1. TIF News

TIF yasaidia jeshi la polisi tairi za gari

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limeishukuru taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) kwa msaada wa magurudumu sita kwa ajili gari la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha jeshi hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIF, Sheikh Ibrahim Twaha Ibrahim alikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mwenyekiti wake Arif Nahdi katika hafla iliyofanyika makao makuu ya kitengo hicho cha FFU mjini Morogoro.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim, Afisa Mnadhimu wa jeshi hilo Sospeter Kungura amesema huo ni msaada mkubwa kwao kwani utawawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

Aidha, aliomba taasisi hiyo kuzidi kuwasaidia katika changamoto mbalimbali kwani wamekuwa msaaada mkubwa kwa jamii ya mkoa wa Morogoro na kwa nchi kwa ujumla

Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo wa The Islamic Foundation alisema kuwa wanathamini mchango wa jeshi la polisi katika kulinda amani na wataendelea kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali za jeshi hilo.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close