1. TIF News

TIF yasaidia TIPSO Mil 5, yampeleka mshindi Qur’an Umra

TAASISI ya The Islamic Foundation (TIF) imeahidi kuendelea kushirikiana na Umoja wa Shule za Msingi za Kiislamu nchini TIPSO ili kuwawezesha kufikia lengo lilokusudiwa.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Taasisi ya hiyo, Aref Nahdi, katika mashinadano ya 16 ya kuhifadhi Qur’an tukufu ya Tipso yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambako alialikwa kama mgeni rasmi.

Katika hotuba yake, Mwenyekiti Nahdi aliitaka TIPSO kujitangaza shughuli zake kupitia vyombo vya habari vya Imaan Media.

Katika hatua nyingine, Nahdi aliahidi kumpeleka Makka kwa ajili ya kufanya Umra mtoto aliyeibuka kinara katika mashindano hayo kwa kuhifadhi juzuu 30. Ofa hiyo pia itamhusu mzazi wa mtoto huyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TIPSO, Salim Babdee, amesema kuwa lengo la umoja huo ni kuunganisha shule zote za msingi za Kiislamu na kwamba wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, ingawa bado kuna kazi kubwa inatakiwa kufanyika ili shule nyingi zaidi zijiunge na umoja huo.

Naye mlinganiaji wa dini tukufu ya Kiislam Sheikh Mussa Kundecha aliwataka wazazi kujimarisha katika misingi ya malezi ya dini ili kupatikane kizazi chema. Sheikh Kundecha alisema kuwa jamii bora inapatikana kwa wazazi kuzingatia maadili ya dini katika malezi yao.

Katika risala yao kwa mgeni rasmi, taasisi hiyo ya TIPSO ilitaja changamoto za aina mbalimbali wanazokabiliana nazo. Kutokana na changamoto hizo, Mwenyekiti Nahdi alitoa shilingi milioni tano kuisaidia Tipso.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close