Taasisi ya The Islamic Foundation Sheikh Haruna Jumanne amesema kuwa huu ni muendelezo wa Taasisi ya The Islamic Foundation kuendelea kuaminika na wahisani hao ambapo kaya 29 zimeweza kunufaika na msaada huo wa chakula ukiwemo Mchele Kilogramu 20, Unga wa Ugali Kilogramu 20, Maharage Kilogramu 10, Sukari Kilogramu 5 na Mafuta ya Kula Lita 3 chakula ambacho kitaweza kulisha familia ya watu watano mpaka sita kwa kipindi cha mwezi mmoja.

chakula moro 5

Na hapa wanufaika wa msaada huo ambao ni wakina mama wajane kutoka Kaya 29 Ndani ya Manispaa ya Morogoro wameeleza kufuruhishwa kwao na msaada huo waliopatiwa na Taasisi za Dar Al Ber Society na Dubai Charity Association kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kushirikiana kwa pamoja na Taasisi ya The Islamic Foundation ambao utawapunguzia ugumu wa maisha wao pamoja na familia zao huku wakiziombea Dua njema Taasisi hizo kwa juhudi wanazozifanya.

chakula moro 4
Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close