1. TIF News

TIF ya wa zawadi wanafunzi 38 waliopata division 1 katika shule ya Forest Hill Secondary.

Katika kuhakikisha kiwango cha Taaluma kinazidi kuimarika kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Forest Hill Chini ya Taasisi ya The Islamic Foundation ya Mjini Morogoro,Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Aref Nahdi amekabidhi zawadi kwa wanafunzi 38 waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili .

Mwenyekiti Aref Nahdi amesema wanaamini kuwa kupitia zawadi hizo zitatoa motisha kwa wanafunzi kufanya vizuri ili kufikia kiwango cha taaluma kilicho kusudiwa na Uongozi wa shule pamoja na Taasisi za The Islamic Foundation.

Akikabidhi Zawadi hizo kwa wanafunzi hao waliofanya vizuri kwa kupata daraja la kwanza katika Mtihani wa Kujipima wa kidato cha Pili Mwenyekiti wa Taasisi wa The Islamic Foundation Aref Nahdi amesema kuwa siri ya mafanikio hayo ni ushirikiano ulipo miongoni mwao.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close