1. TIF News

TIF yaijengea BAKWATA msikiti wa kisasa Kilosa

Katika ishara ya kudumisha mahusiano mema ya kitaasisi na umma wa Kiislamu, taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) imekabidhi msikiti mkubwa na wa kisasa kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) uliopo eneo la Kidodi wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Makabidhiano hayo yamekuja baada ya TIF kukamilisha ujenzi wa msikiti huo ambao walifadhili ujenzi wake kwa kushirikiana na Jumuiya ya Dar al Ber Society ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Majid Mwanga, aliyezindua msikiti huo, ambapo alitumia fursa hiyo kupongeza TIF kwa kuwa mstari wa mbele kuendeleza dini tukufu ya Kiislamu na kusaidia jamii.

Akiwanasihi Waumini wa msikiti huo, DC Mwanga aliwataka wazazi kuweka mkazo katika kuwapa watoto wao elimu ya dini ili kujenga kizazi chema. Alisema, ili misikiti itumike ipasavyo, vijana wanatakiwa waandaliwe ili wawe Waumini wema.

Pia DC huyo alitoa wito kwa vijana kujifunza na kutumia elimu ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika kupeleka mbele dini tukufu ya Kiislamu na sio mambo maovu. Moja ya vipengele muhimu vya elimu hiyo ni matumizi ya mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikitumika vibaya miongoni mwa baadhi ya Watanzania.

Naye Mwenyekiti wa The Islamic Foundation, Aref Nahdi alisema kuwa licha ya kukamilika kwa msikiti huo, pia watachimba kisima kirefu Ili kuondosha adha na kero ya maji kwa Waumini wa msikiti huo na wakazi wa eneo hilo.

Tangu kuanzishwa kwake, TIF imekuwa mstari wa mbele katika kusaidiana na serikali katika kutoa huduma za kijamii kwa Watanzania ikiwemo katika sekta mbalimbali hususan afya, elimu na maji.

Nao Waumini wa kata ya Kidodi walishukuru uongozi wa TIF kwa ufadhili wa ujenzi wa msikiti huo na kuiombea dua TIF izidi kufanya mambo makubwa kwa maslahi ya Watanzania.

Kwa upande wake, mlezi wa TIF, mzee Salum Mdula aliwataka Waislamu wa eneo hilo kuutunza msikiti huo kwa kuhakikisha unakuwa katika hali nzuri kipindi chote

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close